Mtazamo: Tundu Lissu atafanikisha Godbless Lema kuondoka nchini Kenya na kupata hifadhi katika nchi mojawapo ya Ulaya au Marekani

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,011
144,371
Kwa mtazamo wangu, pamoja na Godbless Lema na familia yake kupewa hifadhi ya kisiasa nchini Kenya, Lema na familia yake watakuwa salama zaidi iwapo wataishi nje ya region hii ya Afrika Mashariki na zaidi wakiwa Ulaya,Marekani au kwingineko licha ya ukweli kuwa hadhi ya ukimbizi aliopewa nchini Kenya inatosha kumhakikishia usalama wake.

Hivyo, ninaamini Tundu Lissu akiwa nchini Ubelgiji, anaweza kufanya mipango /kushawishi nchi za ulaya hasa Ubelgiji atakokuwa anaishi, kuhakiisha Lema na familia yake wanahama nchini Kenya na kwenda kupata hifadhi katika mojawapo ya nchi za Ulaya,Marekani au katika nchi nyingine tofauti na Kenya ambapo anaweza kukaa kwa muda tu.

Ni imani yangu pia Lissu atafanikisha mambo mengi ya kusaidia wapinzani wenzake pamoja na vyama vya upinzani akiwa huko ughaibuni-anakwenda kuanzisha movement za kusaidia mabadiliko akiwa huko Ulaya pasipo kuvunja au kukiuka mashariti ya kupewa hifadhi katika nchi za watu.

Muda utaongea.
 
Cha Msingi na wengine wote nao wafanikiwe kuondoka hasa Mbowe, Mdee, Sugu, Bulaya, Heche, Wenje, Matiko, Catherine, Jay, Msigwa, Zitto, Jusa, Manzrui, Seif, Duni na Nusrat
 
Nini mustakabali wa CHADEMA sasa?

Kwishney??
Kwani Chadema ni viongozi au wanachama wake? kama unadhani ni viongozi hawa waliopo huwaoni?

Lissu aliondoka then akarudi bado akawa na impact kubwa tu, bado hujifunzi? na Lema pia itakuwa hivyo hivyo.

Chadema ilikuwepo, ipo, na itaendelea kuwepo.

That day hawa watu wakirudi moto utawaka vile vile, spirit never die.
 
Hivi usanii wa chadema utaisha lini? Wananchi wameshawashutukia, uchaguzi uliopita ni kupimo tosha. Nauliza majina ya wabunge wa viti maalum ni yepi? Maana naona kama mnataka kupindua meza kwa kuweka ama ndugu zenu au wake zenu!! Chadema ni usanii tupu
 
Hivi usanii wa chadema utaisha lini? Wananchi wameshawashutukia, uchaguzi uliopita ni kupimo tosha. Nauliza majina ya wabunge wa viti maalum ni yepi? Maana naona kama mnataka kupindua meza kwa kuweka ama ndugu zenu au wake zenu!! Chadema ni usanii tupu
Unapiga kelele kwa kuona vitu feki!, vilivyotengenezwa lumumba.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom