Guatemala: Kipengele cha Katiba yao kinafaa kuwepo kwetu pia

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233


Rais wa Guatemala Alvaro Colom na mkewe Sandra Torres wamewasilisha shauri mahakamani nchini humo kuomba kutalikiana (divorce) kwa utashi wao wenyewe.
Hatua hii inakuja ili kumuwezesha mwanamama huyo kugombea urais wa nchi hiyo katika uchaguzi utakaofanyika nchini humo mwezi Septemba mwaka huu.
Katiba ya nchi hiyo inakataza watu wa karibu wa familia ya Rais aliye madarakani – kama vile mke, mume, mtoto, mjukuu etc – kugombea urais wa nchi hiyo.

My take:
Kipengele hiki cha Katiba kinafaa pia kuwepo katika Katiba yetu, na yumkini katika katiba za nchi nyingi tu za Kiafrika ili kuzuia urais kurithiriana kifamilia. Au mnasemaje wadau?


 
nimecheka kweli leo asubuhi niliposikia hii kitu kupitia BBC.....kwa keli ni nzuri
 
duh inafurahisha sana hii.
Baada ya uchaguzi si watakuwa mahawara hao?
La kumzuia mtoto ni zuri zaidi na rahisi kuimpliment
 
Ndoa nyingine balaa,madaraka yanawafanya watengane..? Hawa lazima walikubaliana kuwa pamoja katika raha tu..!
 
Hii inapendeza kuwa kwenye katiba yetu pia, ebu fikiri miaka kumi ikijirudia kwa ombwe la uongozi tulilonalo, unategemea Tz ya miaka 30 ijayo itakuwaje?
 
Imenichekesha sana hii habari, ikija hapa TZ itatafasiriwa sheria ya kumkana mtooto ili aweze kugombea.
 
Napenda kipengele has kuzuia watoto na ndugu wa karibu. Mke naye hata kama wataachana na mumewe asipate nafasi maana naye ameshatawala akiwa ikulu kwa njia moja au nyingine!!
 
Mke wa rais wa Guatemala ameamua kuivunja ndoa yake ya miaka minane ili aweze kugombea urais.
Mahakama ya nchini Guatemala imeanza kusikiliza kesi ya mke wa rais wa Guatemala ambaye ameenda mahakamani kudai talaka ili kuivunja ndoa yake ya miaka minane na rais Alvaro Colom.

Mke huyo wa rais, Sandra Torres de Colom ameamua kuivunja ndoa yake ili aweze kuwania kiti cha urais ambacho mume wake atakiachia atakapomaliza muda wake mwezi septemba mwaka huu. Mume wake anamaliza miongo yake miwili ya uongozi na hataruhusiwa kugombea tena urais.

Sheria za Guatemala zinakataza watu wa familia ya rais kushiriki kwenye uchaguzi wa kugombea urais.

Sandra alitangaza wiki iliyopita kuwa atagombea urais mwaka huu kwa kupitia chama tawala National Unity for Hope party.

Kama rais Colom atakubali kutoa talaka kuivunja ndoa yake basi Sandra ataruhusiwa kisheria kugombea urais.
5547822.jpg
 
kheee jamani dunianai kuna mambo...sasa wanavunja hii kitu officially tu lakini nyuma ya pazia wanagongana au???
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom