Mheshimiwa Rais, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kwa unyeyekevu mkubwa hivi mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF) ni chanzo cha mapato ya Serikali?

omtiti

JF-Expert Member
Jun 19, 2019
1,022
1,590
Salam kwenu vionngozi wangu, imani yangu hamjambo na ni wazima wa afya.

Naleta malalamiko juu ya mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF)ambao upo chini ya ofisi ya waziri mkuu, ikiongozwa na mama Jenista Mhagama (Ajira Kazi na Wenye Ulemavu) Hii ni baada ya kufanyia marekebisho sheria ya fidia kwa wafanyakazi sura namba 263 mwaka 2015.

Natambua nia njema ya kuanzishwa kwa mfuko huu ilikuwa ni kusaidia wafanyakazi wapatao ajali, ulemavu na magonjwa yatokanayo na kazi wanapokuwa wanatimiza majukumu yao.

Na kuanzishwa kwa mfuko huu ilitokana na baadhi ya waajili kutelekeza wafanyakazi waumiapo kazini au wapatapo magonjwa yatokanayo na kazi walizozifanya.

Nikubali moja kwa moja wabunge na serikali kwa ujumla mlifanya jambo jema sana. Tatizo linalojitokeza kwenye mfuko huu kwa sasa ni namna ya kukokotoa mafao ya ugonjwa, ulemavu au ajali itokanayo na kazi.

Kiukweli kikokotoo kimelenga kumuumiza mlemavu, mgonjwa aliepata ajali kazini.

Kikokotoo hiki kinaifanya serikali kukusanya pesa nyingi na kuwalipa waathirika fedha kidogo hivyo serikali imegeuza mfuko huu (WCF) kama chanzo cha mapato yake badala ya kusaidia waathirka.

Naishauri serikali kupitia upya vikokotoo na asilimia au kanuni za mfuko huu ili wagonjwa, walemavu, au waliopata ajali kazini wanufaike nao badala ya serikali kunufaika na mfuko huu kama chanzo cha mapato yake. Inasikitisha fidia kutolewa bila ya muathirika kusikilizwa.

Mfano kabla ya kuanzishwa kwa mfuko huu, mwajiri hakuruhusiwa kumwachisha kazi mwajiliwa mgonjwa au mlemavu aliepata tatizo akiwa kazini.

Mwajili aliwajibika kumtibu muathirika kwa miaka isopungua minane, akimlipa baadhi ya haki zake au kumpa kazi nyepesi kulingana na hali ya muathirika, hivyo mfanyakazi huyo kumudu maisha yake, kwani bima yake ilisaidia na familia yake, na mwisho walifikia muafaka kwa kukaa mezani na kuachana kwa kulipana kwa jinsi watakavyokubaliana.

Kupitia utaratibu huu wafanyakazi walinufaika na malipo mazuri ya fao la kuumia au kupata magonjwa.yatokanayo na kazi.

Tofauti kabisa na (WCF), wamegeuka chanzo cha mapato ya serikali, baadhi ya wahanga wanatambuliwa na mamlaka ya usalama na afya mahala pa kazi (OSHA) lakini mfuko wa WCF huwakataa na kusema magonjwa yao hayatokani na kazi, ni wengi wametelekezwa na mfuko huu.fanyeni uchunguzi

WCF wasema wanatibu kwa miaka miwili, cha ajabu wengine hawafikishi miaka tajwa kwa maana ya miezi(24) kama ilivyokusudiwa kisheria, huingizwa kufanyiwa tathimni ambayo ni ndogo sana kulinganisha na kile ambacho waathirika walikua wakipata toka kwa mwajiri baada ya kukaa nae mezani kabla ya huu mfuko

Mfanyakazi alipokuwa anaumwa na imethibitishwa na OSHA, hakuachishwa kazi bima yake na ya familia yake hazikupokwa na mwajili na zilitibu magonjwa karibu yote katika familia na mashahara alipatiwa.

WCF,wanapokea mtu mgonjwa au mlemavu alieachishwa kazi , Bima yao wanachotibu ugonjwa tajwa tu ,haihusiki ukipata malaria, kuhara, tumbo na kadhalika, wakati kwa mwajili haikuwa hivyo. Bima yake ilikubeba wewe na familia kwa ujumla.

Sasa mateso ni pale mwajili kakupeleka WCF huna ajira ya kuingiza kipato kwa mwezi ni mgonjwa familia inakutegemea, Bima ya WCF wewe pekee ndio inakuhudumia na ni ugonjwa tajwa tu, wakati unatibiwa familia inaishije kimatibabu na kilishe(sick period)?

Naiomba serikali kupitia upya kanuni na vikokotoo vya mfuko huu uwe faraja kwa wahanga na si chanzo cha mapato ya serikali.

Wengi wamehuzunishwa sana na mfuko huu na wanajuta kwa sasa kuanzishwa kwake ispokua sauti zao haziwezi wafikia nyinyi viongozi wakuu ambao ndio mna maamuzi ya nini kifanyike kuleta faraja ilikusuduwa.

Imani yangu mnapita hapa jukwaani kama sio nyie basi wasaidizi wenu watawafahamisha na mtalifanyia kazi kuondoa manunguniko ya wahanga watokanao na athari za kazi walizozifanya.
 
Serikali ijaribu kufanyia kazi haya maoni, kiukweli kuna malalamiko mengi sana kuhusu utendaji wa mfuko huu
 
Kuna.jamaa zangu.wanalia na kusaga meno kuhusu huu huu mfuko,nafikiri nia ilikua njema ispokuwa kanuni na kikokotoo kimelenga kuumiza wananchi,yoyote yule alieshiriki katika kuandaa kanuni na kikokotoo alaaniwe kwa kweli
 
Kwanza nimpongeze mtoa hoja, Mimi ni mmoja wa watu ambao nimefaidika na huo mfuko.. lakini ni vizuri kuuelewa huu mfuko vizuri maana shughuli zake ni fidia tu! waingereza wanaita Compensation.

Ni kweli kuna changamoto kidogo kwenye ukokotoaji wa fidia maana fidia inakokotolewa kwa kutumia mshahara wako na Kiwango cha ulemavu uliopata kutokana na ajali au ugonjwa unaohusiana na kazi yako ukiwa unalipwa mshahara mdogo utapata kidogo ukiwa na mshahara mkubwa utapata kikubwa lakini huu ni mfumo unaotumika kwenye taasisi zote za hifadhi ya jamii duniani! Labda hapa kinachoweza kuboreshwa ni mishahara katika sekta zote za umma na binafsi.

Lakini kwenye suala la kutibiwa miezi 24 sheria iliyoanzisha huo mfuko unasema utatoka kwenye ulemavu wa muda na utaenda kwenye ulemavu wa kudumu ambayo sasa utaanza kuingia kwenye kulipwa pensheni ya kila mwezi haisemi hautaendelea kutibiwa Mtu ataendelea kutibiwa mpaka apate maximum medical improvement.
Lakini pamoja na hayo mgonjwa ambaye hajiwezi kabisa analipwa yeye lakini na mtu ambaye anamuangalia anakua analipwa kiasi cha pesa.

Kwa uelewa wangu OSHA na WCF wana majukumu tofauti japo katika kutathmini kama ugonjwa au ajali uliyopata imetokana na kazi ni jukumu la WCF baada ya kuanzishwa kwa huo mfuko na wao ndiyo wanalipa fidia tofauti na mwanzo kabla ya kuanzishwa kwa huo mfuko labda ambacho kinaweza kuboreshwa hapa ni ushirikiano kati ya hizo taasisi mbili.

Lakini naamini kama ikiweza kuthibitishwa kwamba malaria au kuhara tumbo kunatokana na kazi yako WCF watakutibu.. mfuko wa WCF ni mfuko wa fidia mahususi kwa magonjwa au ajali zinazotokana na kazi tu, shughuli zingine zinafanywa na taasisi zingine za hifadhi ya jamii kama mifuko ya pensheni na bima za afya.

kwa sheria ya WCF mtu mwenye ulemavu wa kudumu analipwa pensheni maisha yake yote.. na mtu akifariki kutokana na ajali au magonjwa yanayotokana na kazi familia yake inapokea pensheni kila mwezi kama fidia ya upotevu wa kipato..

Ni vizuri kusoma sheria za taasisi hii na nyingine za Serikali vizuri nadhani itatusaidia Kuweza kuwashauri viongozi wakuu wa nchi na kuleta maboresho chanya na yenye tija kwa taifa letu kwa ujumla..
 
Salam kwenu vionngozi wangu, imani yangu hamjambo na ni wazima wa afya.

Naleta malalamiko juu ya mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF)ambao upo chini ya ofisi ya waziri mkuu, ikiongozwa na mama Jenista Mhagama (Ajira Kazi na Wenye Ulemavu) Hii ni baada ya kufanyia marekebisho sheria ya fidia kwa wafanyakazi sura namba 263 mwaka 2015.

Natambua nia njema ya kuanzishwa kwa mfuko huu ilikuwa ni kusaidia wafanyakazi wapatao ajali, ulemavu na magonjwa yatokanayo na kazi wanapokuwa wanatimiza majukumu yao.

Na kuanzishwa kwa mfuko huu ilitokana na baadhi ya waajili kutelekeza wafanyakazi waumiapo kazini au wapatapo magonjwa yatokanayo na kazi walizozifanya.

Nikubali moja kwa moja wabunge na serikali kwa ujumla mlifanya jambo jema sana. Tatizo linalojitokeza kwenye mfuko huu kwa sasa ni namna ya kukokotoa mafao ya ugonjwa, ulemavu au ajali itokanayo na kazi.

Kiukweli kikokotoo kimelenga kumuumiza mlemavu, mgonjwa aliepata ajali kazini.

Kikokotoo hiki kinaifanya serikali kukusanya pesa nyingi na kuwalipa waathirika fedha kidogo hivyo serikali imegeuza mfuko huu (WCF) kama chanzo cha mapato yake badala ya kusaidia waathirka.

Naishauri serikali kupitia upya vikokotoo na asilimia au kanuni za mfuko huu ili wagonjwa, walemavu, au waliopata ajali kazini wanufaike nao badala ya serikali kunufaika na mfuko huu kama chanzo cha mapato yake. Inasikitisha fidia kutolewa bila ya muathirika kusikilizwa.

Mfano kabla ya kuanzishwa kwa mfuko huu, mwajiri hakuruhusiwa kumwachisha kazi mwajiliwa mgonjwa au mlemavu aliepata tatizo akiwa kazini.

Mwajili aliwajibika kumtibu muathirika kwa miaka isopungua minane, akimlipa baadhi ya haki zake au kumpa kazi nyepesi kulingana na hali ya muathirika, hivyo mfanyakazi huyo kumudu maisha yake, kwani bima yake ilisaidia na familia yake, na mwisho walifikia muafaka kwa kukaa mezani na kuachana kwa kulipana kwa jinsi watakavyokubaliana.

Kupitia utaratibu huu wafanyakazi walinufaika na malipo mazuri ya fao la kuumia au kupata magonjwa.yatokanayo na kazi.

Tofauti kabisa na (WCF), wamegeuka chanzo cha mapato ya serikali, baadhi ya wahanga wanatambuliwa na mamlaka ya usalama na afya mahala pa kazi (OSHA) lakini mfuko wa WCF huwakataa na kusema magonjwa yao hayatokani na kazi, ni wengi wametelekezwa na mfuko huu.fanyeni uchunguzi

WCF wasema wanatibu kwa miaka miwili, cha ajabu wengine hawafikishi miaka tajwa kwa maana ya miezi(24) kama ilivyokusudiwa kisheria, huingizwa kufanyiwa tathimni ambayo ni ndogo sana kulinganisha na kile ambacho waathirika walikua wakipata toka kwa mwajiri baada ya kukaa nae mezani kabla ya huu mfuko

Mfanyakazi alipokuwa anaumwa na imethibitishwa na OSHA, hakuachishwa kazi bima yake na ya familia yake hazikupokwa na mwajili na zilitibu magonjwa karibu yote katika familia na mashahara alipatiwa.

WCF,wanapokea mtu mgonjwa au mlemavu alieachishwa kazi , Bima yao wanachotibu ugonjwa tajwa tu ,haihusiki ukipata malaria, kuhala tumbo na kadhalika, wakati kwa mwajili haikuwa hivyo. Bima yake ilikubeba wewe na familia kwa ujumla.

Sasa mateso ni pale mwajili kakupeleka WCF huna ajira ya kuingiza kipato kwa mwezi ni mgonjwa familia inakutegemea, Bima ya WCF wewe pekee ndio inakuhudumia na ni ugonjwa tajwa tu, wakati unatibiwa familia inaishije kimatibabu na kilishe(sick period)?

Naiomba serikali kupitia upya kanuuni na vikokotoo vya mfuko huu uwe faraja kwa wahanga na si chanzo cha mapato ya serikali.

Wengi wamehuzunishwa sana na mfuko huu na wanajuta kwa sasa kuanzishwa kwake ispokua sauti zao haziwezi wafikia nyinyi viongozi wakuu ambao ndio mna maamuzi ya nini kifanyike kuleta faraja ilikusuduwa.

Imani yangu mnapita hapa jukwaani kama sio nyie basi wasaidizi wenu watawafahamisha na mtalifanyia kazi kuondoa manunguniko ya wahanga watokanao na athari za kazi walizozifanya.
Nilifikiri unamuomba Majaliwa kwa unyenyekevu mkubwa aokoe jahazi.
 
Back
Top Bottom