Hadithi: Wakili wa moyo

Hadithi: Wakili wa moyo

Yani hadithi tamuu . Namuonea huruma Mage kuutupa moyo wake kwa mara ya pili...sijui atapona na maumivu kwa Collin kama alivyoahidi.....Haya huyu Cecy jamani hadi huruma ..tuache utqni mapenzi mabaya.. Lakini mapenzi hayachagui tajiri au maskini. Ngoja tusubiri..fanya fasta mkuu ladha ya hadithi isipotee
 
Wakili wa Moyo - 18

MTUNZI: ALLY MBETU

ILIPOISHIA:
Mama yake alimweleza yaliyotokea muda mfupi, Cecy alishtuka sana kusikia habari zile.
"Mama yaani ndiyo kasema hivyo! Hayo mapenzi na mwanaye yameanza lini?"

"Sijui."
"Mama namfuata sasa hivi anieleze kuja kututukana bila sababu, kama umaskini wetu tumeridhika nao."
SASA ENDELEA...

"Hapana mwanangu mwenye nguvu mwache apite."

"Si kwa hilo, wameniumiza bado wananifuatafuata," Cecy alisema kwa sauti ya kilio.

"Wee waache."

"Mama tukiwaacha watatuzoea, nimeacha kwenda kwao bado tu hawajaridhika mama niache akanithibitishie alichokisema. Ni kweli nampenda Colin lakini hatujatamkiana mambo ya mapenzi yeye kayatoa wapi?" Cecy alisema kwa jazba.

"Mwanangu jasho la mnyonge haliendi joshi."

"Sawa, lakini Mungu yupo."

Cecy aliweka beseni lake na kwenda chumbani kwake akiwa amefura kwa hasira. Moyoni alijiapia siku akikutana na mama Colin siku hiyo atamkosea adabu kwa dharau aliyoifanya nyumbani kwao.

***

Familia mbili zilikutana kupanga tarehe ya harusi ya watoto wao. Kila mmoja alitaka kufanyika harusi ya kifahari kutokana na watoto wao kuwa wa kwanza kuoa na kuolewa katika familia zao.
Baada ya makubaliano ya tarehe ya ndoa, waliwataarifu watoto wao kilichokuwa kikiendelea juu ya ndoa yao.
Mara moja zilisambazwa taarifa kwa ndugu na jamaa kwa kupewa kadi na wengine kuhudhulia vikao vya maandalizi ya harusi vilivyoanza mara moja.

Mage alipanga picha zake za harusi kuzisambaza katika mitandao yote ili kumuonesha Hans naye ana watu wanaompenda kwa dhati kuliko yeye aliye upasua moyo wake kwa kisu butu bila ganzi.

Wakiwa katika Mgahawa wa Samaki Samaki Mlimani City walipokutana Mage na shoga yake kipenzi Brenda kwa ajili ya kula raha, baada ya kutafuna kipande cha piza na kusukumia na juisi ya embe, alisema:
"Brenda yaani sijui siku ya harusi yangu itakuwaje?"

"Mage, litakuwa bonge la harusi ambalo halijawahi kutokea jijini. Mama yako alivyopania, sijui!"

"Yaani, baada ya ndoa wakati tupo honey moon nitazisambaza picha za harusi mitandao yote ili kuwakonga wavimba macho walionicheka baada ya Hans kuoa."

"Najua Hans ataumia sana,"Brenda alisema huku akikata kipande cha piza.

"Aumie nini wakati amefurahia, lakini Mungu yupo. Kisasi changu kwake hakijaisha ningekuwa na uwezo ningemmwagia tindi kali," Mage alisema huku akikunja uso kwa hasira.

"Magee! Tindi kali ya nini ikiwa tayari umepata mtu mwenye mapezi ya kweli?"

"Brenda hujui tu jinsi nilivyoumia kwa kitendo cha Hans kuniharibia ndoto zangu za maisha."

"Mage bado unampenda Hans!"

"Aah, wapi!"Mage aliruka kimanga.

"Muongo unampenda na akitokea leo haki ya nani ndoa hakuna," Brenda alimwambia shoga yake akiwa amemkazia macho.

"Haitatokea hata siku moja, labda jua litoke Magharibi kwenda Mashariki."

"Unajikomba tu, lakini upo na Colin kama bodi lakini injini ni Hans."

"Mawazo yako, kwanza tuachane na mambo ya Hans tuzungumzia harusi yangu."

"Kama kweli umedhamiria kuolewa na Colin basi litakuwa bonge la harusi."

Wakiwa katikati ya mazungumzo, simu ya Brenda iliita. Alipoangalia alikuta namba ngeni alipokea.
"Haloo."

"Haloo Brenda."

"Abee, nani mwenzangu?"

"Yaani nawe umenichukia kama shoga yako, Brenda nimekukosea nini?"

Sauti ile ilimshtua na kugundua anazungumza na Hans.

"Jamani shemu mambo mengi si unajua mitihani ilitukamata."

"Pamoja na mitihani, lakini umenitenga shemeji yangu!"

"Siwezi kukutenga."

"Naomba msaada wa kunikutanisha na Mage, kuna tetesi zimeniumiza moyo wangu. Usishangae wakati wowote ukisikia kifo changu."

"Brenda unazungumza na nani?" Mage aliingilia kati mazungumzo kwa kusimama na kusogea kwa Brenda.

"Mage hebu subiri,"Brenda alimtuliza Mage na kuendelea kuzungumza.

" Kipi tena kitasababisha kifo chako, unaumwa?"

"Heri ningeumwa kuliko ukatili anaonifanyia shoga yako. Anajua mimi na yeye tumetoka wapi na tuliahidiana nini. Kweli Mage unakubali kuolewa na mwanaume mwingine tofauti na mimi?" Hans alisema kwa sauti ya huzuni.

"Hans utakuwa unakosea kusema hivyo, wewe ndiye uliyesababisha yote. Ulikuwa ukifahamu Mage alikuwa akikupenda kiasi gani na unajua nini kilimpata baada ya wewe kufunga ndoa?"

"Najua, lakini nilimweleza kila kitu."

"Mbona ulikwenda kinyume?"

"Nilikuwa na sababu yangu ambayo Mage alitakiwa kunisikiliza na kuelewa sababu ya mimi kufanya vile wala asingefikia huko."

"Hans usimlaumu Mage kwa vile naye kafanya kama wewe."

"Kivipi?"

"Mume katafutiwa na mama yake."

"Duh! Haijawahi kutokea."

"Basi imetokea."

"Basi naomba anipe nafasi ya kuzungumza naye kwa dakika chache."

"Sidhani kama anaweza kupata nafasi kwa muda huu wa maandalizi ya harusi."

"Najua, ila nilikuwa nataka kuzungumza naye hata dakika kumi kabla ya ndoa yake."

"Hans, hiki si kipindi cha kuzungumza chochote na Mage, unaweza kuivuruga ndoa yake."

"Siwezi, nataka tu nizungumze naye ili akiolewa ajue mimi si adui yake."

"Mmh! Nitafikisha ujumbe."

"Naomba shemeji yangu unikutanishe na Mage nitakupa zawadi yoyote unayotaka."

"Sawa shemu."

"Nashukuru kwa kunisikiliza pia wewe ni daraja muhimu kati yangu na Mage."

"Nimekuelewa."

Brenda alikata simu na kumgeukia shoga yake aliyekuwa na kumuhemuhe cha kutaka kujua Hans alikuwa akisemaje.

"Vipi mzushi alikuwa akisemaje?"

Itaendelea...................
 
Dah. Mage anaingia majaribuni...-Hans asije mvuruga mwenzie jamani. tunaaubiri.:'(....:-(...
 
Wakili wa Moyo-19

ILIPOISHIA:
"Nimekuelewa."
Brenda alikata simu na kumgeukia shoga yake aliyekuwa na kimuhemuhe cha kutaka kujua Hans alikuwa akisemaje.
"Vipi mzushi alikuwa akisemaje?"

SASA ENDELEA...

Brenda alimweleza mazungumzo yote waliyozungumza na Hans.

"Mmh! Anataka kuniambia nini?"

"Sijui, wewe ndiyo unajua mlizungumza nini katika ahadi ya penzi lenu."

"Uhuu!" Mage alishusha pumzi na kusema:

"Brenda unanishauri nini?" Mage alionekana kama ametahayari kusikia taarifa za Hans.

"Kwa vile upo katika hatua nzuri za harusi, huu si muda wa kuzungumza na Hans unaweza kuharibu kila kitu ukakosa bara na pwani," Brenda alimtahadharisha rafiki yake.

"Eti eeh, sijui Hans anataka kuniambia nini?"

"Achana naye."

"Mmh! Sawa."

Kwa vile muda ulikuwa umekwenda sana, kila mmoja aliingia kwenye gari lake kurudi nyumbani.

***

Brenda alipofika nyumbani kwao alikwenda kuoga na kupata chakula kisha alijifungia chumbani kwake na kuwasha Ipad yake na kuanza kuchati na marafiki zake kwenye Twiter na Skype.
Akiwa anaendelea kuchati simu yake iliita, namba ilikuwa ngeni aliipokea.

"Haloo."

"Haloo Brenda."

"Abee, nani?"

"Brenda unaniuliza nani wakati tumetoka kuzungumza muda si mrefu."

"Hans?" Brenda aliuliza.

"Ndiyo."

"Unasemaje?"

"Brenda samahani sana."

"Bila samahani."

"Naomba unikutanishe leo na Mage."

"Hans, si tumeisha ongea?"

"Hapana Brenda, kuna kitu cha muhimu sana nataka nizungumze naye kabla siku ya kesho."

"Samahani Hans, nipo Bagamoyo sitarudi leo."

"Naomba hata umpigie simu ili anisikilize hata kwa sekunde tano tu."

"Hans kwanza samahani, hapa nipo na boy friend wangu, ana wivu sana naomba tuzungumze kesho," Brenda alidanganya.

"Samahani, ila utakacho kisikia kesho usishangae najua Mage atafurahi."

"Unataka kufanya nini Hans?"

"Nilitakiwa kumweleza Mage mwenyewe, kwa heri."

Hans alikata simu na kumfanya Brenda abakie na simu mkononi kama anatazama kitu cha kumshangaza. Alijikuta akijiuliza.

"Hans anataka kufanya nini? Au anataka kujiua? Mmh! Ngoja nimweleze Mage maana sasa imekuwa kazi. Lakini kipi cha ajabu Mage akiolewa? Kwani alitaka akae vile mpaka lini? Hivi Hans ana shida na Mage au anataka kumvurugia maisha tu."

Brenda alijikuta akiwaza peke yake, wakati huo simu aliyopiga ilikuwa ikiita. Ilipokelewa upande wa pili.

"Haloo shoga lete stori," Mage alipokea.

"Mmh! Mtu wako ananisumbua sana."

"Nani?"

"Hans."

"Kakupigia tena?" Mage alishtuka.

"Ndiyo."

"Brenda achana naye, kwa nini unamsikiliza?"

"Mage siwezi kumkatia simu kwa vile sina mgomvi naye."

"Yaani hivi najiandaa kwenda kwa Colin, tulikuwa tuna chati tukaona haitoshi, tukaongea vilevile tukaona haitoshi, nimeamua kwenda kabisa kuonana naye uso kwa macho."

"Duh!"

"Brenda, nimeamini Colin ananipenda sana."

"Sasa ndiyo utulie."

"Brenda, lazima nitulie Colin kaniahidi vitu vingi sana baada ya ndoa. Nina imani ndoto zangu nilizoziota kwa Hans zitakuwa mara kumi."

"Basi ndiyo hivyo mtu wako, roho ya Mungu anatapatapa kama mfa maji."

"Kwani alikuwa akisemaje?"

Brenda alimweleza yote aliyoelezwa na Hans na alivyomdanganya, Mage baada ya kumsikiliza alishusha pumzi na kusema:
"Kwani Hans anataka kuniambia nini?" Mage aliuliza.

"Akwambie nini! Yule mharibifu, huu si muda wa kumsikiliza, ukirogwa kumsikiliza tu ndoa huna."

"Mmh! Nimekuelewa japo moyo unatamani kumsikiliza ili nijue anataka kusema nini?"

"La kusema hakosi, anaweza kukuvuruga akili na ndoa yako ukaiona chungu. Najua bado unampenda sana Hans, kama utampa nafasi narudia tena ndoa hakuna," Brenda alimtahadhalisha Mage.

"Hata siku moja, labda siyo Mage mimi. Siwezi kuumizwa mara ya tatu, mbili zinatosha."

"Basi ndiyo hivyo kuwa makini na Hans, kwa nini muda wote akae kimya, kusikia unataka kuolewa ndiyo ajifanye anakupenda sana."

"Nimekuelewa basi wacha niwahi kwa mahabuba wangu."

"Mambo si hayo."

Brenda alikata simu na kuendelea kuchati na mashoga zake.
***
Mlio wa simu ulimshtua Brenda aliyekuwa bado amelala. Alipoangalia ilikuwa namba ngeni, aliipokea.
"Haloo."

"Haloo, nazungumza na Brenda?"

"Ndiyo, nani mwenzangu?"

"Naitwa Ndubi rafiki mkubwa wa Hans."

"Ndiyo Ndubi."

"Kuna habari siyo nzuri."

"Habari gani?"

"Hans amepata matatizo makubwa sana, nilijaribu kumpigia Mage simu yake haipatikani nikaona nikupigie wewe ili umjulishe."

"Mmh! Matatizo gani?"

"Jana usiku wamevamiwa na majambazi nyumbani kwake. Mkewe na mwanaye wameuawa na yeye hatujui kama yupo hai."

"Mungu wangu! Yupo wapi kwa sasa?"

"Yupo Hospitali ya Muhimbili, chumba cha wagonjwa mahututi."

"Mungu wangu! Ngoja nimjulishe Mage."

"Itakuwa vizuri."

Baada ya simu kukatwa, Brenda alimpigia simu Mage aliyekuwa bado yupo kwa mchumba wake Colin. Baada ya simu kuita kwa muda ilipokelewa upande wa pili.
"Haloo Brenda mbona unaharibu pozi za watu," Mage alisema kwa utani.

Brenda hakupoteza muda alimweleza taarifa aliyopokea asubuhi ile. Taarifa ile ilimshtua sana Mage.

"Mungu wangu! Yupo wapi?"

"Muhimbili."

"Nakuja sasa hivi twende."

"Noo, tutakutana hospitali."

Mage alinyanyuka kitandani na kupitia nguo zake na kuvaa bila kuoga.

Itaendelea..............
 
Mkuu endelea kutupa uhondo. Najua week end hutaweza kuendelea na hii hadithi.

Wakili wa Moyo-19

ILIPOISHIA:
“Nimekuelewa.”
Brenda alikata simu na kumgeukia shoga yake aliyekuwa na kimuhemuhe cha kutaka kujua Hans alikuwa akisemaje.
“Vipi mzushi alikuwa akisemaje?”

SASA ENDELEA...

Brenda alimweleza mazungumzo yote waliyozungumza na Hans.

“Mmh! Anataka kuniambia nini?”

“Sijui, wewe ndiyo unajua mlizungumza nini katika ahadi ya penzi lenu.”

“Uhuu!” Mage alishusha pumzi na kusema:

“Brenda unanishauri nini?” Mage alionekana kama ametahayari kusikia taarifa za Hans.

“Kwa vile upo katika hatua nzuri za harusi, huu si muda wa kuzungumza na Hans unaweza kuharibu kila kitu ukakosa bara na pwani,” Brenda alimtahadharisha rafiki yake.

“Eti eeh, sijui Hans anataka kuniambia nini?”

“Achana naye.”

“Mmh! Sawa.”

Kwa vile muda ulikuwa umekwenda sana, kila mmoja aliingia kwenye gari lake kurudi nyumbani.

***

Brenda alipofika nyumbani kwao alikwenda kuoga na kupata chakula kisha alijifungia chumbani kwake na kuwasha Ipad yake na kuanza kuchati na marafiki zake kwenye Twiter na Skype.
Akiwa anaendelea kuchati simu yake iliita, namba ilikuwa ngeni aliipokea.

“Haloo.”

“Haloo Brenda.”

“Abee, nani?”

“Brenda unaniuliza nani wakati tumetoka kuzungumza muda si mrefu.”

“Hans?” Brenda aliuliza.

“Ndiyo.”

“Unasemaje?”

“Brenda samahani sana.”

“Bila samahani.”

“Naomba unikutanishe leo na Mage.”

“Hans, si tumeisha ongea?”

“Hapana Brenda, kuna kitu cha muhimu sana nataka nizungumze naye kabla siku ya kesho.”

“Samahani Hans, nipo Bagamoyo sitarudi leo.”

“Naomba hata umpigie simu ili anisikilize hata kwa sekunde tano tu.”

“Hans kwanza samahani, hapa nipo na boy friend wangu, ana wivu sana naomba tuzungumze kesho,” Brenda alidanganya.

“Samahani, ila utakacho kisikia kesho usishangae najua Mage atafurahi.”

“Unataka kufanya nini Hans?”

“Nilitakiwa kumweleza Mage mwenyewe, kwa heri.”

Hans alikata simu na kumfanya Brenda abakie na simu mkononi kama anatazama kitu cha kumshangaza. Alijikuta akijiuliza.

“Hans anataka kufanya nini? Au anataka kujiua? Mmh! Ngoja nimweleze Mage maana sasa imekuwa kazi. Lakini kipi cha ajabu Mage akiolewa? Kwani alitaka akae vile mpaka lini? Hivi Hans ana shida na Mage au anataka kumvurugia maisha tu.”

Brenda alijikuta akiwaza peke yake, wakati huo simu aliyopiga ilikuwa ikiita. Ilipokelewa upande wa pili.

“Haloo shoga lete stori,” Mage alipokea.

“Mmh! Mtu wako ananisumbua sana.”

“Nani?”

“Hans.”

“Kakupigia tena?” Mage alishtuka.

“Ndiyo.”

“Brenda achana naye, kwa nini unamsikiliza?”

“Mage siwezi kumkatia simu kwa vile sina mgomvi naye.”

“Yaani hivi najiandaa kwenda kwa Colin, tulikuwa tuna chati tukaona haitoshi, tukaongea vilevile tukaona haitoshi, nimeamua kwenda kabisa kuonana naye uso kwa macho.”

“Duh!”

“Brenda, nimeamini Colin ananipenda sana.”

“Sasa ndiyo utulie.”

“Brenda, lazima nitulie Colin kaniahidi vitu vingi sana baada ya ndoa. Nina imani ndoto zangu nilizoziota kwa Hans zitakuwa mara kumi.”

“Basi ndiyo hivyo mtu wako, roho ya Mungu anatapatapa kama mfa maji.”

“Kwani alikuwa akisemaje?”

Brenda alimweleza yote aliyoelezwa na Hans na alivyomdanganya, Mage baada ya kumsikiliza alishusha pumzi na kusema:
“Kwani Hans anataka kuniambia nini?” Mage aliuliza.

“Akwambie nini! Yule mharibifu, huu si muda wa kumsikiliza, ukirogwa kumsikiliza tu ndoa huna.”

“Mmh! Nimekuelewa japo moyo unatamani kumsikiliza ili nijue anataka kusema nini?”

“La kusema hakosi, anaweza kukuvuruga akili na ndoa yako ukaiona chungu. Najua bado unampenda sana Hans, kama utampa nafasi narudia tena ndoa hakuna,” Brenda alimtahadhalisha Mage.

“Hata siku moja, labda siyo Mage mimi. Siwezi kuumizwa mara ya tatu, mbili zinatosha.”

“Basi ndiyo hivyo kuwa makini na Hans, kwa nini muda wote akae kimya, kusikia unataka kuolewa ndiyo ajifanye anakupenda sana.”

“Nimekuelewa basi wacha niwahi kwa mahabuba wangu.”

“Mambo si hayo.”

Brenda alikata simu na kuendelea kuchati na mashoga zake.
***
Mlio wa simu ulimshtua Brenda aliyekuwa bado amelala. Alipoangalia ilikuwa namba ngeni, aliipokea.
“Haloo.”

“Haloo, nazungumza na Brenda?”

“Ndiyo, nani mwenzangu?”

“Naitwa Ndubi rafiki mkubwa wa Hans.”

“Ndiyo Ndubi.”

“Kuna habari siyo nzuri.”

“Habari gani?”

“Hans amepata matatizo makubwa sana, nilijaribu kumpigia Mage simu yake haipatikani nikaona nikupigie wewe ili umjulishe.”

“Mmh! Matatizo gani?”

“Jana usiku wamevamiwa na majambazi nyumbani kwake. Mkewe na mwanaye wameuawa na yeye hatujui kama yupo hai.”

“Mungu wangu! Yupo wapi kwa sasa?”

“Yupo Hospitali ya Muhimbili, chumba cha wagonjwa mahututi.”

“Mungu wangu! Ngoja nimjulishe Mage.”

“Itakuwa vizuri.”

Baada ya simu kukatwa, Brenda alimpigia simu Mage aliyekuwa bado yupo kwa mchumba wake Colin. Baada ya simu kuita kwa muda ilipokelewa upande wa pili.
“Haloo Brenda mbona unaharibu pozi za watu,” Mage alisema kwa utani.

Brenda hakupoteza muda alimweleza taarifa aliyopokea asubuhi ile. Taarifa ile ilimshtua sana Mage.

“Mungu wangu! Yupo wapi?”

“Muhimbili.”

“Nakuja sasa hivi twende.”

“Noo, tutakutana hospitali.”

Mage alinyanyuka kitandani na kupitia nguo zake na kuvaa bila kuoga.

Itaendelea..............
 
Mkuu endelea kutupa uhondo. Najua week end hutaweza kuendelea na hii hadithi.

Sawa mkuu nimekuelewa; tukutane jioni tena muda huu majukumu nayo yamebana hapa.

Tupo pamoja.
 
Sawa mkuu nimekuelewa; tukutane jioni tena muda huu majukumu nayo yamebana hapa.

Tupo pamoja.

Teh teh hata haya ni majukumu mzeee...huwezi kuja kututia genye alafu ukaondoka hvi hvi
 
Wakili wa Moyo - 20

ILIPOISHIA:
Brenda hakupoteza muda alimweleza taarifa aliyopokea asubuhi ile. Taarifa ile ilimshtua sana Mage.
"Mungu wangu! Yupo wapi?"
"Muhimbili."
"Nakuja sasa hivi twende."
"Noo, tutakutana hospitali."
Mage alinyanyuka kitandani na kupitia nguo zake, akavaa bila kuoga.
SASA ENDELEA...

Hakutaka kumwamsha Colin aliyekuwa bado amepitiwa na usingizi. Alitoka hadi kwenye gari lake na kuondoka kuelekea Muhimbili kumuona Hans.

Njia nzima alijilaumu kukataa kusikiliza wito wa Hans kwa kuamini kuna kitu cha muhimu alitaka kumueleza.

Alijiuliza Hans alitaka kumweleza nini na kwa nini alilazimisha waonane usiku wa jana yake kisha asubuhi asikie habari kama zile za kushtusha!

"Mungu wangu kama Hans atakuwa amekufa atakufa na kinyongo. Sikutakiwa kuwa katili kiasi kile. Japokuwa sikuwa tayari kurudiana naye lakini nilitakiwa kumsikiliza."

Mage alikuwa kwenye lindi la mawazo juu ya Hans kuwa katika hali ile. Alijikuta akitokwa na machozi kumlilia. Alijiuliza kama yeye ndiye angekuwa mke wa Hans na tukio lile likatokea ina maana angekufa yeye.

Kutokana na mawazo mengi alijikuta akiendesha gari pasipo kuwa na umakini. Alifunga breki mbele ya gari lililosimama baada ya taa nyekundu kuwaka katika makutano ya barabara za Ocean na Upanga.

Alikanyaga breki kwa nguvu zote huku akifumba macho na kuuma meno. Gari lilisota na kwenda kujigonga kidogo kwenye gari aina ya Land Cruser aliloendesha Mwarabu.

Kelele za breki zilifanya watu wote kugeuka kuangalia, askari wa barabarani alifika lakini Mwarabu hakutaka kesi kwa vile gari lake halikuharibika sehemu yoyote. Askari alimfuata Mage kumuuliza:

"Vipi mbona hivyo?"

Mage alishindwa kumjibu kwa vile presha ilikuwa juu na uso ulikuwa umejaa machozi. Askari hakutaka kumuhoji kitu, alimruhusu kuondoka. Mage aliondoa gari kuingia barabara ya Upanga kuelekea Muhimbili kumuona Hans.

Njia nzima Mage alikuwa akilia, alikumbuka maisha aliyoishi na Hans, mwanaume akiyempenda kuliko kitu chochote chini ya jua.

Waliishi maisha ya mapenzi kama njiwa, kila mmoja alimpenda mwenzake penzi la glasi halikuwa na kificho kila mmoja aliamini anapendwa na mwenzake.

Alikumbuka ahadi ya Hans alipomwambia kumuacha yeye ni sawa na roho kuachana na mwili. Alimhakikisha yeye ndiye mwanamke wa maisha yake.

Baada ya Hans kuozwa kwa shinikizo la wazazi, walikubaliana avumilie ili baadaye amuache mwanamke wa kulazimishwa ikiwa pamoja na kutozaa naye.

Lakini Hans alionekana kugeuka pale alipopata mtoto ndani ya ndoa yake, tofauti na walivyokubaliana kutozaa na yule mwanamke na kwenda kinyume na kumfanya naye akubali kuolewa na Colin.

Alijiuliza nani aliyefanya kitendo kile, alijikuta akitengeneza mawazo ya kijinga kuwaza labda mpango ule kaufanya Colin kutokana na wasiwasi wa kurudiana na Hans.

"Nikigundua Colin kama ndiye aliyemuua mpenzi wangu, nitamchukia mpaka kufa na nitakuwa shahidi namba moja kuhakikisha na yeye ananyongwa," Mage aliwaza.

Alipofika Muhimbili alisimamisha gari na kuelekea kwenye wadi ya wagonjwa mahututi. Nje ya wadi aliikuta familia ya Hans, hakuna aliyemjali japokuwa alionekana amevimba macho kutokana na kumlilia Hans.

Alipojaribu kuingia wadini alikatazwa na kuamua kusimama pembeni peke yake, baada ya muda shoga yake Brenda alifika na kwenda aliposimama.

"Vipi shoga?"

"Yaani mama Hans kanifukuza kama mbwa!"

"Kwa nini?"

"Hata sijui wakati anafahamu mimi na mwanaye tulikuwa vipi."

"Kwa hiyo hujui hali ya Hans?"

"Sijui chochote."

Mara simu ya Mage iliita alipoangalia ilikuwa ikitoka kwa Colin, aliitazama na kukunja uso bila kuipokea. Brenda aliyekuwa akimtazama usoni, alimuuliza.

"Simu ya nani?"

"Achana nayo," alijibu kwa mkato.

"Mmh!"

Baada ya muda simu iliita tena, Brenda alishtuka kuona jina la Colin bila kupokelewa.

"Shoga mbona hupokei?"

"Achana naye."

"Ha! Wewe si ulikuwa kwa Colin na umeondokaje?"

"Sijamuaga nimemuchana bado amelala."

"Unajua unachokifanya unaiweka ndoa yako njia panda."

"Kwani asiponioa nitapungukiwa nini?" Mage alijibu huku akiibinua midomo.

"Mage, usipoteze muda wa Colin, kuamini unampenda kumbe upo naye kivuli tu."

"Brenda mwenye uamuzi wa kumpenda ninao mimi."

"Kwa hiyo Colin si chaguo lako?"

"Brenda huu si wakati wa kuzungumzia Colin zaidi ya kujua hali ya Hans ndiye aliyetuleta hapa."

"Mmh! Sawa."

***

Colin baada ya kushtuka usingizini alijua mpenzi wake yupo msalani au bafuni, lakini muda ulikatika bila kuonekana. Alikwenda msalani kumtafuta huku akimwita bila kupata jibu. Alitoka hadi nje na kumuuliza mlinzi.

"John umemuona shemeji yako?"

"Ametoka asubuhi sana, hakukuaga?"

"Ameniacha nimelala."

"Tena alionekana kama analia nilijua mmegombana."

"Hata sielewi kitu."

Colin alimpigia simu mchumba wake, lakini iliita bila kupokelewa. Alirudia zaidi ya mara tatu, vilevile haikupokelewa. Alijiuliza Mage amepatwa na nini, wasiwasi wake labda kwao kumetokea tatizo.
Aliingia ndani na kuvaa pensi na fulana, chini alivaa ndala na kuingia kwenye gari kuelekea Kigamboni kwa kina Mage ili ajue amepatwa na nini.

Alikimbiza gari, kutokana na foleni aliamua gari lake kulipaki Posta ya zamani na kuchukua bodaboda ili awahi kufika. Baada ya kuvuka alichukua nyingine iliyo mpeleka nyumbani kwao Mage.
Alimlipa dereva na kuingia ndani ya geti, alipofika sebuleni alimkuta msichana wa kazi akifanya usafi.

"Habari Sofi?"

"Nzuri shemu, shikamoo."

"Marahaba, vipi Mage yupo?"

"Sijamuona toka asubuhi."

"Mama?"

"Yupo chumbani kwake."

"Kaniitie."

Colin alibakia sebuleni kumsubiri mama Mage, baada ya muda alitokea na kushangaa kumuona Colin katika hali ile.

"Vipi baba, kwema?"

"Kwema, sijui hapa."

"Hapa hatujambo, mwenzio yupo wapi?" mama Mage alimuulizia mwanaye baada ya kumuona Colin peke yake.

Itaendelea..........
 
Naombea toleo lijalo Colin apewe upeo wowote ikiwezekana hata Brenda ampigie simu kisirisiri Colin amfahamishe mahala walipo ili na yeye(Colin) aende Muhimbili wakutane na Mage ambae amekuwa akidharau simu za Colin, sipati picha Mage atakavyotahayari
 
Wakili wa Moyo - 20

ILIPOISHIA:
Brenda hakupoteza muda alimweleza taarifa aliyopokea asubuhi ile. Taarifa ile ilimshtua sana Mage.
“Mungu wangu! Yupo wapi?”
“Muhimbili.”
“Nakuja sasa hivi twende.”
“Noo, tutakutana hospitali.”
Mage alinyanyuka kitandani na kupitia nguo zake, akavaa bila kuoga.
SASA ENDELEA...

Hakutaka kumwamsha Colin aliyekuwa bado amepitiwa na usingizi. Alitoka hadi kwenye gari lake na kuondoka kuelekea Muhimbili kumuona Hans.

Njia nzima alijilaumu kukataa kusikiliza wito wa Hans kwa kuamini kuna kitu cha muhimu alitaka kumueleza.

Alijiuliza Hans alitaka kumweleza nini na kwa nini alilazimisha waonane usiku wa jana yake kisha asubuhi asikie habari kama zile za kushtusha!

“Mungu wangu kama Hans atakuwa amekufa atakufa na kinyongo. Sikutakiwa kuwa katili kiasi kile. Japokuwa sikuwa tayari kurudiana naye lakini nilitakiwa kumsikiliza.”

Mage alikuwa kwenye lindi la mawazo juu ya Hans kuwa katika hali ile. Alijikuta akitokwa na machozi kumlilia. Alijiuliza kama yeye ndiye angekuwa mke wa Hans na tukio lile likatokea ina maana angekufa yeye.

Kutokana na mawazo mengi alijikuta akiendesha gari pasipo kuwa na umakini. Alifunga breki mbele ya gari lililosimama baada ya taa nyekundu kuwaka katika makutano ya barabara za Ocean na Upanga.

Alikanyaga breki kwa nguvu zote huku akifumba macho na kuuma meno. Gari lilisota na kwenda kujigonga kidogo kwenye gari aina ya Land Cruser aliloendesha Mwarabu.

Kelele za breki zilifanya watu wote kugeuka kuangalia, askari wa barabarani alifika lakini Mwarabu hakutaka kesi kwa vile gari lake halikuharibika sehemu yoyote. Askari alimfuata Mage kumuuliza:

“Vipi mbona hivyo?”

Mage alishindwa kumjibu kwa vile presha ilikuwa juu na uso ulikuwa umejaa machozi. Askari hakutaka kumuhoji kitu, alimruhusu kuondoka. Mage aliondoa gari kuingia barabara ya Upanga kuelekea Muhimbili kumuona Hans.

Njia nzima Mage alikuwa akilia, alikumbuka maisha aliyoishi na Hans, mwanaume akiyempenda kuliko kitu chochote chini ya jua.

Waliishi maisha ya mapenzi kama njiwa, kila mmoja alimpenda mwenzake penzi la glasi halikuwa na kificho kila mmoja aliamini anapendwa na mwenzake.

Alikumbuka ahadi ya Hans alipomwambia kumuacha yeye ni sawa na roho kuachana na mwili. Alimhakikisha yeye ndiye mwanamke wa maisha yake.

Baada ya Hans kuozwa kwa shinikizo la wazazi, walikubaliana avumilie ili baadaye amuache mwanamke wa kulazimishwa ikiwa pamoja na kutozaa naye.

Lakini Hans alionekana kugeuka pale alipopata mtoto ndani ya ndoa yake, tofauti na walivyokubaliana kutozaa na yule mwanamke na kwenda kinyume na kumfanya naye akubali kuolewa na Colin.

Alijiuliza nani aliyefanya kitendo kile, alijikuta akitengeneza mawazo ya kijinga kuwaza labda mpango ule kaufanya Colin kutokana na wasiwasi wa kurudiana na Hans.

“Nikigundua Colin kama ndiye aliyemuua mpenzi wangu, nitamchukia mpaka kufa na nitakuwa shahidi namba moja kuhakikisha na yeye ananyongwa,” Mage aliwaza.

Alipofika Muhimbili alisimamisha gari na kuelekea kwenye wadi ya wagonjwa mahututi. Nje ya wadi aliikuta familia ya Hans, hakuna aliyemjali japokuwa alionekana amevimba macho kutokana na kumlilia Hans.

Alipojaribu kuingia wadini alikatazwa na kuamua kusimama pembeni peke yake, baada ya muda shoga yake Brenda alifika na kwenda aliposimama.

“Vipi shoga?”

“Yaani mama Hans kanifukuza kama mbwa!”

“Kwa nini?”

“Hata sijui wakati anafahamu mimi na mwanaye tulikuwa vipi.”

“Kwa hiyo hujui hali ya Hans?”

“Sijui chochote.”

Mara simu ya Mage iliita alipoangalia ilikuwa ikitoka kwa Colin, aliitazama na kukunja uso bila kuipokea. Brenda aliyekuwa akimtazama usoni, alimuuliza.

“Simu ya nani?”

“Achana nayo,” alijibu kwa mkato.

“Mmh!”

Baada ya muda simu iliita tena, Brenda alishtuka kuona jina la Colin bila kupokelewa.

“Shoga mbona hupokei?”

“Achana naye.”

“Ha! Wewe si ulikuwa kwa Colin na umeondokaje?”

“Sijamuaga nimemuchana bado amelala.”

“Unajua unachokifanya unaiweka ndoa yako njia panda.”

“Kwani asiponioa nitapungukiwa nini?” Mage alijibu huku akiibinua midomo.

“Mage, usipoteze muda wa Colin, kuamini unampenda kumbe upo naye kivuli tu.”

“Brenda mwenye uamuzi wa kumpenda ninao mimi.”

“Kwa hiyo Colin si chaguo lako?”

“Brenda huu si wakati wa kuzungumzia Colin zaidi ya kujua hali ya Hans ndiye aliyetuleta hapa.”

“Mmh! Sawa.”

***

Colin baada ya kushtuka usingizini alijua mpenzi wake yupo msalani au bafuni, lakini muda ulikatika bila kuonekana. Alikwenda msalani kumtafuta huku akimwita bila kupata jibu. Alitoka hadi nje na kumuuliza mlinzi.

“John umemuona shemeji yako?”

“Ametoka asubuhi sana, hakukuaga?”

“Ameniacha nimelala.”

“Tena alionekana kama analia nilijua mmegombana.”

“Hata sielewi kitu.”

Colin alimpigia simu mchumba wake, lakini iliita bila kupokelewa. Alirudia zaidi ya mara tatu, vilevile haikupokelewa. Alijiuliza Mage amepatwa na nini, wasiwasi wake labda kwao kumetokea tatizo.
Aliingia ndani na kuvaa pensi na fulana, chini alivaa ndala na kuingia kwenye gari kuelekea Kigamboni kwa kina Mage ili ajue amepatwa na nini.

Alikimbiza gari, kutokana na foleni aliamua gari lake kulipaki Posta ya zamani na kuchukua bodaboda ili awahi kufika. Baada ya kuvuka alichukua nyingine iliyo mpeleka nyumbani kwao Mage.
Alimlipa dereva na kuingia ndani ya geti, alipofika sebuleni alimkuta msichana wa kazi akifanya usafi.

“Habari Sofi?”

“Nzuri shemu, shikamoo.”

“Marahaba, vipi Mage yupo?”

“Sijamuona toka asubuhi.”

“Mama?”

“Yupo chumbani kwake.”

“Kaniitie.”

Colin alibakia sebuleni kumsubiri mama Mage, baada ya muda alitokea na kushangaa kumuona Colin katika hali ile.

“Vipi baba, kwema?”

“Kwema, sijui hapa.”

“Hapa hatujambo, mwenzio yupo wapi?” mama Mage alimuulizia mwanaye baada ya kumuona Colin peke yake.

Itaendelea..........

Mizambwa vipi tena mbona umetususa ati? Hadithi wapi?
 
Wakili wa Moyo-21

ILIPOISHIA:
Colin alibakia sebuleni kumsubiri mama Mage, baada ya muda alitokea na kushangaa kumuona Colin katika hali ile.
"Vipi baba, kwema?"
"Kwema, sijui hapa."
"Hapa hatujambo, mwenzio yupo wapi?" mama Mage alimuulizia mwanaye baada ya kumuona Colin peke yake.
SASA ENDELEA...

"Nimeshtuka kitandani sikumkuta, nimempigia simu haipokelewi, nikawa na wasiwasi na kuamua kuja huku."

"Hapa sijamuona, atakuwa amekwenda wapi? Mmh! Basi atakuwa kwa Brenda tu."

Colin alipiga simu kwa mara nyingine lakini haikupokelewa, alirudia mara mbili vilevile haikupokelewa baadaye ikazimwa kabisa.
"Mama simu haipokelewi niliporudia imezimwa kabisa."

"Mmh! Atakuwa wapi mtoto huyu la.."

Mama yake alinyamaza baada ya kumuona mwanaye akiingia, wote walipeleka macho kwake. Walishtuka kumuona macho yake yakiwa yamevimba kuonesha alikuwa akilia.
Aliwapita bila kuwasemesha na kuelekea chumbani kwake kitu kilichomshtua mama Mage na kumuuliza Colin.
"Colin umemfanya nini mwanangu?"

"Mama sijamfanya kitu, si umuulize mbele yangu."

Mama Mage alimfuata mwanaye chumbani na kumkuta amejilaza kwa kulalia tumbo.

"Mage."

"Abee."

"Kuna nini?"

"Hans ana hali mbaya asishangae kusikia amefariki."

"Amefanya nini?"

"Amevamiwa na majambazi, mke wake na mwanaye wameuawa."

"Mungu wangu! Ndipo unapotoka?"

"Ndiyo, mama."

"Mbona hukumuaga mwenzio?"

"Ningemuaga nakwenda wapi?"

"Na mbona umempita bila kumsalimia."

"Nitamweleza nini?"

"Kwa hiyo itakuwaje?"

"Mwambie aondoke siwezi kuzungumza naye chochote kwa sasa."

"Magee, unajua Colin ni nani yako?"

"Mchumba wangu na mume wangu mtarajiwa, lakini kwa leo naomba aniache nitamtafuta mwenyewe."

"Mage, unajua unanitafutia lawama, Colin atatuelewa kweli?"

"Mama fanya kila uwezalo ili Colin aondoke, nitamtafuta."

"Unanitia kwenye ubaya, Mage unaibomoa ndoa yako kwa mikono yako, unapoteza uaminifu kabla ya ndoa."

"Mama ndoa ni zawadi toka kwa Mungu, kama si riziki yangu siwezi kuilazimisha."

"Mmh! Sawa wacha nitajaribu," mama Mage alitoka chumbani na kumwacha mwanaye amejilaza huku akiwa na mtihani wa kumueleza Colin ili aondoke bila kuhoji kitu.

Colin alibakia sebuleni akiwaza kipi kimempata mchumba wake, alijiuliza alikwenda wapi asubuhi ile kama hakurudi nyumbani na kwa nini ameonekana analia kipi kimemsibu? Alibaki kusubiri kwa hamu kujua kipi kimemsibu mchumba wake, ambaye aliamini ndiye moyo wake yeye alibakia na mwili tu.

Mama Mage alirudi hadi sebuleni, Colin aliyekuwa ametazama juu akiwa mwingi wa mawazo kutokana na kilichotokea asubuhi ile, aliposikia sauti ya miguu ikisogea alipokuwa amekaa aliyahamisha macho yake na kumuona mama Mage, alijikuta akinyanyuka kama anampokea mheshimiwa.

"Vipi mama?"

"Mmh! Safi tu," Mama Mage alijibu huku akijitahidi kutengeneza uso wa mbuzi ili aweze kutengeneza mambo hasa kutokana kuwa mzazi.

"Vipi Mage alikuwa wapi na amepatwa na nini?" Colin aliuliza akiwa amemkazia macho.

"Mmh! Si..si..au fanya hivi, baba wewe nenda nyumbani, mpenzi wako kuna mambo yao ya kitoto si unajua baba mwenzio bado mdogo?"

"Ndiyo najua, lakini amepatwa na nini na alikwenda wapi bila kuniaga ikiwa na wewe hujui?"

"Mwanangu, wala hakuna jambo la kutisha, u..u..najua mwenzio, baba eeh, hebu kwanza hili tuliache jioni mwenyewe atakueleza kila kitu," mama Mage alijitahidi kubadili mazungumzo.

"Sawa mama, lakini Mage ni mchumba wangu natakiwa kujua kila kitu chake, sasa hivi ni mke wangu, tumebakishwa ndoa tu ambayo haipo mbali. Hivi nirudi nyumbani namweleza mama nilichokikuta hapa, kisha naulizwa kimetokana na nini nitajibu nini?" Colin alitetea hoja yake.

"Mwanangu ngoja nikutoe wasiwasi, mwenzio alikwenda kwa shoga yake sijui nini anamdai, basi wametibuana ndiyo maana yupo vile," mama alitengeneza uongo.

"Sasa mama kama ni hivyo kwa nini hataki kuzungumza na mimi?"

"Colin mwanangu, mi mkubwa naomba uondoke ili jioni uzungumze vizuri na mwenzako. Atakachokuambia hata wewe utacheka."

"Mmh! Sawa, basi mi naondoka."

Colin alisema huku akinyanyuka kuelekea nje, alipofika nje alikodi bodaboda hadi Kivukoni ambako alivuka upande wa pili na kukodi bodaboda nyingine hadi kwenye gari lake na kuingia ndani.

Kabla ya kuondoka alitulia, mikono aliweka juu ya usukani na macho aliangalia mbele, alikuwa kama anaona lakini alizama kwenye mawazo na kujiuliza Mage alikwenda wapi bila kuaga, na kwa nini amerudi akilia? Kipi kimempata alipokwenda na mwisho alijiuliza kwa nini amekataa kuzungumza naye?

Baada ya kukosa majibu ya maswali yake, aliondoa gari kuelekea nyumbani. Alitembea mwendo wa kawaida huku akili yake ikiwa haijakaa sawa. Alipofika katika makutano ya Barabara ya Kawawa na Morogoro, macho yake yalishtuka kumuona msichana mmoja akiuza ndizi.

Sura yake haikuwa ngeni machoni mwake lakini mavazi yalifanya macho yapingane na akili yake. Sura ilikuwa ya Cecy lakini mavazi yake yalikuwa machakavu na mwili ulimvaa vumbi kwa ajili ya kutembea barabarani kwa miguu kuuza ndizi. Kwa vile alikuwa kwenye foleni, alituliza macho yake kwa binti yule ambayo yalimwambia ni Cecy.

Wakati anataka kuondoa gari alisikia mtu akimwita.
"Cecy leta ndizi mbili."

Kwa vile taa ziliruhusu aliliondoa gari na kwenda kulipaki kituo cha mafuta cha Magomeni, alilizima na kutoka nje.

Kwa vile Cecy alikuwa amevuka barabara kwenda kuuza ndizi maeneo ya hospitali, alimtuma kijana mmoja aliyekuwa akiuza miwa.

"Samahani mkubwa, naomba kamwambie yule msichana alete ndizi kumi."

Yule kijana alimfuata Cecy aliyekuwa ametua beseni lake chini akiuza ndizi, alipofika alimwambia.
"Dada peleka ndizi kumi kwenye lile gari."

"Kumi hazitafika zitabaki sita."

"Mpelekee zote."

Itaendelea.................
 
kwa jinsi hali inavyoonekana Cecy anaweza kuja kuwa mama mwenye nyumba mtarajiwa na maisha ya mtaani itakuwa basi tena. Mage asipojiangalia hapo baadae atakuja tafuta mchawi kumbe amejiloga mwenyewe.

Nasubiri uhondo zaidi
 
Wanawake hata watendwe vipi akishapenda huwezi kumbadirisha.
 
Back
Top Bottom