Godbles Lema: Wafanyakazi wengi wa Serikali ni jobless, baadhi wanafanya uovu ili walishe familia

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Leo kwenye Maria Space iliyokuwa na mada ya mfumuko wa Bei man of the space was Lema. Ameongea mambo mazito na muhimu Kwa Taifa Leo.

Moja ya jambo kubwa ninalotaka kushare na wewe ni hili:

1. Tanzania haitaendelea kama hakuna miundombinu ya kisera yakutufanya tuendelee.

2. Wafanyakazi wa serikali ni jobless, wengi kipato chao kwa mwaka ni chini ya milioni 8, wanafanya kazi Lakini ni Jobless. Kipate cha mfanyakazi kwa mwaka ni mtaji wa machinga wengi waliopo masoko makubwa nchini.

Endeleeni kuwahita wenzenu jobless mkasau ninyi pia ni jobles
 
Huyu Lema alikuwa anategemea Ubunge, alipwe million 12 kwa mwezi, itakuwa Bomba imekata , nataka kujua huko nje anafanya mishe Gani?
 
Kisa yeye analishwa na mabeberu ndo anajiona siyo jobless, atuambie anafanya kazi gani huko ughaibuni huyu baba wa nyumbani.
 
Kaongea ukweli mchungu sasa mwalimu wa sekondari au shule ya msingi hawezi kusave hata laki tatu kila mwezi na yuko kazini, matumaini yote anahamishia kujifariji kwenye job security na pension ambayo kwa miaka yote ya kazi kama 30 hatolipwa zaidi ya dola 50000 , akistaafu anakufa mapema maana elimu ya mtaani hana, nawapongeza wafanyakazi wenye mafanikio hasa waliojiongeza kwenye kilimo na biashara na uwekezaji mwingine zaidi.
 
Kaongea ukweli mchungu sasa mwalimu wa sekondari au shule ya msingi hawezi kusave hata laki tatu kila mwezi na yuko kazini, matumaini yote anahamishia kujifariji kwenye job security na pension
kwa hiyo kumbe job security wanayo!

na pesheni wanayo!

basi Lema hawezi kuwa "kaongea ukweli mchungu" kwa saab Lema kasema watumishi ni jobless

joblessness haina job security na haina pensheni

excuse me Sir, but you are contradicting yourself...
 
kwa hiyo kumbe job security wanayo!

na pesheni wanayo!

basi Lema hawezi kuwa "kaongea ukweli mchungu" kwa saab Lema kasema watumishi ni jobless

joblessness haina job security na haina pensheni

excuse me Sir, but you are contradicting yourself...

Lema alichojaribu kujadili ni malipo hafifu ya mishahara ya wafanyakazi, na ndio maana wafanyakazi japo sio wote lakini wengi wao wako kwenye stress zone, hebu mfikirie mwalimu kwa mfano au polisi ambae kutokana na mshahara wake anapata jumla ya mwaka mzima milioni sita hadi nane.

Huyu mtu mwaka unaisha hajasave hata mia moja, huyu akipata mwanya wa kuiba ataiba tu, akipata mwanya wa rushwa atachukua tu maana kazi yake haimfanyi aishi vile anavyotakiwa kuishi hivo anakua sawa na jobless tu sema tofauti ana sehemu ya kwenda kuongelea kila akiamka lakini maslahi ni duni.
 
kwa hiyo kumbe job security wanayo!

na pesheni wanayo!

basi Lema hawezi kuwa "kaongea ukweli mchungu" kwa saab Lema kasema watumishi ni jobless

joblessness haina job security na haina pensheni

excuse me Sir, but you are contradicting yourself...
Wacha kujiliwaza, huwezi kusema umeajiriwa halafu muda wako wote ukiwa kazini unaishi kwa mawazo sababu ya kipato kidogo cha ajira yako.

Wewe kwa miaka yako yote ya utumishi huna tofauti na jobless coz unasubiri mafao ndio ujenge uzeeni, au bahati mbaya kikitokea kifo? huu ni utumwa am sorry Sir, you are contradicting yourself too.
 
Huyu Lema alikuwa anategemea Ubunge, alipwe million 12 kwa mwezi, itakuwa Bomba imekata , nataka kujua huko nje anafanya mishe Gani?
Anaosha masufuria kwenye restaurant. Kumbuka kisomo hana, ufundi hana, kingereza hana, kifaransa hana. Sasa unategemea atafanya kazi gani zaidi ya kuosha masufuria.

Huko aliko anajutia, kwa nini alijidanganya kwenda huko huku akijua alichopoteza ni kiti cha ubunge tu. Angekuwa huku anapiga pesa ya biashara zake.

Alidanganyika na Lissu ambaye hata umachinga hauwezi, sasa analia kilio cha mbwa koko.
 
Kama kweli vile!! Nakumbuka mid 2000 nilikuwa na store yangu pale yombo relini. Wengi ya watu niliokuwa nikiwakopesha ni wafanyakazi. Nampa mchele mchele, unga, sukari, mafuta ya kula wakati mwingine na sabuni.

Mwisho wa mwezi ukifika wanakuja kulipa. Hazipiti siku kumi wanarudi tena kukopa. Yaani mtindo ndio huo. Alichomaanisha lema ni kwamba wanakazi ambazo haziwaondoi kwenye hali waliyonayo.
 
Huyu Lema alikuwa anategemea Ubunge, alipwe million 12 kwa mwezi, itakuwa Bomba imekata , nataka kujua huko nje anafanya mishe Gani?
Tafakari ujumbe wake jiulize anaekufa mapema ni nani Kati ya mfanyanzi na machinga kwa stress za maisha.
 
Back
Top Bottom