Habari za afya ya Dr. Harrison Mwakyembe

Habari za afya ya Dr. Harrison Mwakyembe

Jasusi,

Sawa tuachane na Lowassa, lakini vipi wale vijana wa kule Kyela waliofukuzwa kwenye chama bila kufuata sheria, je kwao hizo principles of natural justice hazifanyi kazi?

Vipi hao vijana wengine wa Kyela ambao yeye anapita mitaani kuwaambia watu kwamba wamehongwa milioni 400, bila hata kuwauliza, kutoa hata chembe ya ushahidi, huku anajua hawapo na hawawezi kujitetea; je wao hawahitaji hizo principles of natural justice?

Mtu akiwa na double standards na unafiki, JF tutaendelea kumuumbua tu. Mimi nilitegemea msomi aliyebobea kwenye sheria angelikuwa wa kwanza kuongoza kwa kufuata sheria.

Vijana wepi tena kyela wametimuliwa? hii nyuzi daa si mchezo
 
Vijana wepi tena kyela wametimuliwa? hii nyuzi daa si mchezo

MkamaP,

Imo mbona humu humu JF? Ila hao vijana wote wamerudishiwa vyeo vyao na badala yake mwenyekiti ndiye kapewa warning baada ya kugundulika kutofuata sheria katika kuwahukumu hao vijana.

Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu huwa mchungu hasa.
 
Mkuu hizo nyuzi sijaiona, na ningependa tu kupata tu hints kidogo ni nani aliyechochea hadi hao jamaa kutimuliwa? kwa maelezo niliyojaribu kuanganisha vipande inaonekana ni Mwakyembe kama nimekosea nisahihishe.

Harafu huyu Mwakyembe kwa kweli mimi haziivi kabisa naye hasa alivyo nazarau kwa sisi ambao umande ulikuwa kikwazo kwetu. Maana ukijaribu kuitafsiri senteso yake unapata picha ya kwamba mtu yeyote ambaye elimu yake ipo chini ya Mwakyembe hatakiwi ku argue naye.

Sasa swali nalojiuliza na bila kupata jibu yeye Mwakyembe mfano akiwa wakili na jamaa mwingine aliyemfundisha pale udsm mwenye digrii moja naye wakili wapo ktk kesi kwa pande tofauti nahisi Mwakyembe anaweza argue kwa kusema huyu wakili hana uelewa kama wangu.

Na kingine nachohisi kutokea huko kyela 2010 huyu jamaa ataweza kuwaambia wananchi mimi ninaelimu kubwa kuliko yule ,hivyo yote anayosema yule hana uelewa nayo kama mimi.
teh teh teh teh teh teh teh
 
Mkuu kwa upande fulani unachosema ni kweli. Hata waingereza wanasema kama huna facts huna haki ya kuongea. Kuna ukweli fulani ndani yake. Ndio maana hata wabunge wetu ambao walikimbia umande bungeni wanakaa kimya tu. La mmuhimu ni kuwa na facts zaidi ili tuweze kuwa na haki ya kuongea.
 
Shalom,

Unanichekesha maana mara unapinga baadaye unageuka. Kama unaenda kuwekeza Kyela karibu sana na utakuwa umefanya jambo muhimu sana. Wengine tulianza zamani na tumekumbana na kila aina ya matatizo. Kama utakwama jambo nitakuwa tayari kukupa tips namna ya ku survive kwenye jungles za Kyela. Sitakuonea wivu mkuu! kwi kwi kwi!!!

Hakuna anayetoa vizawadi kuwapa watu, ndio majungu ya Kyela hayo. Kama wengine tumewahi kutoa misaada basi ni kwenye mashule na afya na wala sio kwa mtu mmoja mmoja, of course ukiachia ndugu. Pia mimi ni mjamaa, sikubaliani na mawazo yako hayo ya kwamba asiyefanya kazi na asile. Kuna watu wanatakiwa kusaidiwa kwasababu mbalimbali. Pia kuna misaada mingine inaweza kumsukuma mhusika ili aweze kujitegemea. Kwa mfano ukiweza kumsaidia kijana akimbie Dar kujaza forms na kushughulikia loan ili aende mlimani, huo ni msaada endelevu, vinginevyo angeweza kukosa nafasi shauri ya vijisenti kidogo tu.

Huyo kijana nimeandika bora asiige ya wazazi. Kila mtu na msalaba wake, huwezi kumtwisha mtoto msalaba wa babake. Nilitaka tu kukuonyesha kwamba ninaelewa unamsema nani.

Mimi mtoto wa wakulima, babangu asingeweza kumwibia mtu yeyote. kama baba yangu alifanya makosa, basi JF ni kumkoma nyani giladi, wewe weka tu. Ila kwa jinsi nilivyoona unaandika hapa, najua hujui kitu na mambo ya Kyela; you are not well informed. Ukijisahau sana Dar au USA kweli huwezi kuyaelewa ya huko kwenu vijijini.

Mimi sikupingi hata kidogo uenda tuko pamoja kwenye mambo mengi tu. tatizo langu mimi ni kwa nini kwa kila jambo unampinga DK sababu ya kusema kuwa eti anawagawa wana kyela hiyo ni ya kitooto kabisa. Siasa ni mchezo kura zinagawa watu hata iwe 80-20. Ningejua unampinga ingekuwa powa. Nilikuuliza unataka kugombea ubunge kyela ukang'aka haya tupe sababu za kuwa kinyume na DK kwa kila kitu husemi sasa tukubebeje. Mimi siitaji tips yoyote ninaporudi nyumbani siendi kujenga gorofa kule!

kama umetoa misada kwenye afya na shule hongera kwani huo nimtizamo wako. Sasa unataka kusema kuwa matatizo ya afya na shule yameisha kwa sasa? kama yako vile vile haukuwa msaada bali pozeo hilo. na mimi sio mzee wa mapozeo (tempo.. Solutions) mimi naamini katika kutatua tatizo na siyo kupoza maumivu. hapo atuko pamoja. Je huko UK umeshaaona watu wakigawa hiyo misaada kama yako? na matajiri wako kibao wenye mihera sasa hujajiuliza wanamatatizo gani kama wewe uko njia sahihi?

Kunionesha kuwa unamjua ilikuwa lazima utaje mazambi ya baba yake? hakuna lingine positive la kuweza kunionesha kuwa unamjua kama vile labda ni brain, HB na n.k. Ndugu yangu kwako wewe kuiba peke yake ndiyo problem, ukiwa mzinzi, dhuluma, uchawi na mengineyo siyo shida na hayo yanafanywa sana na maskini. Mimi niliweka hili kwa kukutega tu nilitaka kujua kama kweli unahoja na chuki yako na DK au wivu tu. kwa jinsi ulivyoonekana kumbe hata rafiki zake unawachukia kwangu ni kipimo tosha kuwa una lako jambo. marafiki zako wangapi ni wezi mbona huwataji humu?

Wewe kama ni mjamaa kivyako vyako mimi kwangu ujamaa ni evil! Lucifa's philosphy period! na kwenye hili sibishani hata kidogo kwani siitaji mjadara kwenye kanuni za Mungu hata kidogo.

halsafu mimi sio CCM hata DK kura yangu hapati na wewe pia kama utagombea maana naona wameshakuvunja nguvu hupati pia. Mimi ni kati ya wale asilimia ndogo tunaona kuwa tupo hapa kwa sababu ya CCM.

Private massage sijibu!
 
Kabla ya kulaumu wengine tuambie wewe umefanya nini? Kama mtu amejenga ghorofa si huyo afadhali angalau vijana wamepata ajira kuliko bingwa wa kuongea kwenye mtandao au wanaoiba Tanzania na kuhamishia huku nje?

Mimi nimekupa sababu za kutofautiana na Mwakyembe, badala ya kutoa sababu zako unaanza maneno ya kejeli. Toa hoja zako kwanini unaona Mwakyembe anafaa na sio kunishambulia mimi. Lakini kwasababu umeamua kunifanya mimi ni hoja wacha nikuvae na kukupa ukweli wako.

Si afadhali wanaosaidia shule na hospitali kuliko nyie mnaopeleka wazungu fake kwenda kudanganya wananchi eti mtasaidia huku ni utapeli tu? Vipi wale uliowapeleka safari iliyopita wamefanya nini? Ni kweli huhitaji tips zangu maana mwekezaji tapeli toka lini akataka kujua taratibu? Mnawakusanya vijana wa vikoba na kuanza kuwadanganya, aibu kweli kweli!

Kwanza hata hizo solutions za kudumu unazozisema uwezo wa kuzifanya unazo? Toka lini anayetegemea mke kuishi akawa na uwezo wa kusaidia wengine? Mkuu achana na ujinga wa kuzunguka huku na huku kutapeli watu, fanya kazi. Unasema ujamaa unauchukia, huku ishi yako inategemea fadhila za wengine? Usituzuge hapa mkuu, tunakufahamu ipasavyo.

Kama mimi nimekwisha kweli ungehangaika humu kwenye net kufuatilia hoja zangu? Una wasiwasi gani mpaka utumiwe hivyo? Unakubali utumiwe ili tu jina lako litokee kwenye reports, utambulishwe kwa spika. Kama unataka kufika bungeni si gombea kwa nguvu zako?

Mimi si nilikuruhusu umtaje huyo mzazi wangu? Najua hauko informed; hunijui. Taja lolote unalolijua kuhusu wazazi wangu. Hata hao marafiki zangu wataje, nimekupa ruhusa maana sina cha kuficha.

Vipi zile shares za kwenye upepo umewauzia Wakorea? Hiyo ndio miradi endelevu? Mnachukua ardhi ya watu maskini halafu mnawauzia wageni? je mbona matatizo ya umeme bado yapo pale pale? Si mungejiita tu kwamba nyie ni watu wa property or land management?

Kama una matatizo na mimi kugombea ubunge basi nenda kabadili katiba ya TZ na iwafanye wabunge waliopo wawe wa kudumu. Je wote wanaopinga hoja za Mwakyembe hapa wanataka kugombea ubunge Kyela? Ubunge haugombewi JF, kama ubunge ungekuwa unashindaniwa JF basi CHADEMA wangeshinda Busanda.

Kama hujui huku wenye pesa wanatoa sehemu ya pesa zao kusaidia wenye shida. Hata huko uliko akina Bill Gates wanatoa pesa kibao kusaidia miradi mbalimbali ya kusaidia maskini. Mmeshindwa hoja mnaanza kuingiza majungu ya kwamba wanagawa pesa. Pesa ulizozipata kwa kuchapa kazi utagawa kwa watu kwenye vijiwe? Labda mnaopata pesa za utapeli au za kwenye siasa ndio mna uwezo huo.

Hata ukibeza hatuwezi kuacha maana tunaona vijana wanaofaidika. Wewe utawajua wapi hao vijana wakati unachoweza ni kutumia influences za wanasiasa ili kuidanganya serikali ikupe nafasi ya kuwekeza?

Ila mkuu tunajua utapeli wako, tafuta kazi ujitegemee na sio kutegemea mke kama mgonjwa. Utawekeza TZ huku huna mpango wowote; acha kudanganya watu kwa utapeli.

Unafikiri Tanzania inahitaji Wazungu kuendelea? Tumia akili yako kwenda kuwekeza nyumbani kwani huo utapeli hautakufikisha popote.

Kama projects zangu zinakupa kiwewe, basi subiri na zingine zinakuja tena kwa kasi mpya. Mtachukia mpaka mpasuke mwaka huu, hata mukwamishe vipi tutaendelea kufanikiwa tu maana hatumwibii mtu.
 
Shalom na Mtanzania,
Wakuu vipi tena?.. heee mara imekuwa tena personal between U guys ambao nawategemea ktk issue hii. najua fika nyie mnafahamu vizuri kinachoendelea Kyela na siasa zake, bahati mbaya ile mada ya Kyela mmeiacha na kuingia huku..
Nitapenda sana kuona majadiliano yenye kujenga baina yenu hasa kuhusiana na chaguzi za Kyela. Iwe mmoja wenu ni mfuasi au mwakilishi wa Dr. Mwakyembe na mwingine wa huyo kijana wa UK..
Mijadala kama hii inajenga na inaweza kuwa moto hapa JF lakini msijaribu kuiweka personal kati yetu kwani nyie nyote ni wajumbe (watumwa) tu..Na kama ni wanasiasa (Wabunge watarajiwa) itakuwa vizuri zaidi kuanza kuuza kura zenu hapa, mtaipandisha JF ktk daraja jingine ambako Wabunge wanaweza kupambana kwa hoja openly and free!
 
Mtanzania + Shalom..........lets take another course puuuliiiiizz.....that does not build Kyela or either of you
 
Ogah, Mkandara,

Wakuu nimewasikia na sitachangia tena hoja za Shalom ili kukwepa kuwaingiza wana JF wengine kuingia kwenye mambo yasiyowahusu.

Samahani kwa posts zangu mbalimbali ambazo hata mimi mwenyewe naona hazijengi ila kuna wakati inabidi iwe jino kwa jino. Tumeumana vya kutosha na wacha niendelee na mambo mengine ya maana.
 
Duu, Mtz.

Hii ndiyo Siasa au kukoma nyani? Lazima niseme kidogo, narudia tena, kidogo umevuka kampaka. Hapa umetembeza u-Inzaghi kwa kuotea kwa milimita kadhaa.

Yes, nyani akomwe ila tukumbuke mstari wa kuotea uko wapi.

Ngengengeee, Let's get ready to Rumble............ 2010 hiyoooo!!!!
 
shalom,

kabla ya kulaumu wengine tuambie wewe umefanya nini? Kama mtu amejenga ghorofa si huyo afadhali angalau vijana wamepata ajira kuliko bingwa wa kuongea kwenye mtandao au wanaoiba tanzania na kuhamishia huku nje?

Mimi nimekupa sababu za kutofautiana na mwakyembe, badala ya kutoa sababu zako unaanza maneno ya kejeli. Toa hoja zako kwanini unaona mwakyembe anafaa na sio kunishambulia mimi. Lakini kwasababu umeamua kunifanya mimi ni hoja wacha nikuvae na kukupa ukweli wako.

Si afadhali wanaosaidia shule na hospitali kuliko nyie mnaopeleka wazungu fake kwenda kudanganya wananchi eti mtasaidia huku ni utapeli tu? Vipi wale uliowapeleka safari iliyopita wamefanya nini? Ni kweli huhitaji tips zangu maana mwekezaji tapeli toka lini akataka kujua taratibu? Mnawakusanya vijana wa vikoba na kuanza kuwadanganya, aibu kweli kweli!

Kwanza hata hizo solutions za kudumu unazozisema uwezo wa kuzifanya unazo? Toka lini anayetegemea mke kuishi akawa na uwezo wa kusaidia wengine? Mkuu achana na ujinga wa kuzunguka huku na huku kutapeli watu, fanya kazi. Unasema ujamaa unauchukia, huku ishi yako inategemea fadhila za wengine? Usituzuge hapa mkuu, tunakufahamu ipasavyo.

Kama mimi nimekwisha kweli ungehangaika humu kwenye net kufuatilia hoja zangu? Una wasiwasi gani mpaka utumiwe hivyo? Unakubali utumiwe ili tu jina lako litokee kwenye reports, utambulishwe kwa spika. Kama unataka kufika bungeni si gombea kwa nguvu zako?

Mimi si nilikuruhusu umtaje huyo mzazi wangu? Najua hauko informed; hunijui. Taja lolote unalolijua kuhusu wazazi wangu. Hata hao marafiki zangu wataje, nimekupa ruhusa maana sina cha kuficha.

Vipi zile shares za kwenye upepo umewauzia wakorea? Hiyo ndio miradi endelevu? Mnachukua ardhi ya watu maskini halafu mnawauzia wageni? Je mbona matatizo ya umeme bado yapo pale pale? Si mungejiita tu kwamba nyie ni watu wa property or land management?

Kama una matatizo na mimi kugombea ubunge basi nenda kabadili katiba ya tz na iwafanye wabunge waliopo wawe wa kudumu. Je wote wanaopinga hoja za mwakyembe hapa wanataka kugombea ubunge kyela? Ubunge haugombewi jf, kama ubunge ungekuwa unashindaniwa jf basi chadema wangeshinda busanda.

Kama hujui huku wenye pesa wanatoa sehemu ya pesa zao kusaidia wenye shida. Hata huko uliko akina bill gates wanatoa pesa kibao kusaidia miradi mbalimbali ya kusaidia maskini. Mmeshindwa hoja mnaanza kuingiza majungu ya kwamba wanagawa pesa. Pesa ulizozipata kwa kuchapa kazi utagawa kwa watu kwenye vijiwe? Labda mnaopata pesa za utapeli au za kwenye siasa ndio mna uwezo huo.

Hata ukibeza hatuwezi kuacha maana tunaona vijana wanaofaidika. Wewe utawajua wapi hao vijana wakati unachoweza ni kutumia influences za wanasiasa ili kuidanganya serikali ikupe nafasi ya kuwekeza?

Ila mkuu tunajua utapeli wako, tafuta kazi ujitegemee na sio kutegemea mke kama mgonjwa. Utawekeza tz huku huna mpango wowote; acha kudanganya watu kwa utapeli.

Unafikiri tanzania inahitaji wazungu kuendelea? Tumia akili yako kwenda kuwekeza nyumbani kwani huo utapeli hautakufikisha popote.

Kama projects zangu zinakupa kiwewe, basi subiri na zingine zinakuja tena kwa kasi mpya. Mtachukia mpaka mpasuke mwaka huu, hata mukwamishe vipi tutaendelea kufanikiwa tu maana hatumwibii mtu.

linga linga linga!
 
Shalom na Mtanzania,
Wakuu vipi tena?.. heee mara imekuwa tena personal between U guys ambao nawategemea ktk issue hii. najua fika nyie mnafahamu vizuri kinachoendelea Kyela na siasa zake, bahati mbaya ile mada ya Kyela mmeiacha na kuingia huku..
Nitapenda sana kuona majadiliano yenye kujenga baina yenu hasa kuhusiana na chaguzi za Kyela. Iwe mmoja wenu ni mfuasi au mwakilishi wa Dr. Mwakyembe na mwingine wa huyo kijana wa UK..
Mijadala kama hii inajenga na inaweza kuwa moto hapa JF lakini msijaribu kuiweka personal kati yetu kwani nyie nyote ni wajumbe (watumwa) tu..Na kama ni wanasiasa (Wabunge watarajiwa) itakuwa vizuri zaidi kuanza kuuza kura zenu hapa, mtaipandisha JF ktk daraja jingine ambako Wabunge wanaweza kupambana kwa hoja openly and free!

Mkandara,

Asante kwa ushauri wako mzuri, ila si kwamba nimefanya haya kwa bahati mbaya ila ulikuwa ni makusudi kabisa hasa baada ya kuona jamaa akimsulubu Mwakyembe bila ya sababu yoyote eti amewagawa watu wa kyela kitu ambacho sio kweli

DK alikuwa ana nafsi kubwa sana ya kulikomboa jimbo la Kyela kutoka kwenye umaskini lakini kutokana baazi ya watu kutojua wakati wa siasa na wakati wa kazi wamemfanya ashindwe kabisa kufanya mambo ya maendeleo na kumfanya awe defensive kila wakati.

Hawa jamaa hawakumpa hata wiki moja siku moja baada ya kushinda ubunge wakamzushia eti amepingwa wakizani anaweza pewa uwaziri na baada ya hapo wamendelea kumfuatilia na kumfanya muda wake wote awe anafuatilia mambo ya siasa kuliko kuikomboa kyela

halafu walichokianzisha kinafanikiwa wanakuja na kuanza kumpiga mawe sasa kama kweli mlitaka alate umoja na maendeleo si mngempa muda wa kutosha ili mje mmpime na sio kumfanya awe kwenye kampeni miaka yote mitano? si ata Bush amesema hapendi kumpinga obama lakini haimanishikuwa ameacha kuwa pro life la hasha ila nikuheshimu maamuzi ya watu na kusubiri kuona mtu anafanya nini.

Walahi mgempa muda wa kufanya kazi leo mama zetu wasingekuwa wanajifungulia kwenye baiskeli ipinda lakini haya ndiyo mnayotaka ili mpate muda wa kugawa zawadi na kujionesha.

mimi sitaaacha kujibu hoja za chuki kwa Mwakyembe kwa kisingizio cha kuwa tuwaache watu wakiturudisha nyuma kwa political ambition zao.

nakushukuru tena kwa ushauri hasa kama utampa mwakyembe muda wa kufanya kazi yake mpaka wakati wa kampeni hapo mwakani. Tunaitaji maendeleo Kyela hatutaki zawadi.

Pamoja na kumchanganya mwakyembe bado emefanya 10 time aliyoyafanya aliyemlisi wa kubisha na abishe.
 
Shalom,
Pamoja na kumchanganya mwakyembe bado emefanya 10 time aliyoyafanya aliyemlisi wa kubisha na abishe.
Shukran, heshima mbele..
Maadam umeanzisha hii hoja, mkuu unaweza kutuambia kafanya nini 10x ya aliyemrithi?..
 
Shalom,

Shukran, heshima mbele..
Maadam umeanzisha hii hoja, mkuu unaweza kutuambia kafanya nini 10x ya aliyemrithi?..

Mkuu,

10x lugha ya picha maana yake amefanya mambo kuliko huyu aliymtangulia sasa sijui kama ulielewa kuwa kuna vitu kumi?

Ngoja nikupe ingalau machache
jamaa aliacha shule mbili na sasa ziko more than 14.

Mkutano wake wa kwanza ulikuwa kuhusu vijana wa darasa la saba ambao 93% walikuwa wamefaulu lakini only less than ten walikuwa wanaenda secondary, ask what %ntage wanaenda sasa?

Sasa tuaongelea Kyela alipokuwa jamaa basi ni kuupiga tu uzingizi bungeni usinekuwa mchele wetu unaonukia ukipikwa mpaka mita hamsini tulipotea kabisa katika ramani ya nchi yetu

jamaa walikuwa wanauza mchele wote kwa wapemba na njaa ilikuwa ni ishu ya kawaida kabisa huko sio leo sasa watu wanajua kuweka akiba ya chakula. Kumbuka kuwa nyuma mazao yalikuwa mengi kuliko sasa lakini njaa imekuwa history.

Amehamasisha vijana kupenda kazi. kyela ilikuwa ni moja ya wilaya ambazo vijana wake wanapenda kutofanya kazi sasa hali hiyo inatoweka.
 
Shalom,
Mkuu nilipokuwa Bongo niliambiwa ule mchele wa Kyela haupo tena.. na wala sikuuona Dar isipokuwa wa kichina.. vipi?
 
Shalom,
Mkuu nilipokuwa Bongo niliambiwa ule mchele wa Kyela haupo tena.. na wala sikuuona Dar isipokuwa wa kichina.. vipi?

Upo mzee ila ni adimu kidogo, mama katoka kuvuna na kanitumia imebidi nikaombe radhi majirani si unajua tena uswazi!
 
10x lugha ya picha maana yake amefanya mambo kuliko huyu aliymtangulia sasa sijui kama ulielewa kuwa kuna vitu kumi?

Ngoja nikupe ingalau machache
jamaa aliacha shule mbili na sasa ziko more than 14.

Mkutano wake wa kwanza ulikuwa kuhusu vijana wa darasa la saba ambao 93% walikuwa wamefaulu lakini only less than ten walikuwa wanaenda secondary, ask what %ntage wanaenda sasa?

Sasa tuaongelea Kyela alipokuwa jamaa basi ni kuupiga tu uzingizi bungeni usinekuwa mchele wetu unaonukia ukipikwa mpaka mita hamsini tulipotea kabisa katika ramani ya nchi yetu

jamaa walikuwa wanauza mchele wote kwa wapemba na njaa ilikuwa ni ishu ya kawaida kabisa huko sio leo sasa watu wanajua kuweka akiba ya chakula. Kumbuka kuwa nyuma mazao yalikuwa mengi kuliko sasa lakini njaa imekuwa history.

Amehamasisha vijana kupenda kazi. kyela ilikuwa ni moja ya wilaya ambazo vijana wake wanapenda kutofanya kazi sasa hali hiyo inatoweka.

Mkuu Shalom,

Hapo unaongea na tunaweza kujibizana na kuelemishana.

kwa taarifa yako tu, Kyela ina shule za sekondari 23 na kati ya hizo 21 ni za serikali. Shule hizo ni KCM, Itope, Ipande, Ikolo, Ipinda, Kyela, Matema Beach, Bujonde, Ngonga, Katumba Songwe, Kajunjumele, Ikama, Lusungo, Kafundo, Makwale, Nkuyu, Ikimba, Itunge, Mwaya, Masukila na Shule ya Wasichana ya Kayuki wilayani Rungwe. Mwigo na Ngana zinamilikiwa na taasisi zisizo za kiserikali ingawaje kuna mpango wa kuzifanya za serikali.

Wakati Mwakyembe anaingia madarakani kulikuwa na shule za sekondari zifuatazo: ni Itope, Kyela, Ipinda, Ipande, Ikolo, Matema Beach, Ikolo, Ngana, Katumba, Mwaya, kayuki na Mwigo, sio mbili kama ulivyosema, maana ya mbili inaelekea mwenzetu unaongelea mambo ya mwaka 80 ndio kulikuwa na shule mbili ambazo ni Itope na Ipinda. Unaweza kuhakikisha hizi data kwa kuangalia matokeo kupitia necta. Shule ambazo zilianza wakati Mwakyembe ni mbunge ndio kwanza wako form four mwaka huu, hivyo hazitakuwa kwenye list ya waliofanya mtihani mwaka jana.

Mbali ya hiyo ni kwamba baada ya serikali ya JK kuingia madarakani kupitia PM Lowassa alitoa amri kwa wanafunzi wote waliofaulu kuhakikisha wanaenda secondari na kila kata iwe na shule. Hilo lilikuwa agizo la serikali wala sio mbunge aliyeamua kuwe na shule kila kata. Mbunge, wananchi, mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa walishirikiana wote kwenye kusimamia shule. Sio kwa Kyela tu au Mbeya tu bali kwa Tanzania nzima.

Hata hizo shule ambazo zilianza mwaka 2006, nyingi zilianza kujengwa 2005 ila wanafunzi wakaweza kuanza shule 2006. Ukiweka kwa pamoja utakuta wakati Mwakyembe anaingia, Kyela kulikuwa na shule zaidi ya 15. Hakukuwa na na shule ya kidato cha tano na mpaka leo hakuna kidato cha tano Kyela pamoja na kwamba ilikuwa ahadi ya Mwakyembe 2005. Jitihada ya kuanzisha shule mbili mwaka huu zimekwamisha shauri ya siasa hizo hizo.

Na kwa taarifa yako kikao cha halmashauri ya CCM Kyela cha wiki mbili zilizopita kilimtuhumu mbunge kutangaza ujenzi wa shule kwenye television huku hata hajui hizo shule zimejengwa na nani, na kutumia pesa zipi. Kama unasema amejenga hizo shule basi kuna viongozi wa kata wa Kyela wanaona tofauti; wanaona wao kwa kushirikiana na DC aliyeondoka ndio walisimamia na kuchangisha pesa za ujenzi wa hizo shule. Pia walimtuhumu kuhusu michango anayochangisha Dar kwamba haifiki Kyela. Of course kwenye mafanikio kama ambavyo pia kwenye lawama huwezi kumwondoa mbunge. Binafsi naamini mbunge na wana Kyela wengine waliohusika wamesaidia kuongeza uwingi wa shule na kuwafanya watoto zaidi wasome.

Hilo la kuhamaisha vijana kupenda kazi sahau, halipo. Vijana gani hao waliohamasishwa? wako wapi, wanafanya nini? Hilo bado ni tatizo kubwa na nimeliandika mara nyingi kwenye posts zangu hapa.

Kuhusu mpunga looh! mkuu kweli uko out of touch, nenda Kyela mwezi wa tisa au kumi, watu mpaka vijijini wananua unga, mpunga umeisha, wote umeuzwa kwa wapemba kwasababu badala ya mpunga kuwa zao la chakula sasa ndio limekuwa source of income kwasababu Cocoa nyingi ni zile zilizopandwa miaka ya 60. Imekuwa miti na sio kokoa tena. Uzalishaji wa mpunga umeshuka mno wakati sisi tunakua familia yangu ilikuwa na uwezo hata wa kupata gunia 80 kwa mwaka, sasa wanavuna kama gunia tano na wanajiona wao ndio wajanja. Kuna factors nyingi zimechangia, hatuwezi kumlaumu mbunge kwa hili ingawaje angeweza kuwatumia vizuri mabwanashamba ambao sasa wanashinda tu ofisini huenda ingelikuwa nafuu kidogo.

Kwenye huu ujumbe mkuu Shalom ndio umeonyesha kweli uko out of touch na Kyela, nafikiri vijana wakikusoma wanacheka tu. Uliyoongea yote hayapo, kazi kweli kweli!
 
Mkuu Shalom,

Hapo unaongea na tunaweza kujibizana na kuelemishana.

kwa taarifa yako tu, Kyela ina shule za sekondari 23 na kati ya hizo 21 ni za serikali. Shule hizo ni KCM, Itope, Ipande, Ikolo, Ipinda, Kyela, Matema Beach, Bujonde, Ngonga, Katumba Songwe, Kajunjumele, Ikama, Lusungo, Kafundo, Makwale, Nkuyu, Ikimba, Itunge, Mwaya, Masukila na Shule ya Wasichana ya Kayuki wilayani Rungwe. Mwigo na Ngana zinamilikiwa na taasisi zisizo za kiserikali ingawaje kuna mpango wa kuzifanya za serikali..........!

Mtanzania vipi hapo juu....shule iliyoko Wilaya ya Rungwe kuhesabiwa kama ni ya Wilaya ya Kyela.....enlighten us plse
 
Back
Top Bottom