Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Rais wa Guatemala Alvaro Colom na mkewe Sandra Torres wamewasilisha shauri mahakamani nchini humo kuomba kutalikiana (divorce) kwa utashi wao wenyewe.
Hatua hii inakuja ili kumuwezesha mwanamama huyo kugombea urais wa nchi hiyo katika uchaguzi utakaofanyika nchini humo mwezi Septemba mwaka huu.
Katiba ya nchi hiyo inakataza watu wa karibu wa familia ya Rais aliye madarakani kama vile mke, mume, mtoto, mjukuu etc kugombea urais wa nchi hiyo.
My take:
Kipengele hiki cha Katiba kinafaa pia kuwepo katika Katiba yetu, na yumkini katika katiba za nchi nyingi tu za Kiafrika ili kuzuia urais kurithiriana kifamilia. Au mnasemaje wadau?