Habari za afya ya Dr. Harrison Mwakyembe

Habari za afya ya Dr. Harrison Mwakyembe

Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Kyela (Mwakasumi) amepewa onyo kwa kuwa chanzo cha mgogoro uliosababisha baadhi ya viongozi wa wilaya kupigwa.

Kamati ya CCM mkoa iliyokaa siku ya Jumamosi imeridhika na maamuzi ya halmashauri ya wilaya ya Kyela. Imewarudisha kwenye chama vijana waliopiga viongozi wao na kuwapa onyo kwamba wasirudie kitendo hicho.

Pia limetoa onyo kwa Mwenyekiti na kuagiza akifanya kosa lingine katika miezi 18 ataadhibiwa.

Inaelekea mwenyekiti kajifunga mwenyewe goli la kisigino baada ya kupanga kumdhibiti mtu fulani lakini imeishia kudhibitiwa yeye mwenyewe.

Ndio hizo habari za Kyela na Mbeya.
 
Mkandala,

Naona umeadika Samwel ila umechukua maneno yake na yangu.

Ni mie nilisema kuwa nazifahamu kesi mbili/tatu tayari ambazo nina imani Mafisadi mwakani WANAWEZA kuzitumia kummaliza Mwakyembe. Nimeandika kabisa hizo kesi zote mbili na sikuzificha. Kesi ya kwanza aliiandika kwa kurashia FMes hapahapa JF na kama sikosei iko kwenye hii thread. Ukitaka zaidi waweza kumuuliza. Kesi ya pili inafanana sana na hiyo, sema ya kwanza ilifanyika Dar na ya pili imekuja kujianika bila kukusudia kwenye mazishi ya mama yake.
Kesi ya tatu hiyo hata wewe unaifahamu na siyo siri ingawa mie niseme nilikuja kuipata humuhumu ndani na hiyo ni wakati wa Uchaguzi Zenji (Utawala wa Mkapa). Sijawahi ifahamu vizuri ila ina uhusiano na kipigo kilichotembea Zenji.

Sasa si unaona zote tunaziweka hapa ili kumpa muda ajiandae? Kama tungelikuwa hatumpendi unavyofikiri, tungelikaa kimya. Nimesema tangu mwanzo kuwa Mwakyembe ana uwezo mkubwa ila anajiharibia mwenyewe.

Mkandala, tatizo la Mwakyembe anataka kujifanya Rostam wa Kyela. Yaani lazima uwe na yeye tu na akisikia ulienda kwenye party kwa Mwakipesile (Boiler la kutupwa) basi siku hiyohiyo unakuwa mbaya wake. Analazimisha uwe na marafiki anaotaka na uhusiano na watu wale tu unataka. Ukifanya kivyako basi kwishieni. Ni sawa aje hapa akute mmekubaliana na Zitto juu ya jambo fulani basi hapohapo urafiki kwisha. Anakuwa kama Mwanaume mwenye wivu. Kila akiona mke wake kasimama na mwanaume basi ugomvi. Namhurumia huyo mwenyekiti wa CCM aliyemfanya mali yake na jamaa hajui hata afanye nini maana anaendeshwa na Mbunge na huku sheria/katiba ya CCM inamdai afanye vile. Nafikiri binadamu ili uishi na wengine lazima ujifunze kuwaamini. Vinginevyo, nenda kashike chaki.

Juu ya MAFISADI kama watataka kummaliza, nina imani wanazo kali zaidi ya hizi tunazozifahamu sisi hapa. Si uliona kwenye swala la umeme, walimtekenya kidogo na akaanza kuhaha kila sehemu?

Juu ya kupaka watu, juzi kampaka kijana mmoja aliyeko UK kuwa analeta mambo jambo. Na kibaya zaidi, imetoka kwenye geazeti la MAJIRA ukurasa wa mbele wakat jamaa yuko busy na Mabox yake UK, huku analimwa eti anataka kugombea. Haya magazeti nayo sijui yakoje, habari ya MBEBA mabox mnaiweka ukurasa wa mbele, kisa makala ya Mwakyembe? Na kwa ufupi ni kuwa alishaanza muandama jamaa siku nyingi sana. Na amekuwa akija hapa kwa kutumia jina la LAZARUS MTINDI (Soma nyuma jumbe zake - Ninaamini kwa asilimia 90 kuwa ni yeye). Ila jamaa wa UK naona mwisho atafikia sasa achoke na aamuwe kwenda kugombea. Akishaamua kufanya hivyo basi usiwe na wasiwasi, NITAKUJULISHENI <> kama ninataka kwenda kugombea (heeee Sikonge...🙂

Hizo sababu mbili kwa kweli zimekaa vibaya sana. Itabidi kumtafuta Dr. mzuri sana wa Plactic Sugery ili kuondoa hayo makovu aliyojiwekea. Mwakyembe alimtoa Mwakipesile kwa kumtolea uvivu na madudu kibao na moja wapo likiwa hilo la kugawa watu. Yeye anafanya hayohayo.
Anyway, madudu mengine sintayaweka kwa hisani ya ndugu zangu wa Kyela. Ila siku ikifika basi nitayaanika. Ila lazima ujuwe kuwa kama kuna sehemu mwakani uchaguzi utakuwa katika hadhi ya KIMATAIFA, basi Kyela utakuwa namba 1. Hapa hatuongelei pesa ila mbinu za kivita. Watu watakaa chini na kuchora Algorithm ya kushinda.

Mkuu, huyo unayemweleza, si Mwakyembe ninayemfahamu kwa karibu na kwa siku nyingi. Ni Mwakyembe uliyemuunda wewe kujifurahisha na wana JF ambao ni extremely ill-informed. Cheers!
 
Mkuu, huyo unayemweleza, si Mwakyembe ninayemfahamu kwa karibu na kwa siku nyingi. Ni Mwakyembe uliyemuunda wewe kujifurahisha na wana JF ambao ni extremely ill-informed. Cheers!

Nimeandika mengi sana pale juu. Sasa wewe unachosema SI KWELI ni kipi? Kuwa yeye Si Dr? Kuwa yeye alimshinda Mwakipesile? Kuwa anamuendesha Mwenyekiti wa CCM ambaye hapo juu pia tunasoma kakaripiwa? Ni nini hasa unataka hapa kusema?

Kama la kuwa yeye ni Mtindi, nilisema naweza kuamini kwa asilimia 90, ila kumbuka asilimia 10 ni kubwa sana.

Mwisho, kama wana JF tupo extremely ill-informed huoni kuwa na wewe kama mwanachama wa JF pia umo ndani? Au ndiyo yale mambo ya NYANI haoni...
 
wana Jf baada ya kutokea ajali ya Mh mwakiembe nimejaribu kufatilia baadhi ya matukio yalo muhusu mh huyu.

A; richmond case.
nimeangalia na kufatilia kesi inayoendelea kuhusu richmond kutokana na riporti ya mwakiembe bungeni walituamiisha kuwa RICHMOND NI KAMPUNI FAKE na serekali imeilipa mamilioni kampuni hiyo,kwa kesi hii inayoendelea mwakiembe ameonyesha kuwa si mkweli kwani imethibitika mpaka sasa kuwa RICHMOND hawakulipwa hata senti moja na serekali,na ni kampuni halali iliyosajiliwa Tanzania. IMEDANGANYA

B;DOWAN ISSUE.
Mwakiembe kwenye sakata la dowans alitowa kauli kuwa Mh Zitto kabwe ameehongwa/amepewa rushwa na Tanesco kuwatetea ili dowans inunuliwe,na kauli hii aliitowa kupitia luninga ya ITV lakini kilichotokea ni kuwa alishindwa kuthibitisha na zitto kupitia Tz Daima alituonyesha wa Tanzania kuwa Mwakiembe yeye na kamati yake walilipwa pesa za ziada na tanesco na kupewa posho zilizo kinyume na utaratibu.AMEDNGANYA

C;AJALI ALOPATA HIVI KARIBUNI.
Akiwa kitandani aliweza kutuambia watanzania kupitia ITV na NIPASHE kuwa aligongwa kwa nyuma,na ajali hiyo ni kuundwa,ingawa kamati ya IGP imethibitisha kuwa taarifa za mwakiembe ni za uongo na hazina ukweli ajali hiyoimetokana na uzembe wa dereva wake.AMEDANGANYA

D;SAKATA LA KYELA JIMBONI.
Akiwa mbunge mwakiembe alituaminisha kuwa kuna watu wan mvuruga jimboni na tukio la hivi karibuni la ugomvi kati ya katibu wa ccm na makatibu kata lilitokana na watu wasiomtakia mema,wiki iliyopita wakati anapata ajali alikuwa anatoka ktk kikao cha halmashauri kuu ya wilaya yake,kupitia kikao hicho mwakiembe alionywa kuwa yeye ndie anaesababisha vurugu na anaendesha migawanyiko ndani ya jimbo lake na kutakiwa aache tabia hiyo.AMEDANGANYA

wana jf nimejaribu kuonyesha haya kutokana na imani yangu kwa mwakiembe kuanza kupotea baada ya kuona kila alofanya linakuja kuonekana jambo na kuletea maswali juu ya alicho kifanya,

Leo nimesoma gazeti la Tanzania Daima,na kuona kauli alotowa kashilila katibu wa bunge kuwa mwakiembe kuna vitu anavyo moyoni,najiuliza swali kwanini hakutuambia siku ya kwanza?je anataka kutunga uongo mwingine?au alificha ili iweje?je ni style ile ile ya yeye kusema tutaumbuana?kwani aliposoma ripoti ya Richmond kuna vitu alisema ameamua kuficha,alipoongea na waandishi pale PIKOK HOTELI alisema kuwa anasitiri vitu akonya silazimishwe kulipua vitu vingine na kusema tutalipuana,leo baada ya ajali inajitokeza kauli kuwa kuna vitu anavyo moyoni hajasema,i can see any controvasal thing coming,hapa ndipo credibillity yake inaponitia shaka na kuanza kupoteza imani yangu kwake,hebu tujadili na mnisaidie.
 
walituamiisha kuwa RICHMOND NI KAMPUNI FAKE na serekali imeilipa mamilioni kampuni hiyo
...Walituaminisha? unafikiri hili ni suala la kufikirika.......please calm down ndugu yangu, yaani mpaka leo unafikiri tu issue ya Richmond ni yakufikirika.......unadhani ingekuwa ya kufirikirika kina EL, Karamagi na ''Bangusilo'' wangekubali kirahisi kuachia ngazi?

kwa kesi hii inayoendelea mwakiembe ameonyesha kuwa si mkweli
Hiyo kesi inaendelea wapi.....kisutu, mahakama kuu.....please help hapa! na Mwakyembe ameonyesha vipi kuwa ni mwongo au nani kathibisha huo uwongo wake mkuu?

kwani imethibitika mpaka sasa kuwa RICHMOND hawakulipwa hata senti moja na serekali,na ni kampuni halali iliyosajiliwa Tanzania. IMEDANGANYA
Khaaa! we ni mbongo au umehamia hivi majuzi....yaani umesahau hata yale malipo ya Ths 152m per day ambayo hata Tanesco walikiri kuyalipia?

Kwanza hapa unajichanganya, umesema Richmond ni kampuni halali....na tunajua iliingia mkataba na Tanesco.....sasa kama ni halali na ilifanya kazi halali ya kufua umeme kwa nini isiwe imelipwa mpaka sasa mjomba?

zitto kupitia Tz Daima alituonyesha wa Tanzania kuwa Mwakiembe yeye na kamati yake walilipwa pesa za ziada na tanesco na kupewa posho zilizo kinyume na utaratibu.
Kama unasema Mh. Mwakyembe alishindwa kuthibitisha kauli yake kuwa Mh.Zitto kapokea hela toka dowans, Je. Mh. Zitto yeye alithibitisha wapi na vipi kwamba kamati ya kina Mwakyembe walipokea posho kinyume na utaratibu? au mambo ya double standards?

Akiwa kitandani aliweza kutuambia watanzania kupitia ITV na NIPASHE kuwa aligongwa kwa nyuma,na ajali hiyo ni kuundwa
Acha kuunda meneno yako mjomba....wengi tulimsikia kupitia ITV yes, hakuconfirm kuwa ajali ile iliundwa...yeye alisema, kama ilikuwa planned basi the planner was very smart..........!angalia maneno yake haya hapa:

Mh. Mwakyembe:

``...Mimi ni Mkisto, nimemuachia Mungu hayo, nimesema Mungu kama hiyo, kilichotokea leo, ni binadamu alikipanga basi namshitakia yeye, na kama kilichotokea ni ajali, basi tumuachie Mungu. Lakini kama kilichotekia kilipangawa basi huyo aliyepangwa kufanya hivyo ni mtaalam wa hali ya juu sana maana jinsi alivyoigonga ile gari, kupoteza mwelekeo, mimi kwa kweli nimeiona hiyo, hayo matukio, kwenye sinema tu.``

ingawa kamati ya IGP imethibitisha kuwa taarifa za mwakiembe ni za uongo na hazina ukweli ajali hiyoimetokana na uzembe wa dereva
wake.
Uwongo wa mwakyembe ni upi? yaani mtu aliyekuwepo kny tukio na kamati ambayo haikuwepo wakati tukio linatokea.....hivi wewe unatoa benefit of dought kwa yupi....kamati au Mwakyembe aliyekuwepo pale?

Jiulize hivi mwakyembe aseme uwongo kwa faida ipi hasa mkuu? to me kamati inawezekana haikuwa makini sana wakati inafanya uchunguzi na hivyo kutoa matokea yanayo mislead!

wana jf nimejaribu kuonyesha haya kutokana na imani yangu kwa mwakiembe kuanza kupotea baada ya kuona kila alofanya linakuja kuonekana jambo na kuletea maswali juu ya alicho kifanya,
Wewe inaonyesha hukuwahi kuwa na imani yoyote na Mwakyembe, vinginevyo ungejaribu kuwa obejective kidogo kwenye comments zako!
 
Pole sana fred

Kuna wakati nilishasema humu kuwa Mwakyembe anaishi kwenye dampo, wakati yeye aliposema kuwa Rostam anaoga maji taka. kumbuka.CCM ni dampo!

1.Ni mwanasiasa, kama wengine wowote wale popote pale duniani
2.Ni mwana-CCM watafanya lolote yeye na chama chake kusema lolote au kuwatwist watanzania
3. Analinda jimbo lake kwa chama hicho hicho anachopiga kelele kuwa kuna mafisadi!

Sasa sijui ni lini alishawahi kuwa na credibility!

Viongozi wote wanaojiita wasafi na yet wako ndani ya CCM ni wanafiki!, hawana ujasiri, waoga, wanapenda vyeo, fedha na kutaka chama chao kiwabebe kwa namna yoyote ile!

Nashangaa baadhi ya watanzania kuingia kwenye huu mkumbo vikiwemo vyama vya upinzani!

Nimekuwa ni kiwauliza Chadema mnamsifiasifia Mwakyembe je huko kyela mtamsimamisha mgombe wa Chadema hiyo 2010!!!! hayawezi kujibu yanabaki yanatoa macho!

Hii sio yanga na simba, we need to be strategic!

SIJAONA MSAFI CCM!!!, ANGALAU MREMA ALIONYESHA NJIA!! wote wako kukilinda chama , chama kile kile tulichokipa miaka 40 lakini wameshindwa kazi!

mkumbo huu wa kuwagawa CCM wasafi na wachafu umewakumba wengi wakiwemo wapinzani pasi kujua CCM wasafi ni CCM na CCM wachafu wote ni CCM.

Top yote ya CCM ni walewale akina Rostam, Lowassa, Karamagi!!!!!!!! n.k
 
Pia wiki mbili zilizopita wakati anafungua tawi la CCM Kyela alitamka bila hata kutoa ushahidi mmoja kwamba kuna milioni 400 zimetengwa kummaliza kisiasa Kyela na tayari milioni 5 imepewa kata moja. Akaanza kumhusisha kijana mmoja bila hata kutoa chembe ya ushahidi kuonyesha huyo kijana ana uhusiano hata mdogo na hao anaowaita mafisadi.

Kwa kweli Mwakyembe na ukweli ni vitu viwili mbali mbali kabisa. Anajua kweli kutafuata ukweli wa wengine lakini yeye sio msema ukweli?

Kwa taarifa zenu tu tayari halmashauri ya wilaya inashughulikia malalamiko ya madiwani kwamba michango kwa ajili ya Kyela kupitia NGO ya akina Mwakyembe (KDF) haijafika Kyela. Wajumbe wameomba atafutwe mtu huru kuchunguza pesa zilizochangwa tokea 2006 mpaka leo, mbunge anapiga chenga na toka aunde hiyo KDF hajawahi hata siku moja kutoa mahesabu yake kwenye halmashauri ya wilaya.

Mwulizeni hilo na muone kama atakanusha. KDF inaongozwa na yeye na wezi wengine akiwemo Kifukwe aliyefukuzwa kazi kwa ufisadi Nordic na pia mtunza fedha ni jamaa mmoja alikuwa mkurugenzi wa fedha na utawala NMB, naye kafukuzwa kazi kwa wizi.

Hawa CCM wote ni mafisadi tu, kama kuna wasafi ni wa kuhesabika lakini Mwakyembe sio mmojawapo.
 
Pole tena Fred kwa kupoteza muda kumzungumzia mtumishi wa Mungu Mwakyembe... Mungu akusamehe hujui utendalo

Wakati Yesu alipokufa msalabani neno la mwisho alisema

"Ee Mungu uwasamehe maana hawajui walitendalo..." si vyema Mwakyembe kuanza kulumbana na wewe..... ashakusamehe
 
Next Level uko makini, maana inaonekana kuna nguvu moja kubwa sana inahangaika kumwangusha Dk Mwakyembe nina mashaka hata JK huenda nae yumo! Lakini wanakosea wanafanya haraka mno kumuandama ilitakiwa wasubiri tena wawe kimyaa kabisa labda hata baada ya miaka 5 hivi ndiyo wafanye huo uovu wao.

Lakini sasa hivi tunashtuka,....bado hakuna kosa lolote alilonalo Mwakyembe ukilinganisha na makosa ya mafisadi kama Rostam linaloweza kumfanya apungue credibility yake.

Ni kweli mafisadi wako smart kwenye kushughulikia maadui zao kwani pia huwa shirikisha UWT, lakini wanafanya makosa ya wazi kwenye plan zao ovu, wenye uwezo wa kufikiri tunawashtukia mapema tu.
 
Kwa kweli Mwakyembe na ukweli ni vitu viwili mbali mbali kabisa. Anajua kweli kutafuata ukweli wa wengine lakini yeye sio msema ukweli?

Engineer, mbona kauli yako inapingana na mtoa mada? mwenzio kasema Mwakyembe ni Mwongo kwa kila kitu.......wewe unasema, anajua kweli kutafuta Ukweli wa wengine......mi nilifikiri ungesema anajua kweli kutafuta uwongo kuhusu wengine..au vidole vimeteleza?
 
Pia wiki mbili zilizopita wakati anafungua tawi la CCM Kyela alitamka bila hata kutoa ushahidi mmoja kwamba kuna milioni 400 zimetengwa kummaliza kisiasa Kyela na tayari milioni 5 imepewa kata moja. Akaanza kumhusisha kijana mmoja bila hata kutoa chembe ya ushahidi kuonyesha huyo kijana ana uhusiano hata mdogo na hao anaowaita mafisadi.

Kwa kweli Mwakyembe na ukweli ni vitu viwili mbali mbali kabisa. Anajua kweli kutafuata ukweli wa wengine lakini yeye sio msema ukweli?

Kwa taarifa zenu tu tayari halmashauri ya wilaya inashughulikia malalamiko ya madiwani kwamba michango kwa ajili ya Kyela kupitia NGO ya akina Mwakyembe (KDF) haijafika Kyela. Wajumbe wameomba atafutwe mtu huru kuchunguza pesa zilizochangwa tokea 2006 mpaka leo, mbunge anapiga chenga na toka aunde hiyo KDF hajawahi hata siku moja kutoa mahesabu yake kwenye halmashauri ya wilaya.

Mwulizeni hilo na muone kama atakanusha. KDF inaongozwa na yeye na wezi wengine akiwemo Kifukwe aliyefukuzwa kazi kwa ufisadi Nordic na pia mtunza fedha ni jamaa mmoja alikuwa mkurugenzi wa fedha na utawala NMB, naye kafukuzwa kazi kwa wizi.

Hawa CCM wote ni mafisadi tu, kama kuna wasafi ni wa kuhesabika lakini Mwakyembe sio mmojawapo.

Hey mbona tuliaminishwa hapa kuwa Mwakyembe ni shujaa, kamanda, mpiganaji, kiboko ya mafisadi nk.

Kulikoni tena?
 
Hoja yako ina harufu ya ufisadi. Ume-miss point kwenye kila aya uliyoandika. Unapotosha hoja zote zilizotolewa na mpiganaji huyu kwa makusudi au kwa kutoelewa. Rejea tena report ya Kamati ya Bunge kuhusu Richmond kabla hujatoa hoja yako. Halafu utambue kwamba ile ni ripoti ya Bunge na sio ya Mwakyembe.
 
wana Jf baada ya kutokea ajali ya Mh mwakiembe nimejaribu kufatilia baadhi ya matukio yalo muhusu mh huyu.
A; richmond case.
nimeangalia na kufatilia kesi inayoendelea kuhusu richmond kutokana na riporti ya mwakiembe bungeni walituamiisha kuwa RICHMOND NI KAMPUNI FAKE na serekali imeilipa mamilioni kampuni hiyo,kwa kesi hii inayoendelea mwakiembe ameonyesha kuwa si mkweli kwani imethibitika mpaka sasa kuwa RICHMOND hawakulipwa hata senti moja na serekali,na ni kampuni halali iliyosajiliwa Tanzania. IMEDANGANYA

You are too late and lack objectivity.My question to you is whats your next step? to bring back Lowassa?
 
Pia wiki mbili zilizopita wakati anafungua tawi la CCM Kyela alitamka bila hata kutoa ushahidi mmoja kwamba kuna milioni 400 zimetengwa kummaliza kisiasa Kyela na tayari milioni 5 imepewa kata moja. Akaanza kumhusisha kijana mmoja bila hata kutoa chembe ya ushahidi kuonyesha huyo kijana ana uhusiano hata mdogo na hao anaowaita mafisadi.

Kwa kweli Mwakyembe na ukweli ni vitu viwili mbali mbali kabisa. Anajua kweli kutafuata ukweli wa wengine lakini yeye sio msema ukweli?

Kwa taarifa zenu tu tayari halmashauri ya wilaya inashughulikia malalamiko ya madiwani kwamba michango kwa ajili ya Kyela kupitia NGO ya akina Mwakyembe (KDF) haijafika Kyela. Wajumbe wameomba atafutwe mtu huru kuchunguza pesa zilizochangwa tokea 2006 mpaka leo, mbunge anapiga chenga na toka aunde hiyo KDF hajawahi hata siku moja kutoa mahesabu yake kwenye halmashauri ya wilaya.

Mwulizeni hilo na muone kama atakanusha. KDF inaongozwa na yeye na wezi wengine akiwemo Kifukwe aliyefukuzwa kazi kwa ufisadi Nordic na pia mtunza fedha ni jamaa mmoja alikuwa mkurugenzi wa fedha na utawala NMB, naye kafukuzwa kazi kwa wizi.

Hawa CCM wote ni mafisadi tu, kama kuna wasafi ni wa kuhesabika lakini Mwakyembe sio mmojawapo.

Aibu iliyoje na si kawaida kwa injinia kuwa mzushi.Kwa vile maandiko yako hayana ushahidi wowote isipokuwa kutoelewana kwako na Mwakyembe , basi hayo maneno yanalingana na haiba yako.MZUSHI
 
FRED, nadhani you have been taken to the NEXT LEVEL....sijajua lengo lako ni lipi?? lakini huu ndio uhuru wa kujiexpress tuliokuwa nao...tatizo umemhukumu kabisa kwa hoja zako unazoona zinanguvu kwamba..AMEDANGANYA..at least ungeleta kama hoja na kutaka ku-question his credibility...angalia bwana sio watanzania wote sio makini...people knows the fact..unaweza kuleta propaganda zikagonga ukuta...
huwezi ukaziamini report za polisi kuhusu ajali ya mwakyembe..liko wapi gari lililosababisha ajari, hivi kweli gari kubwa linaweza likapotea kirahisi njiani??? na gazeti la leo limeseme (mwanahalisi)limesema polisi aliyetakiwa kusaidia baada ya ajali hakuwa na msaada mpaka derva alipotokea na kuomba msaada wa magari yanayopita...wewe na akili yako lile shimu ni la kuangusha l/cruiser???
kesi za dowans/richmond kama hazina ukweli wowote basi akina lowasa wangekata rufaa na kutaka wasafishwe....

ila lazima tukubali kwamba wapiganaji walioko CCM lazima ifike hatua watoke tuwaweke mstari wa mbele katika mapambano, otherwise watakuwa hwana msaada kwetu....
 
Pole sana fred

Kuna wakati nilishasema humu kuwa Mwakyembe anaishi kwenye dampo, wakati yeye aliposema kuwa Rostam anaoga maji taka. kumbuka.CCM ni dampo!

1.Ni mwanasiasa, kama wengine wowote wale popote pale duniani
2.Ni mwana-CCM watafanya lolote yeye na chama chake kusema lolote au kuwatwist watanzania
3. Analinda jimbo lake kwa chama hicho hicho anachopiga kelele kuwa kuna mafisadi!

Sasa sijui ni lini alishawahi kuwa na credibility!

Viongozi wote wanaojiita wasafi na yet wako ndani ya CCM ni wanafiki!, hawana ujasiri, waoga, wanapenda vyeo, fedha na kutaka chama chao kiwabebe kwa namna yoyote ile!

Nashangaa baadhi ya watanzania kuingia kwenye huu mkumbo vikiwemo vyama vya upinzani!

Nimekuwa ni kiwauliza Chadema mnamsifiasifia Mwakyembe je huko kyela mtamsimamisha mgombe wa Chadema hiyo 2010!!!! hayawezi kujibu yanabaki yanatoa macho!

Hii sio yanga na simba, we need to be strategic!

SIJAONA MSAFI CCM!!!, ANGALAU MREMA ALIONYESHA NJIA!! wote wako kukilinda chama , chama kile kile tulichokipa miaka 40 lakini wameshindwa kazi!

mkumbo huu wa kuwagawa CCM wasafi na wachafu umewakumba wengi wakiwemo wapinzani pasi kujua CCM wasafi ni CCM na CCM wachafu wote ni CCM.

Top yote ya CCM ni walewale akina Rostam, Lowassa, Karamagi!!!!!!!! n.k
mkuu heshimaa..

mwakyembe hana lolote ni mviziaji tuu wa political capital kwani kwa sasa anatapatapa tuuu..

nashukuru jeshi la polisi limekamilisha uchunguzi wa ajaili yake na dereva wake atapanda kizimbani ili haki itendekee..

huwezi kuwa na malalamiko ya kitoto kila siku kwamba nafuatwa, naonewa, namalizwa nk nk wakati wote unaowalalamikia na kuwahisi ndo wafadhili wa chama lako lilnalokupa KULA wewe na wote nyuma yakoo..

Usomi wa namna hii unaturudisha nyumaaa..MWAKYEMBE ukombozi wako ni elimu ulopata kwa taabu ya mzazi wako na kodi ya taifa hilii..vyeo vyote ulivyowahi na ulivyonavyooo ni matokeo tuuu ya msingi huooo..

sasa kama mafisadi huwapendi kweli (kwa dhati) ya nini kungangania CCM wakati msingi wa chama hicho kwa sasa ni UFISADIIII.....???? MREMA HAKUPENDA KUITESA NAFSI YAKE ALIHAMAAAAA...LEO NI MIAKA 14 BADO NI MTU WA KUHESHIMIWA KATIKA JAMII...

CCM SI MAMA YAKO...NA KAMA UNAIPENDAAA KWA KUKUPA ULAJIII KAA NA UFISADI WAKO NA USITUHADAE WEWE NI MPINGA UFISADIIIIIII.

GET WELL SOONER!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hey mbona tuliaminishwa hapa kuwa Mwakyembe ni shujaa, kamanda, mpiganaji, kiboko ya mafisadi nk.

Kulikoni tena?

Masatu, sasa wewe unaaminije? Kuwa Mwakyembe ni shujaa, kamanda, mpiganaji..... au ni Msanii? Tupe msimamo wako.
 
Nipashe
Ripoti ya Kamati ya IGP iliyoundwa kuchunguza ajali aliyopata Mbunge wa Kyela, Dk. Hurrison Mwakyembe wiki iliyopita imeanika yote kuhusiana na ajali hiyo lakini inadaiwa kuongeza giza nene kutokana na maswali kadhaa ya baadhi ya watu wanaofuatilia sakata hilo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya kitaalam na ambayo iliongozwa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, James Kombe, ni kwamba chanzo cha ajali hiyo ni ni uzembe wa dereva wa Mheshimiwa Mwakyembe aitwaye Joseph Msuya.

Maelezo ya ripoti hiyo ya kitaalam, yanatofautiana kwa kiasi kikubwa na yale yaliyowahi kutolewa na dereva Msuya na hata Mheshimiwa Mwakyembe, hivyo kuibua giza hilo nene la maswali kuhusiana na ukweli hasa wa chanzo cha ajali hiyo.

Katika ripoti hiyo, Kamati imesema kuwa uzembe wa dereva Msuya ndio uliosababisha ajali hiyo mbaya iliyotokea alhamisi iliyopita, mishale ya saa 1:10 asubuhi pale Iringa, kati ya maeneo ya Ihemi na Ifunda.

Kwa mujibu wa sehemu ya ripoti hiyo iliyosomwa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, James Kombe, dereva Msuya alikuwa akiendesha gari hilo kwa mwendo mkali kiasi cha kushindwa kulimudu gari hilo aina ya Toyota Landcruiser, lenye namba T 362 ACH na kusababisha ajali.

Aidha, imedai kamati hiyo kuwa wakati wa ajali, Dk. Mwakyembe alikuwa usingizini, tofauti na maelezo ya awali ya Mheshimiwa Mwakyembe aliyesema aliiona ajali hiyo na namna dereva wa lori alivyochangia kutokea kwake.

Kutokana na yale yaliyogunduliwa na kamati hiyo, sasa kibao kimegeuka baada ya Kamanda Kombe kumuagiza Kamanda wa Polisi mkoani Iringa, Advocate Nyombi, kumkamata dereva Msuya na kumburuza kortini kutokana na makosa matatu, likiwemo lile la kuendesha gari kwa mwendo wa kasi na kusababisha ajali iliyomletea maumivu Mheshimiwa Dk. Mwakyembe.
Kufuatia maamuzi hayo ya kamati, Alasiri iliwasiliana na Kamanda Nyombi leo asubuhi.

Yeye akasema kwa mujibu wa utaratibu, ni lazima atekeleze maagizo ya tume hiyo, ambayo ni kumkamata dereva Msuya na kumburuza kortini.

Hata hivyo, akasema bado hawajamtia mbaroni dereva Msuya kwa vile suala hilo la kumsaka mtu na kumkamata lina mchakato wake.

"Ninatekeleza maagizo niliyopewa na kamati... hata hivyo, hadi sasa sijamkamata maana kumkamata mtu ni mchakato," akasema Kamanda Nyombi.

Alipotakiwa kueleza iweje maelezo yake ya awali yakatofautiana na baadhi ya amelezo ya ripoti ya uchunguzi wa kamati, Kamanda Nyombi amekataa kuzungumzia lolote juu ya ripoti hiyo, kwa madai kuwa imeandaliwa na mabosi wake.

"Uchunguzi umefanywa na mabosi wangu, kazi yangu ni kutekeleza maagizo na siwezi kuzungumzia lolote juu ya ripoti hiyo," akasema Kamanda Nyombi.

Katika maelezo yake ya awali, Kamanda Nyombi alidai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni gari la Dk. Mwakyembe kulivaa shimo lililokuwa katikati ya barabara na hivyo tairi likachomoka na gari likapoteza mwelekeo kabla ya kuingia porini na kupinduka mara nne.

Hata hivyo, dereva wa gari la Dk. Mwakyembe, Bw. Msuya, alidai kuwa alipata ajali wakati akijaribu kulipita lori, ambalo lilimgonga kwa nyuma na kusababisha apoteze mwelekeo na kupinduka.

Dereva huyo akadai kuwa kabla ya kumgonga alijaribu kulikwepa lori bila mafanikio, hali iliyoibua hisia kuwa huenda ajali hiyo ilikuwa na mkono wa mtu, hasa kwa vile ilimhusisha miongoni mwa wabunge wanaosimama kidete katika kupiga vita ufisadi nchini.

Aidha, Mheshimiwa Mwakyembe naye alidai kuwa gari lake likiwa katika mwendo wa kasi, lilitaka kulipita lori lililokuwa mbele yao.

Akasema dereva wa lori aliwaruhusu kupita, lakini wakati wakikaribia kulivuka lori hilo lisilokuwa na namba, dereva wake huyo akalipindisha upande wao na kusababisha ajali mbaya ambayo yeye alisema anamuachia Mungu hata kama kweli ina mkono wa binadamu.

"Nadhani kamati imefanya kazi yake vizuri. Hata hivyo, ilipaswa kueleza japo kwa uchache kuhusiana na lori ambalo inadaiwa halikuwa na namba na hata baada ya ajali bado halikuweza kusimama," akasema mkazi mmoja wa Sinza Jijini.

"Giza jingine kuhusiana na ajali hii ni huku kutofautiana kwa maelezo... nadhani huko mahakamni kila kitu kitafahamika," akadai mwananchi mwingine aliyezungumza leo na mwandishi wa Alasiri...

kuna siku uongo hatimaye utajitenga tu, huwezi danganya watu wote all the time, ndiyo siasa zetu za kibongo
 
Back
Top Bottom