Ghorofa refu Tanzania litakuwa hili la TRA DSM, nembo ya jiji

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,305
24,200
Msanifu wa majengo Arch. Yassin Mringo kutoka kampuni ya Y&P Architect aeleza kwa undani kuhusu jengo tarajiwa.



Kampuni ya Y&P Architects (T) Ltd ni ya kitanzania na inaongozwa wa wakurugenzi wawili watanzania.

Muonekano wa jiji la Dar es Salaam unazidi kuwa wa kisasa katika ukanda huu wa Afrika ya Mashariki na barani Afrika kwa ujumla.

Uwezo wake katika wilaya ya Ilala jirani na bandari utasaidia kuwa kituo cha huduma chini ya paa moja One Stop Centre kutoa huduma kwa wateja wa ndani na nje ya nchi kutokana na Dar es Salaam kuwa eneo la kimkakati (geostrategic position) ukanda huu wa Afrika ililoona hata na wafanyabishara wa karne iliyopita chini ya Sultan wa Zanzibar, utawala wa kikoloni wa Ujerumani, utawala wa kikoloni na Waingereza na utawala wa nchi huru ya Tanzania.

Muonekano wa jiji letu Dar es Salaam City 2023

1700918556602.png
 
Fedha za uchaguzi zinaanza kuchotwa na kuwekewa mifereji kabisa.

Boss wa TRA anateuliwa na nani?!! Akiambiwa project hiyo weka 20bln plus za wadau anakataa?!! Makusanyo ya TRA kwa mwezi ni 1.5trln

FISIEMU na miradi ya wizi ngozi na damu!!
 
Huo mradi waachane nao. Ni kuchezea hela. Hayo mabilioni. Sio bora wangenunua hata mtambo wa kuzalisha umeme wa gesi asilia hata Megawatt 100 au Megawatt 200(toka Japan, Korea au Siemens),
Au wangewekeza kwenye usambazaji wa maji.
Au wangewekeza kwenye kununua kupima viwanja na kupanga miji ili watu wapate hati na kumaliza migogoro ya ardhi.
Kwanza maghorofa mengi yapo Tupu. Serikali si imehamia Dodoma?

Uwezo mdogo wa kufikiria ndio chanzo za matatizo.
 
Back
Top Bottom