Habari mbaya kwa Wapenzi wa Samsung Galaxy ulimwenguni

Habari mbaya kwa Wapenzi wa Samsung Galaxy ulimwenguni

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
1,322
Reaction score
2,694
Samsung itaweza kuachia Teknolojia mpya ya Privacy Display kwenye Baadhi ya model ya Simu mpya ya Galaxy S27 sio zote.

Kwa ufupi tu Privacy Display Ni teknolojia ya ndani ya OLED inayo punguza sana kile ambacho mtu aliye pembeni anaweza kuona kwenye screen yako.

Tofauti na privacy glass ya kawaida, imejengwa moja kwa moja kwenye display kwa kutumia teknolojia ya Samsung Display ya Flex Magic Pixel. Unaweza kuitumia kwenye screen nzima au baadhi ya apps/maeneo yenye taarifa nyeti

Sasa kwenye toleo jipya la Galaxy S27 Kuna baadhi ya model zitapata zingine hazitaweza kuzipata kabisa kama ifuatavyo:
✅ Galaxy S27 Pro — inaripotiwa kupata Privacy Display.
✅ Galaxy S27 Ultra — pia inaripotiwa kupata.
❌ Galaxy S27 na S27+ — ripoti ya hivi karibuni inasema huenda zisipate Kabisa.
❌ Galaxy S27 FE — pia inaweza isipate hii feature.

Kwaiyo hi Teknolojia inaweza kuletwa kwenye Baadhi ya matoleo sio kwa watu wote 👋.
 
Back
Top Bottom