Ndoto ya Dar es Salaam kuwa na jengo refu zaidi ilivyotokomea wakati wa utawala wa serikali ya Awamu ya Nne

Undava King

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
3,205
5,333
Ndoto ya jiji la Dar es salaam kuwa na jengo refu zaidi la ghorofa 40 ilivyotokomezwa na utawala wa serikali ya awamu ya nne:-

Hii ni kufuatia chapisho lililoandikwa na Martin Maranja Masese katika ukurasa wake wa mtandao wa X unaozungumzia taarifa kuhusiana na uliokuwa mpango wa ujenzi wa jengo refu zaidi Dar es salaam ambao ungekuwa ndiyo landmark ya jiji la Dar es salaam na Bwana Freeman Aikaeli Mbowe.

Nanukuu.."Architectural, Engineering consultants and master planners G+40 Bilicanas Tower on Mkwepu Street, Dar es salaam (perspective view),

Mradi huu ungelikuwa na ghorofa refu zaidi Dar es salaam, mali ya Freeman Aikaeli Mbowe, walikataliwa na serikali ya Jakaya Mrisho Kikwete...hoja ilikuwa ni "mpinzani atajengaje the landmark of Dar es salaam!?"
Mwisho wa kunukuu.

Kama ni kweli hili lilifanyika kwa kigezo cha mambo ya kisiasa basi serikali iliwakosea sana watanzania ambao wanatamani maendeleo ya nchi yao na wangependa kuona wawekezaji wazawa wakipewa nafasi zaidi.

Hili jengo si kuwa tu lingeipendezesha Dar es salaam lakini pia lingezalisha ajira nyingi kwa watanzania, kuliko ilivyo hivi sasa baada ya kuibomoa iliyokuwa club ya Bilicanas (chanzo kingine kisicho rasmi pia kinadai ni sakata la kikodi kati ya wamiliki wa Billz na NHC ambalo liliamuliwa kimahakama)

Eneo hili lenye thamani kubwa katikati ya jiji hivi sasa linatumika kama parking ya magari yanayolipia sh.1000/= na hivyo kupoteza mapato na ajira nyingi ambazo zingeweza kutengenezwa na Bilicanas Tower endapo ingeruhusiwa iweze ku-exist.

Ombi langu kwa mwekezaji na Serikali kama kweli ilikuwepo azima hii nzuri kwa maendeleo ya Dar es salaam na Tanzania kiujumla warudi mezani na Serikali ya Mama Samia Suluhu naamini ni sikivu na inapenda wawekezaji.

Wayaweke sawa hili mwekezaji huyu aruhusiwe kuianza upya project yake maana mwisho wa siku watanzania tunachotaka kuona sisi ni maendeleo na ajira kwa watu wetu na siyo vinginevyo.

Maana hatuna haja ya kugombania fito wakati sote twajenga nyumba moja, tunatambua kuwa project zina maandalizi na gharama zake pamoja na muda wa utekelezaji ukishapita huwa umepita, pengine mwekezaji nae alishakata tamaa akaamua kuendelea na mengine,

lakini endapo Mbowe atakuwa na dhamira ya dhati ya kurejesha plan yake mezani na akaamua kuanza upya nafikiri hakuna mtanzania atakayepinga ujenzi wa jengo la namna hii katikati ya jiji letu pendwa la mzizima na itakuwa furaha kwetu kama wazalendo kuwa na mzawa mwenye kutuheshimisha kwa uwekezaji mkubwa wa namna hii ndani ya Tanzania.

IMG_20231117_200718.jpg
IMG_20231117_200731.jpg
IMG_20231117_200724.jpg
IMG_20231117_200727.jpg
 
Kiwanja cha Serikali hicho mkuu, unawaza kuweka jengo kabla ya mwenye ardhi hajaamua? Ninachojua ujenzi kwenye Viwanja vya serikalihufanyika kwa misingi ya sera ya Ubia yaani Joint Venture. Kwa kipindi ulichotaja sera ya ubia ilibinishwa na CAG kwamba ina kasoro za Kisheria. Hivyo ilikuwa jikoni ikipikwa.
Leo 2023 sera ya Ubia imekamilika Nchi imefunguka ni wakati sahihi hilo jengo lianze hakuna kipingamizi.
Hilo la GSM kutwaa hilo eneo na kugeuza Parking haiingii akilini. Huyu GSM amegeuka Mungu mtu sana kutwaa mali za Umma. Time will tell
 
Kibiashara hailipi jiji la Dar kuwa na jengo la ghorofa 40. Kuanzia floor ya 16 uko unakosa wapangaji mapema kabisa, floor ya kwanza inaweza kuwa kodi mara 7 zaidi ya floor ya juu.
Pia miundombinu ya Tanzania hairuhusu majengo marefu hivyo. Ni biashara kichaa
Sasa mkuu hapo shida ni nini maana watanzania tuna hujuaji mwingi ambao huwa hauna manufaa yeyote, ebu fikiria kuna mtu ana courage ya kufanya jambo kubwa kama hili ambalo wewe na mimi tumeshindwa, then uko hapa mstari wa mbele kupinga hiyo biashara hailipi kana kwamba hizo pesa za mradi unatoa wewe.
 
Yaani mtu akae ghorofa ya 40 awe anazoom kabisa mpaka kwenye mjengo mweupe
Asubiri kwanza ikulu ihamie dodoma mazima
Sasa ikulu (nyumba ya mtu ya kuishi) ina nini cha maana aisee ambacho kikwamishe maendeleo? Nani ana shida na Rais wa nchi maskini kama Tanzania mpaka hamvamie?

Dunia ya leo imeendelea mno kisayansi kiasi kwamba mtu akiwa na lengo baya ashindwi kutumia njia zingine kufanikisha malengo yake si lazima apande juu ya majengo marefu, hayo ni maisha ya kwenye muvi za miaka ya 90s.
 
Kiwanja cha Serikali hicho mkuu, unawaza kuweka jengo kabla ya mwenye ardhi hajaamua? Ninachojua ujenzi kwenye Viwanja vya serikalihufanyika kwa misingi ya sera ya Ubia yaani Joint Venture. Kwa kipindi ulichotaja sera ya ubia ilibinishwa na CAG kwamba ina kasoro za Kisheria. Hivyo ilikuwa jikoni ikipikwa.
Leo 2023 sera ya Ubia imekamilika Nchi imefunguka ni wakati sahihi hilo jengo lianze hakuna kipingamizi.
Hilo la GSM kutwaa hilo eneo na kugeuza Parking haiingii akilini. Huyu GSM amegeuka Mungu mtu sana kutwaa mali za Umma. Time will tell
Tatizo ni lile lile katika taifa letu URASIMU yaani kila linapokuja jambo la maana halitekelezeki au linakwamishwa kimakusudi kwa faida ya wachache.
 
Sasa ikulu (nyumba ya mtu ya kuishi) ina nini cha maana aisee ambacho kikwamishe maendeleo? Nani ana shida na Rais wa nchi maskini kama Tanzania mpaka hamvamie?

Dunia ya leo imeendelea mno kisayansi kiasi kwamba mtu akiwa na lengo baya ashindwi kutumia njia zingine kufanikisha malengo yake si lazima apande juu ya majengo marefu, hayo ni maisha ya kwenye muvi za miaka ya 90s.
Ni mawazo tu
Alafu mtu anaweza kukaa juu akawa anachungulia tu sio hata kwa lengo baya
 
Ni mawazo tu
Alafu mtu anaweza kukaa juu akawa anachungulia tu sio hata kwa lengo baya
Ikulu ile ilijengwa pa-baya tokea mwanzo, kwa kuwa ilikuwa plan ya mkoloni ambayo haikuwa na focus kuhusiana na mabadiliko yajayo ya mji katika siku za usoni, hivyo kama ni suala la kuepuka kuzungukwa na majengo marefu hawana budi wao ndiyo waupishe mji, kwa maana hata zile TPA, NSSF, Utumishi na towers nyingine bado ni hatarishi kiusalama kwa muktadha huo.
 
Sasa mkuu hapo shida ni nini maana watanzania tuna hujuaji mwingi ambao huwa hauna manufaa yeyote, ebu fikiria kuna mtu ana courage ya kufanya jambo kubwa kama hili ambalo wewe na mimi tumeshindwa, then uko hapa mstari wa mbele kupinga hiyo biashara hailipi kana kwamba hizo pesa za mradi unatoa wewe.
Watanzania wapo wengi wenye uwezo wa kuwekeza nyumbani. Serikali ndio inaendekeza mazingira mabovu. Kama kuna mtu alijenga Ngurdoto, mpaka marais wa Marekani walikuja wakalala pale. Kuna wazungu waliamini ile hoteli ni ya muisraeli kumbe ni ya mtanzania. Aisee serikali inabidi iiipigie chapuo sekta binafsi. Ikiwezekana wasilipe kodi wapewe tu kigezo cha kutoa idadi fulani ya ajira na ziwe na pensheni na bima ya afya. Nchi kama nchi tutafika mbali sana.
 
Back
Top Bottom