Kiuhalisia mwezi wa tisa unaitwa ni mwezi wa shetani
mabalaa yote hutokea mwezi huu, mwezi huu huwa una vifo vingi sana
Vielelezo vinasema ajali zimeongezeka. Mtanzania anakupa majibu ya sababu za ajali, kwamba
"ni mwezi wa shetani."
Unajua, wengine labda tuna ka bahati mbaya fulani ka kutembelea kidogo nchi za wenzetu za waliopiga hatua, sasa wanapokuwa wanaongelea takwimu zimeonyesha ajali zime spike mwaka huu, au mwezi huu, huwezi kusikia hata kidogo, hata siku moja, katika nchi ya watu milioni mia moja, huwezi kusikia hata kiumbe kimoja kinakwambia "ni mwezi wa shetani." Kwa hiyo wengine tukisikia hayo hushtuka.
Sasa unapokuwa na jamii ya watu wa aina hii, wenye ma imani na mapokeo ya ajabu ajabu kama haya, jamii ya kizazi ambacho bahati mbaya hatukupata elimu nzuri, then huwezi kupunguza ajali, huwezi kupiga maendeleo ya infrastructure safety, huwezi kufanya chochote kama nchi. Mchangiaji mmoja mwenye imani kali, Max Shimba, huuliza, kama wewe huna imani then inakusumbua nini mpaka kuhangaika kujaribu ku disprove na kupinga imani za wengine za mamungu na mashetani ambayo unasema hayapo anyway?
Well, ni mambo kama haya sasa, yani ma imani haya yanatu-affect wote kama taifa. Badala ya kujiuliza kiweledi tufanye fanye fanyeje tupunguze ajali, tuongeze usalama barabarani, tuepuke vifo vinavyozuilika, Mtanzania anakwambia mwezi wa tisa "ni mwezi wa shetani." Nothing short of ridiculous.
Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe'
Kwa lipi?
Jina lake lihimidiwe kwa wale waliopona au kwa wale waliokufa au kwa kuumba watu ili waje wafe kikatili kwenye ajali au ni kwa lipi hapa hasa hasa tunalotaka jina la bwana lihimidiwe kwalo? Kwa nini atoe halafu atwae kikatili kwa watu kuchomwa na mavyuma mazito machoni na shingoni na sehemu za siri na midomoni mpaka wafe? What's his point? Ahimidiwe kwa lipi?
Madereva nendeni mwendo mzuri.kuweni makini barabarani.Tumepoteza wa Tanzania wenzetu wengi,inasikitisha.Hakika sisi ni wa Mwenyeenzi Mungu,na kwake tutarejea.
Then there is no point ya kuwa makini.
Huwezi kutuambia madereva twende mwendo mzuri, tuwe makini, halafu unasema sisi ni wa Mungu na kwa Mungu tutarejea. Inakuwa hakuna faida ya kuwa makini, why bother?
Manake kwa Mungu tutarejea anyhow!
One of these days tuwe makini tusiwe makini Mungu atatupangia kifo cha kikatili na cha kishetani barabarani anyhow! Na ni kitu chema kabisa kufa kikatili kwa mipango ya Mungu kwa sababu kazi ya Mungu haina makosa!