Gharama za bando zitaua creativity, biashara na ndoto nyingi za vijana

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,499
86,037
Nawasalimu wote. Nitaangazia nyanja kadhaa na nitakapoweza tena mifano. Pale patakapopungua naomba mjazie.

Hivi karibuni makampuni ya mawasiliano yaliongeza karibia kwa 50% gharama za Internet kwa Watumiaji kwenye ile option waliojificha humo kama "Offer" ya mtandao! GB tatu kwa mfano kwa Vodacom Tanzania ilikua ni Tzs 3,000 kwa siku saba, japo kila MTU "nasikia" ana package yake, Leo hii 3000 unapata 1.5GB, mnaweza kuweka mitandao mingine katika hili.

Sera ya Mlaji kwenye Mawasiliano (Communication Consumer Policy) inamtaka mtoa huduma kutoa taarifa kwa Mlaji juu ya mabadiliko yoyote kwenye huduma husika, kwa bahati mbaya pengine hili halikufanyika safari hii, maana safari ya kwanza lilipofanyika watu wakapiga kelele zikafutwa. This time wakaamua kupunguza kimya kimya, pengine wanajua hatusomi na hata tukisoma hatuna cha kufanya na huenda kina baraka kutoka kwa Wakubwa.

Tanzania haiishi kwenye kisiwa, Tanzania ni nchi kama nchi nyingine Leo hii kuongeza gharama kiasi kikibwa hivi tutarajie yafuatayo.

Moja, Vipaji vingi vya Vijana kufa, ubunifu kuishia hapo hapo. Nilifikiri Wizara husika ingesaidia kuwaongoza Vijana kwenye Ulimwengu wa Sayansi na Technology ambapo kuna ajira nyingi ila tumedhamiria kuwauwa kabisa.

Mfano, Apps developers ambao wengi ni Vijana wa 18yrs + hawataweza kuendelea na ubunifu wao kwakua bando ni ghali sana. Hivi hata Wizara inajua kuwa Tanzania kuna App inaitwa THL ambayo inawaingizia Watanzia zaidi ya BILLION MOJA hadi sasa??

Tukiwa na Vijana wengine wengi wa kuunda Apps kwa ajili ya Ticketing, Health, Sokoni App, Weather, Websites za masomo, ONLINE libraries HUONI tutakua na Vijana wenye kujitegemea na kujiongezea kipato?? Huyu shetani ametoka wapi anayetaka kuuwa ndoto na creativity ya vijana wetu??

Pili, Kuna Vijana wengi sana was Kitanzania na Ulimwenguni ambao wanafanya kazi ONLINE kama Freelancers, maisha yao wanategemea "bando" na wanalipwa vizuri, kuna vijana wanalipwa mamilion kwa assignment moja, kwanini tusipunguze gharama za Internet ili kuwavutia Vijana wengi zaidi kijiajiri kama Freelancers? Pesa watakazopata watakula, watakunywa, watajenga, na kwa njia hio serikali itaongeza mapato na kuongeza mzunguko was fedha. Huyu Shetani ametoka wapi anayeongeza gharama za Bando ili Vijana wetu washindwe kumudu wakacheze kamari?

Tatu, Leo hii ninapoandika hapa muda huu 20th October 2021 thamani ya Bitcoin moja ni zaidi ya 150,000,0000 yaani 1BTC=150,000,000Tzs. Tukiongeza gharama za Bando Vijana wetu watashindwa ku-trade ONLINE. Imagine kama kijana angeweza kununua BTC October mwaka Jana 25,000,000 Leo hii pesa yake ingekua kiasi gani?? Kwanini Tanzania hatutaki kuwasaidia Vijana wetu??

Tuangalie Interest ya Vijana then tutumie interest hizo kuwafanya wawe Independent Financially, kama wanapenda kutumia Smart phones sana ndio tuangalie fursa kama hizo tuwaonyeshe kuwa wakati unachati unaweza kujiingizia kipato.

Binafsi, Mimi Elli nimehudhuria mikutano mingi sana ya ONLINE (Webinars) za Wetu/Vyuo mbali mbali, kuna maarifa mengi, kuna training nyingi ambazo Vijana wetu wakiwa exposed watajifunza na huenda wakajenga network nzuri na kufahamu yanayotokea ulimwenguni ila tukiongeza gharama za net tunajifungia milango.

Kwa mfano, ukiingia mtandao wa LinkedIn kuna training nyingi sana na opportunities nyingi sana ambazo Vijana wetu wangeweza kujiingiza huko, lakini utawezaje kuwa ONLINE uhudhurie semina wakati una bando la mawazo??

Kwenye hii Event kwa mfano; EVENT SCHEDULE: Future Of EdTech IV - Online Pitch Night (Today 1900-2100 CET) Mtanzania kijana sana alitoa presentation yake nzuri sana, na ukumbuke ni Ulimwengu mzima unafuatilia kwahio naamini hadi sasa atakua amepata Potential Partners.

Leo hii tukiwanyima bando, tunataka tujenge taifa la Wavuta bangi, Wadangaji wa kike na kiume, Wapiga nanihii, etc. Huyu shetani aliyeruhusu mitandao ya simu kuongeza gharama alaaniwe yeye na kizazi chake chote.

Kuna Website nyingine nyingi sana sana akina DEVEX ambao wanatoa kila fursa na Webnars za maana, kwanini tunawanyonga Vijana wetu kwa ulafi wetu?

Leo hii mlipunguza kodi ya smartphone halafu mkaongeza gharama za bundle, mnadhani smart phone inakuja na bundle yake? Kwanini tusijifunze hata kwa majirani zetu? Leo hii tunasema kila kijjiji kina umeme ila bando juu! Sasa umeme una faida gani?

Walimu wa shule za msingi wana mfumo wa kutuma taarifa Wilayani, hawa nao wanatumia bando, tunataka shule zitumie COMPUTERS kwenye kufundishia huku bando ziko juu, unadhani ataweza kuingia online na kufanya conference call kwa kutumia tu charge na sio bando?

Materials nyingi sana sana ziko kwenye ONLINE LIBRARIES utadhani huyu mwanachuo atamtegemea Dr au Profesa wake aje kufundisha na kuishia hapo tu? Bytheway madokta wenyewe na maprofesa ndio hao wanaosema wameokotwa kwenye majalalaa??

Nasisitiza sana, GHARAMA ZA INTERNET ZISHUSHWE SANA tuache ujinga wa kusema eti Tanzania ndio nchi ambayo gharama za bando ziko chini, so what? Kama ziko chini tunashindwaje kufanya bure kabisa??

Leo hii Vijana ambao ni YouTubers wanapata pesa kwa matangazo, bado tunaona sio fursa? Wallah tumerogwa! Hawa Vijana wamewakosea nini?

Aliyekuja na wazo mfu namna hii yampasa kufungiwa jiwe shingoni kisha akazamishwe baharini.

Alamsiki
 
TCRA wapo wapo tu, kazi yao kubwa ni kuimplement vifaa vya kutrack na kurecord watu, malamiko ya wateja hawasikilizi kabisa, how come unaamka asubuhi unakuta bando limeshushwa (Kupunguzwa MB) nusu nzima bila notification yeyote.

Hivi mnadhani mkifanya hivyo ndio mtazuia watu wasicomment maovu ya serikali? Hivi unadhani mtu ambaye anayefichua maovu ya serikali atashindwa kuweka bando? Mtawapoteza vijana/wajasiliamali wa insta/facebook/whatsapp ila Makonki wa kuwatemesha ndoano serikali hata mkiweka 1GB kwa elfu 50 watanunua tu.

Mmeongeza tozo kwenye X-pesa lakini bado tu hamjaridhika mmekuja tena kwenye mabando! Upuuzi mtupu.
 
Airtel walikuwa na Night pack ya GB 10 wakaifuta, Usiku wa leo Halotel nao waliokuwa wamebakia na Night pack ya GB 5 wameifuta zamani walikuwa na unlimited ikafutwa baada ya kampuni yao kupigwa fines nyingi mno za mabililioni ya shilingi.We are doomed....
 
Siamini hadi sasa hivi shuguli zangu ni mtandao tu na muda mwingi nacheki na tutorials hivi yote hii ni kwa ajili ya watu kutembelea ma v 8 jamani?
 
Airtel walikuwa na Night pack ya GB 10 wakaifuta, Usiku wa leo Halotel nao waliokuwa wamebakia na Night pack ya GB 5 wameifuta zamani walikuwa na unlimited ikafutwa baada ya kampuni yao kupigwa fines nyingi mno za mabililioni ya shilingi.We are doomed....
5gb ya halotel haipo tena kwa sasa night pack kwa 1500 ni mb 1160,kwa sh 500 ilikuwa gb 1 kwa sasa ni mb 350
 
World Happiness rankings tupo 139 kati ya 146.

Screenshot_2021-10-20-06-35-43.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulimwengu wa sasa internet ni muundo mbinu. Internet ni kama reli, umeme, barabara, hospitali, shule nk. Ni huduma muhimu kwa maendeleo. Lakini si Africa/Tanzania.

Kilichopo ni kuwa mtu wa kipato cha chini atashindwa kabisa kuaccess internet. Kitu ambacho hakina tofauti na kukosa umeme, barabara nk.
 
Yap, internet inabidi iwe moja ya haki ya kimsingi ya kila Mtanzania.

Jukumu la serikali lingekuwa kuwawezesha wengi kupata access. Wenyewe wanafanya kinyume chake.

Huduma nyingi za serikali sasa na huko mbeleni zitakuwa mitandaoni. Mitandao inaongeza tija na kupunguza gharama kwa serikali na Wananchi.
 
Yap, internet inabidi iwe moja ya haki ya kimsingi ya kila Mtanzania.

Jukumu la serikali lingekuwa kuwawezesha wengi kupata access. Wenyewe wanafanya kinyume chake.

Huduma nyingi za serikali sasa na huko mbeleni zitakuwa mitandaoni. Mitandao inaongeza tija na kupunguza gharama kwa serikali na Wananchi.
Uwakute sasa wako kwenye kuandaa miswada, utadhani watu
 
TCRA wapo wapo tu, kazi yao kubwa ni kuimplement vifaa vya kutrack na kurecord watu, malamiko ya wateja hawasikilizi kabisa, how come unaamka asubuhi unakuta bando limeshushwa (Kupunguzwa MB) nusu nzima bila notification yeyote.

Hivi mnadhani mkifanya hivyo ndio mtazuia watu wasicomment maovu ya serikali? Hivi unadhani mtu ambaye anayefichua maovu ya serikali atashindwa kuweka bando? Mtawapoteza vijana/wajasiliamali wa insta/facebook/whatsapp ila Makonki wa kuwatemesha ndoano serikali hata mkiweka 1GB kwa elfu 50 watanunua tu.

Mmeongeza tozo kwenye X-pesa lakini bado tu hamjaridhika mmekuja tena kwenye mabando! Upuuzi mtupu.
Kwa hiyo wakipandisha bando ndo watu watashindwa kushusha spana, wamebugi aisee......
 
Bila kutumia haki yetu ya kikatiba na kuwapa wengine nao nchi hii tuwapime kama watakuwa na uchungu na sisi basi vilio hivi na vyengine vitakuwepo na kuendelea kuwepo mpaka mwisho wa dunia . Watu wenyewe hatueleweki tumeridhika acha watupandishie Hadi tununue mb 5 kwa buku
 
Back
Top Bottom