Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 7,574
- 13,311
Kulikuwa na hekaya kuwa huko juu milimani kuna bonde ambalo wakazi wake wote ni vipofu. Siku moja mpanda milima mmoja kwa bahati mbaya aliteleza na kuporomokea kwenye bonde refu sana. Bonde lililokuwa limezungukwa na milima iliyosimama wima pande zote. Bahati akakuta kuna watu wanaishi. Akakumbuka hekaya za kuwepo kwa bonde la vipofu milimani huko. Akili yake ikamkumbusha msemo, KWENYE NCHI YA VIPOFU MTU MWENYE JICHO MOJA NI MFALME.
Basi akawa na mawazo mengi ya jinsi atakavyowaongoza watu wale na kuwafundisha mambo mengi. Lakini baada ya kukutana na watu wenyewe, ni kweli wote walikuwa vipofu, lakini walikuwa na utaratibu wao mzuri wa maisha walioufuata. Maisha yao yote hawakuwahi kusikia habari ya kuona. Bwana yule alipoanza kuwaeleza habari za kuona wakamuona kama kachanganyikiwa.
Alipowaambia kuwa mchana ndiyo muda mzuri wa kufanya kazi na si usiku walimuona punguani kabisa. Walimwambia kuwa usiku ndiyo muda sahihi wa kufanya kazi sababu hakuna joto, joto linapoanza asubuhi ni muda wa kulala. Kwao tofauti ya mchana na usiku ilikuwa ni joto wala si uwepo wa mwanga.
Na hata walipopapasa macho yake na kuona yanachezacheza walimuona kuwa ni kiumbe duni sana. Basi akawa ndiye kiumbe anayedharaulika kuliko wote kwenye bonde lile. Na maneno KWENYE NCHI YA VIPOFU MTU MWENYE JICHO MOJA NI MFALME yakawa mwiba kichwani mwake.
Mwishowe wakaamua wamtoboe macho, maana waliona kuwa yanavyochezacheza yanasababisha na akili yake nayo iwe inachezacheza.
Bwana yule angetumia njia gani ili kueleweka na vipofu wale?