Ghala la silaha Gongo la Mboto lalipuka!

Ghala la silaha Gongo la Mboto lalipuka!

Yametokea katika kipindi cha wiki moja tu
- Pinda anapindisha sheria kwa kulidanganya bunge na wananchi bungeni
- Msafara wa mke wa kikwete unapata ajali na dereva wake anakufa ajalini
- Spika Makinda anafunika uwongo wa pinda kwa kutomruhusu Mheshimiwa Lema kutoa ushahidi
- Leo tunaona mabomu yanalipuka Gongolamboto kitu ambacho kilishatokea kabla ndani ya miaka miwili huko mbagala.
Tuendelee kuingia kanisani kusali Mungu atunusuru
 
Asante sna ubarikiwee

Ila ukinitajia mtu yoyote yupo connected na ccm nachukiaa:thinking::thinking:
 
Mungu wangu!Alale mahali pema peponi!Waliobaki nawaombea wapone!So sad!
 
Kova jicho lake la kushoto ndo lilivyo kila siku?
 
Poleni sana wakazi woote wa Dar es Salaam mliopata madhara,mishtuko ya namna moja au nyingine!!!... sisi tuliopo mikoani tunawaombea sana...
 
Inasikitisha kuona wachangiaji wengi kwenye hii forum wakichukulia ajali iliyotokea Gongo la Mboto kisiasa.

Pamekuwa na wachangiaji wanaothubutu hata kuhusisha chama cha siasa au ufisadi na milipuko hiyo.

Si ustaarbatu kukurupuka na kutoa majumuisho yasiyo na mantiki. Kulilaumu jeshi au serikali kabla ya kujua chanzo cha milipuko hiyo ni kukosa busara. Wengine wanajidai wanajua hata umri wa mabomu yale, yalivyohifadhiwa na mambo mengine ya taaluma za kijeshi ambazo si kila mtu anazijua.

Tuwe na subira. Kama itagundulika kuwa ni ajali, ieleweke kuwa ajali ni ajali, hata kama ilitokea Mbagala yaweza kutokea pengine pia, hizo ndo ajali.

Mtaalam mmoja wa milipuko amenieleza kuwa mlipuko kama ule unaweza kusababishwa na mambo mbali mbali. Inawezekana ikawa kweli ni umri wa mabomu, au shoti ya umeme au uzembe wa mtu mmoja au hujuma kutoka kwa watu wabaya kama baadhi ya wanachama wa chama cha siasa wanaotaka Tanzania isitawalike.

Tuache kupotosha mambo, tusubiri wataalam wafanye kazi yao na umma utataarifiwa tatizo lilikuwa nini.

Mkuu hii ni JF, kwa taarifa yako tu kama wewe ni propagandist wa CCM ni kwamba JF ni watanzania na Tanzania ina raia na wanajeshi. Ni kwamba wanajeshi wamo humu na ndiyo wanaohifadhi mabomu hayo. Ila cha kusikitisha zaidi ni kitendo cha kuyalundika mabomu yaliyokaa muda mrefu yakisubiri kuharibiwa karibu na makazi ya watu. Ni nani asiyejua kuwa hela za kuharibu mabomu hayo zilikuwa diverted kwenye kampeni za CCM 2010?. Sasa kwa nini CCM na serikali yake visihusishwe na kutokujali usalama wa raia bali wao wanaangalia usalama wao wa kuwa madarakani?
 
Yanayotokea ndani ya wiki moja
- Waziri Mkuu Pinda anapindisha sheria kwa kulidanganya bunge na wananchi huko Dodoma bungeni
- Spika Anna Makinda Samamba anatetea wongo wa pinda Bungeni kwa kumtetea Pinda aheshimiwe kama mkubwa hata akidanganya
- Mheshimiwa Godbless Lema ananyimwa haki bungeni ya kuanika ukweli ambao Pinda amelidanganya bunge na wananchi
- Msafara wa Mke wa Rais Kikwete unapata ajali na dereva wa Ikulu (usalama wa taifa) anafariki ajalini
- Leo ghala la silaha za vita la jeshi la Wananchi mabomu yanalipuka na kuathiri makazi ya raia kitu ambacho kilishatokea ndani ya miaka miwili huko Mbagala.
Tuendelee kuomba Mungu atunusuru
 
Intelijensia hua inafanya kazi ikiwa CDM wanahusika tu!What a shame mijitu inakalia vyeo alafu mambo kama haya yanatokea kwenye maeneo wanayoishi watu!
 
sasa tuna kila sababu ya kukutana mnazi mmoja uwanja wa mashujaa kumshinikiza mkwere aachie ngazi kwani nchi ishamshinda,tumechoshwa na ahadi za uongo kila kukicha...yani nilikuwa Amana hospital hadi saa sita na nusu maiti zilizoletwa kwenye defender la ffu ni zaidi ya tano na majeruhi hawaesabiki

Nina wasiwasi haya mabomu ni usanii wa sirikali. Ndo kama moto wa NASAKO miaka ile na wa IKULU enzi za mkapa.
Kova anasema wanachi warudi majumbani wakausubiri moto na moshi wa sumu?
Yalipuke Mbagala juzi na bado leo hatujui huwa yanalipuka.
Ndo baadaye yatakuja maelezo ya kisanii kama yale ya ikulu kuunguzwa kwa moto wa pasi? Mafisadi sijui wamekusudia nini ila siku yao ipo.
 
"Tanzania Polce force would like to inform you, there has been an accident at Millitary Camp in Ukonga. The situation is under control, be advised to stay calm-IGP"



Ni ujumbe nilioupata kwenye simu yangu nusu saa ilyopita............Polisi wanasema ni ajali, naona harakati za kujisafisha zimeanza
 
Yametokea katika kipindi cha wiki moja tu
- Pinda anapindisha sheria kwa kulidanganya bunge na wananchi bungeni
- Msafara wa mke wa kikwete unapata ajali na dereva wake anakufa ajalini
- Spika Makinda anafunika uwongo wa pinda kwa kutomruhusu Mheshimiwa Lema kutoa ushahidi
- Leo tunaona mabomu yanalipuka Gongolamboto kitu ambacho kilishatokea kabla ndani ya miaka miwili huko mbagala.
Tuendelee kuingia kanisani kusali Mungu atunusuru

Sijapata kuona uzembe wa hali ya juu kama huu kutokea Mbagala na ndani ya miaka miwili itokee tena? kwa sababu serikali haikufanya chochote kwa yaliyotokea Mbagala hapa sasa kuna mambo mengi ya kujiuliza serikali itafanya nini.

Viongozi wa serikali kama wana akili nzuri wanaweza kusoma ishara za nyakati.
 
TUJIKUMBUSHE MABOMU YA APRILI 2009 MBAGALA
8D6U0041.JPG




Picha tu inatosha kuonyesha kuwa huyu prezident sio makini.........Huwezi kuwana na furaha katika mazingira kama hayo hayo, inaonyesha kuwa jamaa ni kama alionekana kutoguswa kabisa na hilo tukio huwezi kutabasamu wakati watu wamepoteza maisha!
 
Katika pitapita yangu, nimekumbuna na hii kwenye Forum za Watanzania:

MABOMU KIKOSI CHA JESHI 511 GONGO LA MBOTO
· Mimi nimeona mwanga mkali nauona nikiwa hapa ubungo nikafikri labda kuna kituo cha mafuta kinaungua moto huko tabata kumbe ni Gongo la moto imelipuliwa???
· USIOMBE KUSIMULIWA ONA MWENYEWE KAMA VILE MUVI FULANI HIVI, jIji linarindima kwa sauti ya kutisha ya mabomu inasikika.
· Tayari redio zinatangaz na TV, KUMBE GHALA LA SILAHA LIMELIPUKA HUKO JESHINI Gongo la Mboto.
· Nimepiga simu kwa shemeji yangu, akiwa kazini, ametoka mbio kwenda nyumbani gongo lamboto, anasema hali ni mbaya sana, amekimbilia nyumbani kuangalia USALAMA WA FAMILIA, amekuta hakuna watu nyumba zote zimehamwa, watu wanakimbia ovyo ovyo, hajuin familia iko wapi, kibaya zaidi aliacha watoto na houseirl, nyumba za karibu zimesawazishwa ardhini. Anasema atanipigia baadae.
· Nilipofuatilia kwa simu baadae akawa hapatikani kwenye simu, sijui kilichompata mpaka hapo kesho nitakapo kwenda huko nitajua.
· Rafiki yangu mwingine anasema jamaa zake walikimbilia kanisa la karibu, bomu bomu limewafuata na watun saba wamekufa humo ndani na watu 40 wako mahututi.
· Kisukuru nao huko tabata bomu limetua na haijajulikana watuy wangapi wamekufa.
· Mwanga mkali na anga la jiji lilikuwa jekundu kwa mlipuko wa mabomu maeneo ya huko Vingunguti, hgongola mboto , Airport.
· Watu wangi kutoka eneo la Mombasa, banana wanakiimbia mchaka mchaka mkuelekea mjini.
· Ni kama vile ambush ya kivita maeneo hayo, mabomu yanalipuka hovyo hovyo maeneo hayo, watu wamechanganyikiwa wanakimbia ovyo hawajui waendako ili mradi tu kuliepuka eneo hilo.
· Hakuna usafiri tena wa kwenda huko Magari yote ya wakaazi wa huko tokea mjini hayaendi huko, hakufikiki usiku huu.
· Watu wamezuiwa kurudi huko, wamezuiwa kulaa kwenye viwanja vya uhuru Dar.
· Ukonga Mageraza: Boumu limedondoka karibu na gereza, wakati watu wanakimbilia uwanja wa magereza mbele yao likadondoka bomu , watu wanaelekea kichanganyi mbele yanaendelea kundoka kwenye nyuma za karibu, hapo kila mtu anaangalia wapi akafiche kichwa chake.
· Vibaka nao ndio peak ya mavuno yao.
· Majeshi yanasaidia kuzima moto mitaani, lakini pia Serikali inawaomba wanachi waondoke katika maeneo hayo kiasi cha umbali wa kiliomita 10 tokansehemu ya mlipuko wa silaha hizo.
· Majeshi yoteya polisi yameamuliwa kuelekea huko kutoa msaada kuokoa watu na mali usiku huu.
· Mabomu mengi ne yameingia kwenye nyumba za watu na bado hayajalipuka
· MAWASILANO YA SIMU NA WATU WA E NE HILO YAMEKUWA MAGUMU. SIJUI NDUGU ZANGU WATAKUWA HAI MPAKA ASUBUHI HII
· Taarifa zaidi zinaendelea...kesho.
· Ni saa saba hii usiku naomba nikalale.

Swali BINAFSI:
Tulipendekeza na kushauri serikali ya Kikwete kuwa ghala za silaha zihamishwe zitoke kwenye makazi ya watu kutokana na somo tulilolipata kule Mbagla. MABOMU YA MBAGALA!!!
Kuna organization au uongozi wowote uliofuatilia uhamishwaji wa silaha hizo??
Bado maghala ya jeshi ya Lugalo, MBWENI,Makongo/ Mwenge, nyuma ya chuo Kikuu nk
Hii ni hujuma au bahati mbaya??UZEMBE AU NI MAKUSUD??
Tukio la mwaka ule liliongelewa sana na watu walipiga sana kelele juu ya maghala ya silaha na utunzwaji wake, je tulifikia wapi??
Hili ndilo jeshi letu la karne hii la wasomi.........
Bado tutaendelea kujiua wenyekufa kabla hatujaenda vitani
Usiku mwema
 
what went wrong?viongozi wanazidi kuneemeka ktk kamati za utafiti na uchunguzi,hawafanyi bure ktk hizi tafiti so wanakula posho za kufa mtu kila kikao its about 250 laki na kuendelea,mpaka kamati iishe mtu ana mshiko wa maana.then hamna kinachotendeka kutokana na findings hizo.sasa hili la gongo la mboto lisingetokea kama findings za mbagala zingekuwepo na kufanyiwa kazi.
asante kwa kuweka hizi picha ,a picture says a thousands words.
haya Mh.Dokata raisi Jakaya kikwete its time kuwa wajibisha wahusika bila aibu kwani bila kufanya hivyo utakuwa umejiabisha mwenyewe ikizingatiwa umepiga hadi picha zako ukiwa muhimbili kuwapa pole waathirika wa mabomu ya mbagala,
TUJIKUMBUSHE MABOMU YA APRILI 2009 MBAGALA
8D6U0041.JPG

Aprili 30. 2009 Mh. Rais J.K Kikwete akiwa eneo la Mbagala jirani na kambi ya jeshi DSM akiwa na wasaidizi wake kuanzia kushoto Naibu waziri ulinzi wa Nchimbi Pili shoto, Mkuu wa JWTZ Jenerali Mwamunyange tatu kushoto na Inspekta jenerali wa Polisi Saidi Mwema.

8D6U0243.JPG

Aprili 30. 2009 Mh. Rais J.K Kikwete akiwa kitengo maalumu cha mifupa- MOI hospitali ya Taifa Muhimbili akiwafariji majeruhi wa milipuko ya mabomu ya Mbagala DSM. Watu 20 alipoteza maisha na zaidi ya 200 kujeruhiwa na mamia ya nyumba kuharibiwa.

DSC06354.JPG

Aprili 2009, Brigedia Jenerali F. Ulomi akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais Dk.Shein.

RIPOTI YA MKUU WA MKOA WA DSM KUHUSU MADHARA YA MABOMU YA 2009
Mkuu wa Mkoa wa Dar es SaLaam, Willium Lukuvi ametoa ripoti maalumu ya milipuko ya mabomu katika kambi ya jeshi Mbagala yaliyotokea na kuharibu nyumba zilizokuwepo karibu na maeneo hayo.
Ripoti hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Dar es SaLaam, Willium Lukuvi na ilifanyiwa uhakiki na kamati maalumu ambayo iliundwa kuhakiki nyumba zilizoharibika ili waweze kupatiwa fidia.
Lukuvi amesema kuwa katika ripoti hiyo nyumba ambazo ziliteketea kabisa na hakuna kitu kilichookolewa ndani zilikuwa jumla ya nyumba 235.
Nyumba 54 ziliharibika ambazo hazifai kwa matumizi ya binadamu ambazo hazikuteketea kabisa na kuanguka.
Amaesema nyumba zingine ziliathiriwa kidogo kidogo na si kuanguka chini na kufaa kwa matumzi ya binadamu.
Amesema jumla ya nyumba zote ambazo ziliathirika hata kama hazikuanguka zilikuwa jumla ya nyumba 9200.
Amesema ripoti ya awali ilionyesha jumla ya nyumba zilizoathiriwa na mabomu hayo zilikuwa nyumba 9254 ambazo si sahihi.

Amesema serikali imeshaanza mchakato wa kuwalipa fidia wananchi hao ili waweze kupata makazi.
 
Dahh kwanini kila kitu kibaya ni sisi Tanzania hivi ni ujinga au tumemkosea nn Mungu ...then hawa viongozi wanajua ht kuongea na watu wakati wa matatizo ...unaongea vitu serious unazungusha zungusha tu makalio yako kama sio askari its very shame hawajawahi ht kuona viongoz wa nchi nyengine kwenye matatizo kama haya....
 
Inasikitisha kuona wachangiaji wengi kwenye hii forum wakichukulia ajali iliyotokea Gongo la Mboto kisiasa.

Pamekuwa na wachangiaji wanaothubutu hata kuhusisha chama cha siasa au ufisadi na milipuko hiyo.

Si ustaarbatu kukurupuka na kutoa majumuisho yasiyo na mantiki. Kulilaumu jeshi au serikali kabla ya kujua chanzo cha milipuko hiyo ni kukosa busara. Wengine wanajidai wanajua hata umri wa mabomu yale, yalivyohifadhiwa na mambo mengine ya taaluma za kijeshi ambazo si kila mtu anazijua.

Tuwe na subira. Kama itagundulika kuwa ni ajali, ieleweke kuwa ajali ni ajali, hata kama ilitokea Mbagala yaweza kutokea pengine pia, hizo ndo ajali.

Mtaalam mmoja wa milipuko amenieleza kuwa mlipuko kama ule unaweza kusababishwa na mambo mbali mbali. Inawezekana ikawa kweli ni umri wa mabomu, au shoti ya umeme au uzembe wa mtu mmoja au hujuma kutoka kwa watu wabaya kama baadhi ya wanachama wa chama cha siasa wanaotaka Tanzania isitawalike.

Tuache kupotosha mambo, tusubiri wataalam wafanye kazi yao na umma utataarifiwa tatizo lilikuwa nini.

Tusubiri wataalamu gani? Yale ya Mbagala mpaka leo bado tunasubiri taarifa kutoka kwa wataalamu. Kumbuka kuna watu humu humu JF ambao ndugu, jamaa na marafiki wameathirika na janga hili. Wengine wamepotzea maisha yao. Hili ni janga la taifa, sio ajali. Yalitokea Mbagala tukahaidiwa na mkky wa nchi kuwa hayatatokea tena. Leo exactly the same incident imetokea tena. Then, utataka kutuambia ni ajali tena. Na kesho kutwa yakilipuka Mgulani utatuambia nini?

Nakubali si ustaarbatu kukurupuka lakini this is too much. Baada ya janga la Mbagala tuliaidiwa kuwa it will never happen again. Wananchi wanayo haki ya kukasirika. Serikali na vyombo vyetu vya habari vimekaa kimya kama vile kilichotokea ni kitu kidogo sana. Nchi nyingine tayari zimeshatoa tahadhari kwa raia wao walio Tanzania kutokanyaga sehemu ya tukio kwa sababu sio salama. Sisi tunawaambia watu warudu kwenye makazi yao.

Kama unasema tusubiri wataalam wafanye kazi yao, then kwa nini wananchi waambiwe eti warudi majumbani mwao? Kweli tuwe na subira but kwa nini Kova anang'ang'ania watu warudi huko? Yeye hana subira? Watu wanalaumu serikali b'se chanzo tayari kinajulikana. Kilichotikea Mbagala is exactly what happened to Gongo la Mboto. Watanzania sio wajinga vile.

Umesema wengine wanajidai wanajua hata umri wa mabomu yale na yalivyohifadhiwa. Inaonekana kama unafanya assumption vile. Unafikiri watu wote hapa ni kama wewe. Eti mlipuko unaweza kuwa umesababishwa na shoti ya umeme. Hivi unaishi wapi wewe to the extent kuwa hujui hata kuwa hakuna umeme?

Na posts zaidi ya 700 kweye hii thread kwako wewe unaona wote wamekurukupa. Ya kwako ndio sahihi. Mkuu unaonyesha hujali kabisa. Badala hata ya kuanza post yako kwa kuwapa pole wale wote waliopoteza maisha au kujeruhiwa kutokana na uzembe unaanza kwa kuponda. Jaribu kuwa na ubinadamu hata kidogo tafadhali.
 
aibu kubwa sana kwa jambo kama hili kiongozi kusema kwenye vyombo vya habari huku akisoma kwenye makaratasi as if ametumwa aseme nini. then anawambia watu warudi makwao na je kama mabomu yameingia ndani kwao kitatokea nini?
 
selikali iliyo corrupt hushindwa kucmamia mambo ya mcngi mku wa majeshi ajiudhuru
 
aibu kubwa sana kwa jambo kama hili kiongozi kusema kwenye vyombo vya habari huku akisoma kwenye makaratasi as if ametumwa aseme nini. then anawambia watu warudi makwao na je kama mabomu yameingia ndani kwao kitatokea nini?

Mbaya zaidi anaonesha kuwa alikuwa hajui kinachoendelea na yeye katumwa kutuliza watu, asivyojua lugha ya Public(diplomasia) anasema eti "NA KUZAGAA HOVYO MITAANI", lugha gani hii anatumia?, Kwa nini jeshi la polisi lisiajiri Public relation officer?, maana kama wasemaji wenyewe ndiyo hawa basi kazi ipo.
 
No big deal (and I ain't tryin' to diss nobody either). However, the truth is CNN iReport is more like DIY kind of journalism. Anybody anywhere with an internet connection can register on CNN iReport and post "Mighty Big Breaking News" or whatever.
 
Back
Top Bottom