Gundu la kinyesi

Da mkuu nashukuru ka maelezo japo kwa nilichokishuhudia mimi hujakielezea.
1)Niliota ndoto niko bafuni naoga katika bafu chafuu yaani bovu bovu tuu halafu ghaflaa kutazama chini nikaona kuna mavi na inzi wapo kiasi Baada ya kuona tuu kisha ghaflaa nikashituka.
2)Nilikuwa kwenye bafu safii,full tiles mpaka ukutani. nikiwa bado naweka maji kwenye ndoo ili nioge ghafla kwenye ndoo naona kinyesi yaani kinyesi kabisaa. Nikasema hii kitu imetoka wapii,nikabeba ndoo nikaelekea kwenye choo ambacho kilikuwa kinajengwa,nikaenda kwenye tundu la kupitishia uchafu.
Ghaflaa nikaona mtu mwanamke amejifunga khanga yuko mabega wazi, anaingia humo chooni,nikamwambia kuna mtu usiingie lakini aliingia tuu kisha akiwa kama ananishangaa wakati namimina ule uchafu akaniuliza, "Hebu nielekeze unafanyajee fanyajee"..... Kisha nikazindukaa.
je,mkuu mshana,hapo kunanii???
 
Ngoja nitulie takujibu kwa ufasaha moja baada ya nyingine
 
Gundu sio kiambishi,gundu ni nomino
 
Naanza kuona ukweli wa hayo usemayo miaka ya 2009 nilifungua biashara ya kuuza Gas za kupikia wakati ninaanza biashara ilikuwa nzuri sana nilianza na Mitungi 30 ikawa namaliza ndani ya siku 1 au 2 na ikafikia kipindi ili nisifukuze wateja wangu ilinilazimu nikiishiwa niwe nachukua Gas kwa wenzangu kwa bei ya reja reja wakati nasubiri Suppliers aniletee mzigo.
Mambo yaliharibika baada ya siku moja asubuhi wakati dada anaenda kufungua duka alikuta Kinyesi cha haja cha mtu mzima katikati ya mlango wa duka , toka hapo biashara ikawa ngumu na ndani ya miezi 3 nikafunga kabisa.
 
Wabaya walikuwa hao majirani zako..next time usirudie kufanya hivyo tena..kama huna mzigo mwambie mteja ndio aende mwenyewe kwa jirani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…