Kasi ya Rais Samia Usipime, Hospitali Ghorofa Sita Yanukia Mbagala

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Imeandikwa katika gazeti la mzalendo:

Kasi ya Rais Dk. Samia Suluhu kufanya mageuzi makubwa nchini inazidi kuleta neema kwa wananchi, safari hi Serikali imekuja na mpango wa kupanua huduma za afya, ikiwemo kujenga hospitali yenye ghorofa sita.

Jiji la Dar es Salaam ikiwemo eneo la Mbagala limetajwa kuwa na wakazi wengi hivyo, kuhitaji miundombinu ya jamii ikiwemo afya, inayoendana na idadi ya watu.

Kwa mujibu zilizothibitishwa na Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel, ujenzi wa hospitali hiyo utakuwa msaada mkubwa kwa wananchi.

Akizungumza Dk. Mollel alisema upanuzi wa hospitali hiyo kwa ukubwa wa ghorofa ambao mpango wake umeanza kutekelezwa, ni miongoni mwa uwekezaii mkubwa unaofanywa na Rais Dk. Samia, katika sekta ya afya kuwapatia wananchi huduma bora za matibabu.

Dk. Mollel alisema ujenzi wa hospitali hiyo, utakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Mbagala na illi la Dar es Salaam kwa ujumla, kupata huduma za afya kwa wepesi bila kuweka foleni kubwa kama ilivyo hivi sasa.

"Ujenzi wa hospitali hiyo nI dhamira ya dhati ya Rais Dk. Samia, kuhakikisha wananchi wa Mbagala na Dar es Salaam wanapata huduma bora za afya kwa karibu bila kutembea umbali mrefu, hivyo tunaendelea kuisimamia vyema,"alisema.

Alisema uamuzi wa kujengwa kiwango cha ghorofa, unatokana na maelekezo ya Waziri wa Afya, Mwalimu, kwa sekta hiyo kuhakikisha ujenzi wowote unaofanyika unafuata ramani ya mipango miji kutokana na ardhi ndogo
 
Back
Top Bottom