Godbless Lema avuliwa ubunge

Status
Not open for further replies.
hahaaha....pole, naona umekuwa mpoleee!
Hongera sana kwa kutoa ile Prefix kwenye jina lako cuz ulikuwa unadhalilisha sana!!

Naona ulikuwa unauguza majeraha tangu jpili jioni..., utaugua tena muda si mrefu Arusha inakuja.
 
inauma saaana. ila sikio la kufa ni lakufa tuu. cdm watalirudisha jimbo.
 
sisi huwa tunashitaki kwa wananchi. ccm mnajifanyia homicide. hamna huruma na watanzania. pesa ya kuendesha uchaguzi ingetumika kwa mambo mengine ya kimaendeleo kwa watu.

Walimu hawapewi mishahara, madawati hakuna! haya wala serikali haijali lakini kurudia uchaguzi utakaogharimu za 20b poa tu! yani tunamaputo huko serikalini! sasa tunasubiri atakayekuja kufungua kampeni za ccm ha ha ha ha! Namuonea huruma mkapa! haha this time mzee kataa unaaibishwa mzee.
 
It is sad day for legal society in Tanzania. Nafikiri lengo lilikuwa ni kutenguliwa matokeo na mahakama ya chini ili mahaka ya rufaa ikaya-upheld kwa muda wanaotaka wao whether ni 2014 au 2015. Kwa kuwa Lema kakataa kukata rufaa, maana yake ni kwamba the precedence stands and will be our new case law in the land. Hii inaua demokrasia na uwezo wa watu kujenga hoja na kuchaza politics. Ila kwa kuwa CCM ni mabingwa wa kutukana majukwaani nimependa hukumu hii kwani inarudisha civility majukwaani na watu sasa watajenga hoja kuombea kura badala ya personal issues.

Kwenye hoja nina hakika CCM haiko salama kwani upepo hauvumii kwao ukiangalia na hali ngumu ya watanzania. Ni njia nzuri kwa CCM kujifariji baada ya kupoteza jimbo la Arumeru ila pia ni njia nzuri kwa CCM kujipigilia misumari kwenye chaguzi zijazo. Ila kibaya zaidi ni kuendelea kuondoa imani ya wananchi dhidi ya mahakama zetu.

Ujumbe kwa Mheshimiwa Lema (Mimi bado ninaamini ni mheshimiwa kwa sababu atashinda uchaguzi wa marudio) ni kwamba hii hukumu ni sehemu ya mapambano dhidi ya ukombozi kamili wa watanzania. Usijisikie unyonge sana kwani mamlaka hutoka kwa mungu, Jipange upya fuata mchakato wa chama wa kuomba uteuzi tena nina imani kuwa chama kitakupatia ridhaa kwa mara ya pili, ni haki yako kikatiba kugombea.
 

Sahau mkuu.Forget forever Arusha kuchukuliwa na MAGAMBA.
 
Pole sana wana Chadema jipangeni na uchaguzi mpya...siasa zina matamu yake na machungu yake.

Ritz, pole sana kwa kichapo Arumeru East. Hata hivyo karibu sana Ars mjini kwa raundi nyingine.
 
mmh....!!! unacheka leo kesho kilio haya sasa tusubiri uchaguzi mwingine tena.Na sijui hizi hela tunazo tumia zatoka wapi wakati wafanyakazi wa serikali wanalia kutolipwa stahili zao.
 
Jamani!!!!
Tatizo ni nchi kuingia kwenye gharama, ila chadema hawajapoteza kiti chao.
 
wewe una ufinyu wa mawazo,huna akili timamu
 
lema amepigwa chini. Reasoning ya jaji inaonyesha alihongwa. The way forward ni kwenda court of appeal. Hata hivyo ccm wahangaika bure maana hata uchaguzi ukirudiwa leo watapigaragazwa kwa mbali

kukata rufaa kutasaidia kuepusha gharama sana kwani mwisho wa siku lema atachaguliwa tena. Cdm inapendwa sana jamani, tuonee huruma kodi zetu. However, nasikia lema kasema yeye hatakata rufaa mahakamani bali atakata rufaa kwa wananchi. Let us wait and see the results after 90 days
 

usiwe unaongea kama punga wewe!!!... au unabwabwaja tu kama umeshikishwa ukuta...
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…