Gazeti Mwananchi: CHADEMA sasa Vipande viwili!

Gazeti Mwananchi: CHADEMA sasa Vipande viwili!

Ningeshangaa kama usinge changia kwa kauli kama hii! Hebu nenda mbele zaidi na useme kwa kusadifu mizania. Zk nae alikuwa kwa maagizo ya nani?! Kabla kamati kuu haijapitisha mgombea weka kwenye mizani majina mawili uone la nani linamzidi mwenzake uzito halafu peleka ripoti Lumumba uone ukiwa una wakabidhi ripoti nyuso zao zitakuwaje.

Asubuhi njema! Naona wewe ndio umeingia kazini rasmi kama kawaida 24/7 baadae kidogo kaka.

Hatutaki mzee kwenye urais wa 2015
 
mpaka sasa siamini kama hon.mbowe alitaja jina la dr.slaa kuwa ndiye mgombea wa chadema.nimeelewa kuwa alichokisema ni kuwa yeye(mbowe) hatagombea urais na badala yake atakisaidia chama kupata wagombea wa nafasi mbalimbali ikiwemo ya urais.alienda mbele zaidi na kusema umakini unahitajika hasa kwenye nafasi ya urais ambayo inahitaji mgombea bora na makini na kwamba haipaswi kufanyiwa majaribio.

Binafsi naamini slaa anafaa lakini sipuuzi mchakato wa kidemokrasia utakaompata mgombea bora hata kama matokeo yatakuwa kinyume na mapenzi yangu.nafikiri twende mbali zaidi na kuelewa alichokisema mbowe pale karatu.watu wenye access tunaomba mtuwekee clip ya video tusikie hasa alichokitamka mwenyekiti kisha tuanzie hapo.

Mkanganyiko upo hata kwa wajumbe wa kamati kuu waliotoa maoni yao kwenye gazeti hili.wakati mtei anasema mbowe ametangaza maamuzi ya vikao halali(kwa maana ya kwamba yeye(mtei) anaamini kuwa mbowe ametamka hayo maneno),akina mkumbo na kitila wao wanasema mgombea atapatikana kwa vikao halali huku baregu akihakikisha kabisa kuwa so far hakuna kikao kilichofanyika kumteua au kumpendekeza yeyote.kwa maneno mengine akina baregu na kitila hawaamini kuwa mbowe ametamka maneno hayo.

Nasisitiza kuna haja ya kuielewa kauli ya mbowe na kuithibitisha kwa clips.magazeti yanaweza kuwa yameamua kupotosha kwa makusudi na mzee mtei nina wasiwasi ametoa maoni hayo akiamini kabisa kuwa ndivyo ilivyo.alipaswa kujua mbowe amesema nini kwa uhakika kabla ya kutoa maoni yake.

Inawezekana mbowe hakutaja jina ila sifa hizo za mgombea anayetakiwa anazo slaa basi watu wakaconclude tu kuwa mbowe amemtaja slaa kwa mawazo yao na ikizingatiwa ilikuwa ni karatu,nyumbani kwa slaa.

unashindana kuyakumbatia maji ya mto!!!!!..gazeti la chama tanzania daima limetoa hiyo taarifa ya habari nalo hamliamini tu???
 
Hv nyie magreat thinker wa CDM inakuaje gazeti likiandika habari mnayoipenda mnaliita la umma, likiandika habari msiyoipenda 'limetumwa', kwani CDM haijagawanyika? Ama mlitaka aseme kuna kundi kubwa la dk.slaa na dogo la Zitto?

Na niseme tu kama kweli mbowe alisema yaliyoandikwa basi cdm mnayo bado kazi ya kuimarisha demokrasia, leo ndo mnaona kutangaza nia mapema siyo tatizo lakin wakati ZZK anatangaza palichimbika, kama mnaweza kumeza vitamu msishindwe kumeza na vichungu...
 
Gazeti yetu huwa hayatabiriki na wakati mwingine magazeti haya hutumika wakiwa wanajua au hawajui ,tumesoma articles zenye ujumbe hasi kwa jamii hasa hii ni mfano mwingine hai gazeti linatumika kutengeneza mpasuko ndani ya chama ambao si rasmi.

Pamoja na kazi yao ya kuripoti huwa wanatengeneza kitu kama wazo likinunulika na wadau wengine gazeti huandika habari hiyo kwa upande wa pili na kuuza gazeti.

INGAWAJE kero ni nyingi kwenye jamii suala la maji, shule n.k hizi taarifa hazipewi kipaumbele sana kwanini hugusa ilani za za chama fulani hivyo kukibomoa na si kukijenga
 
Chadema wanazidi kuwavueni nguo. Ninawaambia tena nyie Magamba/Masalia/CUF and alike kwamba Yule mtu ambaye CCM hawamtaki kabisa ndiye anafaa kuwa Rais. Sikuzote ukiona asichokitaka adui yako kishikilie hicho hicho wala usiachie ili uzidi kumuumiza Adui.
Mkuu mimi binafsi si mshabiki/mwanachama/mpenzi wa chama chochote cha siasa. ebu nieleweshe katiba ya CDM inasema chama kinampataje mgombea wake wa Urais.

Je alichofanya Mbowe kumteuwa Slaa ni halali kikatiba? na kama Si halali huoni wanao sapoti uteuzi alofanya mbowe Wanakanyaga katiba ya Chama chenu tukufu. Je kuna haja ya Mbowe kufuta kauli yake ikithibitika amekosea kikatiba. au CDM katiba ni pambo tu....

Mbowe, Mtei, Slaa wanaweza kuamua chochote na nyie washabiki mkashabikia hata kama ni kinyume na taratibu za Chama. NB. Sina chama ilia sikosi kupiga kura ktk chaguzi zote zilizopita.
 
“Ninaunga mkono Dk Slaa kuwania tena nafasi ya urais mwaka 2015. Mwenyekiti amemtangaza baada ya kupata baraka ya vikao vya chama,” alisema Mtei.( mwananchi dec 21,2012)
....kikao kimefanyika lini??mbona hamjibu??

Hili swali halijibiki kaka.
 
Nadhani unafikiri mimi ni muuza chai kama wewe! Its Freshthinking, wenye mawazo mgando nikiwagundua huwa najitenga nao. All the best bro, nitakuwa nakusoma tu kujiepusha na shari.

Masalia kumi ni sawa na mwanaChadema mmoja.
 
Mkuu mimi binafsi si mshabiki/mwanachama/mpenzi wa chama chochote cha siasa. ebu nieleweshe katiba ya CDM inasema chama kinampataje mgombea wake wa Urais. Je alichofanya Mbowe kumteuwa Slaa ni halali kikatiba? na kama Si halali huoni wanao sapoti uteuzi alofanya mbowe Wanakanyaga katiba ya Chama chenu tukufu. Je kuna haja ya Mbowe kufuta kauli yake ikithibitika amekosea kikatiba. au CDM katiba ni pambo tu.... Mbowe, Mtei, Slaa wanaweza kuamua chochote na nyie washabiki mkashabikia hata kama ni kinyume na taratibu za Chama. NB. Sina chama ilia sikosi kupiga kura ktk chaguzi zote zilizopita.

Huo udaku peleka Lumumba.
 
Mkuu Molemo, soma kauli za Prof Baregu, na Dr Kitila Mkumbo.

Bado kauli ya Zitto, nikuchochea kuni mbichi ili moto uzidi kuwaka.

As you wish..Subiri mkono wa binadamu udondoke.Akili ya Fisi bana!
 
Last edited by a moderator:
Ukisoma vyema kabisa utaona umakini wa wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA hao ambao kimantiki wanakubaliana na kauli ya Mwenyekiti ambaye alisema wazi kuwa kwa nafasi yake ataongoza vikao ili kusimamia chama kipate wagombea sahihi, huku akitilia mkazo kwenye nafasi ya urais kuwa ni nafasi nyeti ambayo chama kupitia vikao hakiwezi kuifanyia mzaha.

Alichosema Mbowe ni kuwa yeye hatagombea ila anaheshimiana sana na Dr Slaa. Sasa hapo tangazo la Mbowe kuwa amemteua Slaa kuwa mgombea urais ni lipi? Hivi mwananchi nao sasa wanaandika kama gazeti la Uhuru?
 
unashindana kuyakumbatia maji ya mto!!!!!..gazeti la chama tanzania daima limetoa hiyo taarifa ya habari nalo hamliamini tu???

Nitajie Tanzania daima la lini limethibitisha kuwa Mbowe amemtaja Slaa kama mgombea urais chadema.
 
Kuna mtu mshipa wa kongosho umemtoka kutetea mabwana zake.
 
Hili bomu ukiunganisha na BOmu kubwa linalokuja ndani ya mwezi wa kwanza au wa pili,Naona CHADEMA ikizama kwenye kina kirefu cha tope kuinasua itachukua miongo kadhaaa.Nakuhakishieni wenye kupuuza puuzeni but soon mambo hadharani
Kukufukuzeni uanachama wewe unaona ni bomu.?

Kamanda Ben Saanane kuna mhalifu hapa.
 
Last edited by a moderator:
wengine kumuunga mkono zitto kuwamgombea urais 2015 ni laana na haramu! Ila mbowe kumuunga mkono slaa agombee urais 2015 ni ruru na ukomavu wa kisiasa! Tukiiacha hali hii iendelee kwa kuogopa kwamba utaniitwa mnafiki au umetumwa na ccm tutaishia kuzalisha maidiamini dada ndani ya taifa la amani.

Hili nalo neno ingawa umepigwa ban pole sana.
 
Gazeti yetu huwa hayatabiriki na wakati mwingine magazeti haya hutumika wakiwa wanajua au hawajui ,tumesoma articles zenye ujumbe hasi kwa jamii hasa hii ni mfano mwingine hai gazeti linatumika kutengeneza mpasuko ndani ya chama ambao si rasmi .pamoja na kazi yao ya kuripoti huwa wanatengeneza kitu kama wazo likinunulika na wadau wengine gazeti huandika habari hiyo kwa upande wa pili na kuuza gazeti .INGAWAJE kero ni nyingi kwenye jamii suala la maji ,shule n.k hizi taarifa hazipewi kipaumbele sana kwanini hugusa ilani za za chama fulani hivyo kukibomoa na si kukijenga

leo ndo mnao hilo bz limeandika mpasuku wa chadema???.... muulizeni mzee mtei kikao kimefanyika lini cha kumteu dr.slaa,, na mbowe akiwa kama mwenyekiti kwa nini leo atangaze mgombea wa urais ..haoni kama anakula mate yake mwenyewe ambayo kila siku anahubiri demokrasia ndani ya chadema.... ZITTO alitangaza nia povu liliwatoka mbowe ,mtei,dr.slaa leo katangazwa dr.slaa kuwa ndo mgombea hakuna shida... ukweli uko wazi ndani ya cdm hakuna demokrasi hata kidogo... wenye chama ni mbowe,slaa,mzee mtei na sasa anaingizwa lema...
 
Back
Top Bottom