Ghorofa la Bernald Membe - Wizi Mtupu

mbona nyumba ya kawaida tu hiyo? Kwa miaka aliyofanya kazi nilikuwa nategemea liwe ni gorofa kweli na siyo hako kagorofa hapo.

Kumbukeni siku hizi kuna access ya loans na other financing facilities.


fikiria kwa kutumia kichwa, hivi wewe unacho hata hicho kighorofa unachokisema? Kama ndo alichagua design hiyo huwezi ku underrate. Kama ndo mikopo basi kila mtanzania angejenga vighorofa.
 
HV mkuu mbona unafanya wana JF ndondocha? HV ni nani asiyejua mshahara wa mawaziri? unataka kusema ni perdiems anazopata kwenye hizo safari za nje ndo zimewezesha kujenga hili ghorofa?. Kuongozana na rais siyo hoja na hauhitaji kujua gharama ya kulijenga ndo mtu atoe comment naomba uelewe hili jumba ni kubwa na ni la kisasa na sas lipo kwenye finishing kwa kwa kiwango tunachoweza kukiita the state of art finishings.
Mkuu hayo maswali yana maana yake. Kujenga si sawa na kununua gari. Mtu anaweza kujenga taratibu kwa pesa za kudunduliza na akawa na nyumba ambayo huwezi kuamini kama ni yake. Hivi mkuu hujui kwamba perdiem ya nje serikalini inalipa sana? Pia unaweza kukuta ana mkopo wa benki akaongezea na savings zake akapata hiyo ghorofa.

Simtetei Membe na wala sina sababu ya kumtetea ila tu siyo kila kitu kinaunganishwa na ufisadi lazima tuwe tunafanya tafakur
 
kwa niaba ya mtoa mada naomba nikuhahakshie ni ghorofa lake bnafsi nilkuwa kikazi huko hadi mwezi wa 3 mwaka huu. Na nilikuwa naishi eneo hilo la shangani veta.

Hata mie naweza kusema kuwa nilikuwa kikazi huko na naomba nikufahamishe sio ghorofa lake binafsi.
Nilikuwa kikazi huko hadi mwezi wa tatu na nilikuwa naishi pia eneo la Shangani veta. Simple.
 
Sunshow inawezekana una kengeza; Pia sioni relationship yoyote kati ya cheo cha serikalini utajiri. Pia umeshasema wajasiriamali wa kawaida wanayo, je huyu bwana ni mjasiriamali au mtumishi wa serikali?
Ok tuseme mshahara wake ni mil. 15 kwa mwezi ambayo ni kawaida maana kama mbunge anapata mil. 7 ni sahihi waziri kupata twice. Per diem tuseme laki 7 ambapo anaweza pata wasitani wa siku 10 nje ya nchi hivyo kufanya apate mil. 7 extra income. Jumla kwa mwezi tuseme anapata mil. 22. Kati ya hiyo mil. 20 inaenda benki kila mwezi kumbuka gharama karibu zote anahudumiwa na serikali kuanzia nyumba, gari, n.k hivyo kwa mwaka atakuwa na mil. 240 benki. Jumlisha idadi ya miaka aliyokaa mambo ya nje more than 5 years sawa na zaidi ya bil. 1.2 na kumbuka pia kwa position yake anao uwezo wa kukopa benki kama wafanyakazi wengine serikalini. Kwa haraka hilo jengo linaweza kuwa na thamani ya bil. 1.
 
Watanzania kazi tunayo! Viongozi wetu wote sasa wafanyabiashara! mitaji hii wanapata wapi? mimi sijui!
 
Ok tuseme mshahara wake ni mil. 15 kwa mwezi ambayo ni kawaida maana kama mbunge anapata mil. 7 ni sahihi waziri kupata twice. Per diem tuseme laki 7 ambapo anaweza pata wasitani wa siku 10 nje ya nchi hivyo kufanya apate mil. 7 extra income. Jumla kwa mwezi tuseme anapata mil. 22. Kati ya hiyo mil. 20 inaenda benki kila mwezi kumbuka gharama karibu zote anahudumiwa na serikali kuanzia nyumba, gari, n.k hivyo kwa mwaka atakuwa na mil. 240 benki. Jumlisha idadi ya miaka aliyokaa mambo ya nje more than 5 years sawa na zaidi ya bil. 1.2 na kumbuka pia kwa position yake anao uwezo wa kukopa benki kama wafanyakazi wengine serikalini. Kwa haraka hilo jengo linaweza kuwa na thamani ya bil. 1.


Kote huku umekwenda mbali sana. Maana mchanganuo huo ukizingatia kuwa ana jimbo, ndugu na watoto wa kuwasaidia na kugharamia zinaweza zisijenge hoteli Mtwara. Mvumbuzi atuletee nyaraka kama tulivyowekewa ya Maige na Ngeleja.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Mfumo wa wafanyakazi Serikalini kutokuwa na biashara ulikufa zamani sana. Nyie bora mngezaliwa wakati wa Nyerere. Kwa sasa wala haina mshiko.

Nachokupendea unabisha kila kitu kuhusu ccm/wanaccm hata kama tuhuma zinaushaidi.!
 
:A S 12::A S cry::A S cry:Hata ombaomba kma matonya huwa anakwenda kwa waganga wa kienyeji kutafuta dawa ya kupata zali la kupewa hela na wasamalia,yaani hata kma unamoyo mgum na uso wa mbuzi utampa tu.
 
hata ombaomba huwa anakwenda kwa mganga wa kienyeji kutafuta dawa ya kuvutia anaowaomba hela,hata kama unaroho ngumu na uso wa mbuzi utampa tu pesa:happy::A S 12::evil:
 
Mbona nyumba ya kawaida tu hiyo? Kwa miaka aliyofanya kazi nilikuwa nategemea liwe ni gorofa kweli na siyo hako kagorofa hapo.

Kumbukeni siku hizi kuna access ya loans na other financing facilities.

View attachment 54632

Asante sana Rejao,
Kazi unayoifanya inaanza kuzaa matunda,
Siku hizi hata ukitype CCM kwenye computer
Ni bendera ya Chadema ndiyo inatokeza.
Asante na endelea hivyo hivyo Mkuu......!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Rejao,
Hivi katika hali ya makundi kundi mliyonayo ndani ya chama cheni wewe upo kundi gani kati ya makundi matatu makubwa (Yaani Kundi la Membe, Lowassa na Sitta)?

TUMBIRI wa JF,
tumbiri@jamiiforums.com
Ungeniambia kwanza upo kwenye kundi gani kati ya kundi la Slaa, Mbowe, Zitto au Shibuda!
 
Last edited by a moderator:
huyu membe hiyo ni hotel yake kweli. Na ana nyingine iko karibu na standa ya mabasi mtwara inaitwa naf blueview
pia pale lindi anataka kumpora mzee mmoja ile lindi oceanic hotel ambayo mzee huyo alinunua kwenye mnada kihalali uliofanywa kwa niaba ya crdb.

Naogopa hata kumuita mheshimiwa maana matendo yake huku kusini wala hayafanani na cheo chake. Nasubiri m4c waje kusini niwauzie hili gazeti

lowassa at work
 
View attachment 54632

Asante sana Rejao,
Kazi unayoifanya inaanza kuzaa matunda,
Siku hizi hata ukitype CCM kwenye computer
Ni bendera ya Chadema ndiyo inatokeza.
Asante na endelea hivyo hivyo Mkuu......!
Nitazidi kuongea ukweli daima. Hata mjaribu kufanya nini. Lazima CDM mkubali kuwa chama chenu hakiwezi kuleta madiliko yoyote. Mabadiliko yatafanywa na sisi wenyewe na siyo chama kituletee.
 
Last edited by a moderator:
afu watu kwa akili zao watachagua tena CCM baada ya kuhongwa bia na kanga
watanzania tusipoitoa CCM madarakani tutabaki maskini daima
upuuuzi kama huu ulaya hakuna waziri au mbunge lazima aeleze kapata wapi fedha za kufanya miradi
kwa wenzetu wameweza kwa kuwa wanajali zaidi utaifa na sio kujilimbikizia kama hivi
hata maskini analala nyumba nzuri na kutibiwa lkn bongo afya,elimu sios bure
kisa hawa wachache wanauza rasilimali zetu ili kujilimbikizia kama hivi
THE DEATH OF CCM, THE BEGINNING OF NEW NATION.
 
WE NI WA KUKATWA KICHWA KABISA
mabadiliko gani mtaleta baada ya kutawala miaka 50?
hata mtoto wa darasa la kwanza anajua hapo unaongea ujinga mtupu
labda sera hizo ataambiwa ndondocha na sio mtu mwenye akili timamu
ipo siku mtajuta na sijui mtakimbilia wapi

Nitazidi kuongea ukweli daima. Hata mjaribu kufanya nini. Lazima CDM mkubali kuwa chama chenu hakiwezi kuleta madiliko yoyote. Mabadiliko yatafanywa na sisi wenyewe na siyo chama kituletee.
 
mbona ni nyumba ya kawaida sana hii! asipo jenga waziri ungependa ajenge nani ndio muamihi hajachakachua?mtu ni waziri zaidi ya miaka kumi ashindwe kujenga nyumba kama hii? acheni utani na kuchafuana kusiko na maana.
 
Ndugu yangu apo bado,kuna ki2 kingine amakishusha SONGEA,Wilayani Mbinga kuna sehemu inaitwa Mbambabay,yan pembeni ya ziwa Nyasa kuna hotel uko japo c famous sana bt ni yake uyu jamaa.Na nyumba nyingine ipo juu ya Mlima kama waelekea Liuli uko uko Mwambao wa Ziwa nyasa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom