Nawashauri vijana wenzangu Udalali ndiyo msingi wa kipato kwa dunia ya leo, hususani Tanzania

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
2,552
2,992
Assalam Alaykum!

Wadau wa JF kila siku kumekuwepo na kawaida ya kuunda nyuzi tofauti za watu kuomba ushauri wa kujikwamua kimaisha lakini wengi wa wachangiaji hawaoneshi nia na azma ya kusaidia,waomba ushauri wengi huangukia patupu leo mimi @Muhafidhina nimeamua kutoa ushauri kwa vijana wenzangu kujiunga katika biashara ya udalali kwa sababu zifuatazo;

Mosi,Udalali ni kazi ambayo haitaji muda mwingi katika utafutaji zaidi ya kuwekeza muda wako zaidi kwenye mitandao ya kijamii, na kwa bahati nzuri kizazi cha sasa kinaendeshwa na teknolojia vijana wengi hawajaachwa nyuma kwenye kumiliki simu na bando hivyo kuna rahisisha kuepuka mizunguko ya kufatilia bidhaa(nyumba,simu,nguo n.k).

Pili,Upatikanaji wa bidhaa,hatuwezi wote kuajiriwa ila tunaweza kujiajiri kupitia bidhaa za watu au kampuni kwa bahati nzuri bidhaa nyingi kwa sasa zinapatikana hapa hapa nchini hivyo unaweza kutafuta mzalisha na soko kwa wakati mmoja bila kutoa gharama Note; Dalali hanunui ila ni middle party kwa maana siyo mwenye hasara.

Mwisho, wengi wa dalali wamebase kwenye majumba, vyumba na vifaa hivyo unaweza kuamua upande upi unakufaa zaidi.
 
Problems

Kusalitiana

Kuuana

Kulogana

Pia kuwa na Sonona.. mara nyingi wanauza au kudalalia vitu sivyo (Vya dhulma au vibovu) mwisho nafsi inawasuta sana...

Kazi ya kipuuzi sana.
duniani upo kuishi siyo kusindikiza watu piga pesa uishii we unaongelea nafsi ipi
 
Ila madalali nyinyi ni wasenge Sana

Kuna Mzee alikuwa anauza nyumba million 100 akatafuta madali , na madalali wakaja kuuza kwa milion 250

Yule Mzee alivyokuja kusikia alisikitika sana
 
Tanzania kuna fursa sana ya kutengeneza fedha ukiwa dalali smart. Jua bidhaa ipo wapi, jua mnunuzi yupo wapi. Usiendekeze tamaa.

Tatizo la madalali wako kama mbuzi. Utasikia "Tupo wa3, tupo wa4. Na hapo bei ya bidhaa wameiongeza mara mbili, wanarudi tena kwa mwenye bidhaa na hadithi za tuna mteja bei sema mara mbili na usipunguze. Matokeo yake mteja hata akinunua akija kujua mlimpiga harudi wala kutoa recommendation.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom