Nachelea kuwa miongoni mwa watu wa ajabu kuweka msimamo kwamba Bernard Membe sio mwizi/fisadi kwavile simfahamu Membe vizuri kama ninavyojifahamu mwenyewe.Vilevile, nachelea kuwa miongoni mwa watu wa ajabu ku-conclude kwamba Membe ni mwizi/fisadi; kwa ku-base kwenye ujenzi wa hiyo hotel peke yake. Awali ya yote, nina-assume kwamba hilo jengo kweli ni hoteli ya Mheshimiwa Bernard Membe.Kwanini nachelea ku-conclude kwamba Membe ni mwizi kwa kuangalia tu hilo jengo?! Awali ya yote, jengo hilo si la kutisha sana kwa kuzingatia muda aliokuwapo Membe kwenye system. Bernard Membe amekuwepo kwenye system tangu alipomaliza tu masomo ya sekondari.....narudia, amekuwepo kwenye system hata kabla hajagusa chuo kikuu! Inasemekana kwamba, Membe alisoma shule ya Seminary, bila shaka ilikuwa ni one step forward kuwa mtumishi wa mungu. Aidha, inasemekana kwamba, siku ambayo alitakiwa kuapa ili aingie rasmi kwenye masomo ya utumishi wa mungu, Bernard Membe aligoma kufanya hivyo. Bila shaka alijiona hakuwa na wito wa kuwa mtumishi. Hakutaka kuwa mnafiki kama wengine wanaoingia huko na kufanya mambo yaliyo kinyume kama vile kuwa na vimada wakati ni jambo lisilokubalika kwa upande wa dini yoyote achilia mbali Ukatoliki ambao hahuruhusu hata kuona.Aidha, inasemekana kwamba siku hiyo ya kiapo hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerer nae alikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa! Hivyo basi, baada ya Membe kugoma kuingia kwenye utumishi, Mwalimu Nyerere akakata shauri la kumchukua dogo (Membe)!! Hivyo basi, tangu hapo Membe akaingia kwenye system.Hata alipoingia UDSM, tayari Membe alikuwa ndani ya CCM! Ikumbukwe kwamba, hayo ya kuingia kwenye system ilikuwa miaka ya katikati ya 70, which means ni more than 30 years now.Baada ya kuchukua shahada ya International Relation pale UDSM (i think miaka ya mwisho ya 70, au mwanzoni kabisa ya 80) Membe akazidi kupaa zaidi. Na miaka ya mwanzo ya 80 akapelekwa ubalozi wa Canada ambako nako alikaa muda usiopungua miaka 5. Aliporudi toka Canada, mwaka 2000 akagombea ubunge wa Mtama na tangu wakati huo hadi leo amekuwa mbunge na waziri (Uwaziri since 2005)!! So, kwa kuangalia mlolongo huo, wala sichelei kutamka wazi kwamba uwezo wa kujenga jengo kama hilo anao hata kama ni kwa mkopo!