Gazeti Mwananchi: CHADEMA sasa Vipande viwili!

Gazeti Mwananchi: CHADEMA sasa Vipande viwili!

kasome gazeti la chama TANZANIA DAIMA

mimi ninataka nione video/nasikie kauli ya Mh.mbowe akihutubia huko karatu.kama hawawezi kutuwekea hiyo clip basi tukubaliane kuwa gazeti la mwananchi lina ukweli fulani kwani kwenda kumtangaza mgombea wa urais bila kupata baraka za vikao vya chama hasa kwa chama kubwa kama CDM ni sawa na kuendeleza migawanyiko ndani ya chama............................
 
[h=5]Demokrasia ni kuchagua moja kati ya nyingi zinazoshindana,demokrasia sio kuteua moja kati ya moja inayoogopa kushindanishwa![/h]
 
Naomba utusaidie kutuwekea ile clip ya hotuba ya mh.mbowe akiwa karatu ili tujue kama kweli alimtangaza Dr.slaa kuwa mgombea urais 2015 au la.
Ukiweza kutuwekea hiyo clip hapa ndipo tunaweza kujua kama hii habari ya gazeti la mwananchi ina lengo nzuri au la kwa CDM.

Mkuu.
Usiingie kwenye mtego! Kauli ya Mbowe kama ilivyo nukuliwa na Tanzaniadaima la jana ni hii hapa.
"
Akizungumza na wananchi wa Karatu kwenye Uwanja wa mpira wa Karatu baada ya kumaliza kikao chake na viongozi wa Karatu, Mbowe alisema kwa sasa amejielekeza kupanga na kutekeleza mikakati kuhakikisha CHADEMA inaingia Ikulu mwaka 2015 na kuhakikisha anasimamia kupata viongozi bora wa kupeperusha bendera ya chama hicho kikuu cha upinzani.

Mbali na kusimamia upatikanaji wa mgombea bora wa urais, Mbowe alisema pia kazi yake kubwa itakuwa kuhakikisha anasimamia upatikanaji wa wagombea bora wa nafasi zote za uongozi kuanzia ngazi ya serikali za vijiji, vitongoji, madiwani, wabunge na urais.

"Kuna taarifa za upotoshaji zinaenezwa kuwa mimi na Dk. Slaa tuna ugomvi wa kuwania urais. Jambo hili sio kweli hata kidogo, mimi sitawania urais mwaka 2015 na Dk. Slaa nafanya naye kazi kwa kuheshimiana na maelewano ya hali ya juu kwani tumekuwa wote kwa muda mrefu sasa," alisema Mbowe".
 
A day will come, utayakumbuka haya maneno unayoyasikia humu JF. CHADEMA isporekebishwa itakuja kuwa kama vile uongozi wa ASSAD wa Syria aliondoka baba akaja mtoto, Congo kwa Kabila, CDM ameondoka muanzilishi akaja Mkwe wake. 'CDM hakuna checks and balance', it is an owner managed party where all decisions are concentrated to party owners. Wengine mnacheza ngoma msiyoijua.

Masalia mna shida sana.Hakika mmeshikwa pabaya.

Nyerere alimwambia Mrema 'I cant let my country to the dogs'
 
Pro-Chadema JF naombeni majibu, kwa nini Chadema kinaitwa chama cha demokrasia wakati hakuna demokrasia.

Uzuri wa majina mara nyingi sio reflection ya hali halisi. Hebu tizama hili jina Lord Resitance Army (LRA), unaweza kukisia kazi zao zinahusiana na kitu gani, tabia zao zikoje (Assume hujui kinachoendelea duniani)?.
 
[h=5]Demokrasia ni kuchagua moja kati ya nyingi zinazoshindana,demokrasia sio kuteua moja kati ya moja inayoogopa kushindanishwa![/h]

Nimeona status hii kwenye FB yenu Masalia mnayoitumia kuwatukana matusi Mbowe na Dr Slaa.
 
@Mohmedi Mtoi, Unajipendekeza kwa viongozi wa Chadema mpaka unatia aibu.

Wasome wakaskazini wenye chama kina Mtei, Molemo, kauli zao.
 
“Ninaunga mkono Dk Slaa kuwania tena nafasi ya urais mwaka 2015. Mwenyekiti amemtangaza baada ya kupata baraka ya vikao vya chama,” alisema Mtei.( mwananchi dec 21,2012)


....Ashakum si matusi, huyo Mzee tayari hayupo sawa kichwani, haiwezekani eti Mtei hajui kuwa chama hakijateua bado mgombea urais, huyu sasa apumzike maana bila shaka sasa ubongo wake umeshachoka....
 
Uzuri wa majina mara nyingi sio reflection ya hali halisi. Hebu tizama hili jina Lord Resitance Army (LRA), unaweza kukisia kazi zao zinahusiana na kitu gani, tabia zao zikoje (Assume hujui kinachoendelea duniani)?.

Masalia mmechemsha mazima.
 
Kamanda Molemo,
Naona unapingana na ukweli. Chadema sasa vipande viwili huo ndiyo ukweli.

Dr Kitila Mkumbo, Prof Baregu wampinga Mbowe, Mtei, Lema, na Heche wapo upande wa Dr Slaa.

Bado kuna makundi mawili ya Bavicha moja lipo upande wenu wa Dr Slaa na Mbowe na kundi lingine la Zitto.



SIDHANI HATA KAMA BREAKFAST YENYEWE UMEPATA, AU JUMA TATU HII UMEFUNGA SWAUMU ILE YA SUNNAH YA KIPENZ CHETU S,A,W?
UNAJICHANGANYA CHANGANYA NA KUWEWESEKA KAMA VILE UMEANGUSHA SINDANO KARIAKOO KWENYE MSONGAMANO WA WATU NA UNAHAHA KUINAMA INAMA UKIITAFUTA HUKU WALE WAPITA NJIA WAKIKUGASI GASI NA KUKUONDOLEA UMAKIN
MKUMBO SI YUKO UPANDE WA ZIITO?

au ww hujui
 
Gazeti la Mwananchi limetoa habari ambayo ni tofauti kabisa na Maudhui yake.

Habari hiyo inasema CHADEMA SASA VIPANDE VIWILI kuhusu Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kumtangaza Dr Slaa kugombea Urais 2015. Lakini ukisoma habari yenyewe hakuna mahali popote panapoonyesha CHADEMA sasa ni vipande vipande.

Ni habari iliyowekwa Heading hiyo kwa malengo yasiyofahamika. Endelea....

=================

SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kumtangaza Dk Willibrod Slaa kuwa ndiye mgombea wa urais mwaka 2015 kwa tiketi ya chama hicho, makada wa chama hicho wamegawanyika baadhi wakimponda na wengine kumuunga mkono.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, baadhi ya makada wa chama hicho walisema mwenyekiti wao amekosea kumtangaza mgombea kabla ya wakati, huku wanaomuunga mkono wakisema hajakosea kwa sababu hatua hiyo itasaidia kuondoa makundi ndani ya chama hicho.

Juzi, Mbowe akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Karatu mkoani Arusha, alisema Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willibrod Slaa atapewa fursa ya kuwania tena urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015, huku mwenyewe akijiweka kando kuwania nafasi hiyo.

Hata hivyo, Dk Slaa alipoulizwa iwapo ana nia ya kuwania nafasi hiyo alihoji: "Kwani mwaka 2010 nilijitangaza mwenyewe,? Iwapo wanachama wa Chadema watanipendekeza nitafikiria kufanya hivyo." Mwasisi wa chama hicho Edwin Mtei, Wajumbe wa Kamati Kuu; Profesa Mwesiga Baregu na Dk Kitila Mkumbo, Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa Bavicha John Heche na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema walitoa maoni yanayopingana kuhusu kauli hiyo ya Mbowe.

Wanaounga mkono

Mtei alisema anaunga mkono kauli ya Mbowe akisema kiongozi huyo hajakosea kumtangaza Dk Slaa kuwania urais mwaka 2015.


"Ninaunga mkono Dk Slaa kuwania tena nafasi ya urais mwaka 2015. Mwenyekiti amemtangaza baada ya kupata baraka ya vikao vya chama," alisema Mtei.

Ingawa Mtei hakuwa tayari kusema ni kikao gani kilichopitisha jina la Dk Slaa kuwania nafasi hiyo, alisisitiza: "Kuna vikao vya Kamati Kuu vimefanyika hivi karibuni, vinaweza kuwa vimefanya uamuzi huo. Mwenyekiti hawezi kuzungumza jambo bila baraka za vikao vya chama."

Hata hivyo,
kauli hiyo ya Mtei inapingana na ile aliyoitoa Oktoba 6, mwaka huu baada ya Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini kutangaza kutogombea tena ubunge badala yake kusema anataka kugombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Mtei alisema hatua ya Zitto kutangaza kuwania urais mapema kungesababisha mzozo na mpasuko ndani ya chama hicho.

Mtei alisema amekuwa akimshauri Zitto mara kwa mara kuhusu hatua yake hiyo akimtaka kuwaunganisha wana Chadema na siyo kuwagawa au kuwavuruga.

"Hakuna shida kuonyesha hisia, lakini unatengeneza mzozo mkubwa sana ukitangaza sasa. Mimi nimeshamshauri sana Zitto, ahakikishe anakiunganisha chama na siyo kukigawa wala kukivuruga."

Alisema mbunge huyo kutangaza kutogombea tena ubunge na badala yake kujipanga kuwania urais mwaka 2015 kumekuja mapema mno na kuonya kuwa itaibua mzozo ndani ya Chadema.

Mtei ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki Kuu enzi za utawala wa Mwalimu Julius Nyerere, alisema kwamba wakati mwafaka ukiwadia, Chadema kitaamua ni nani mwenye sifa za kugombea urais huku akisema kina utaratibu wake wa kuwapata wagombea mbalimbali wa uongozi.

Hata hivyo, Zitto jana alikataa kuzungumzia suala hilo akisema: "Nimesikia hata mimi kwenye vyombo vya habari ila sina cha kuzungumza kuhusu hilo."

Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), John Heche alisema kauli hiyo Mbowe siyo yake binafsi, bali ni ya wananchi.

"Ni kauli na maoni ya Watanzania wanaomwamini Dk Slaa kuwa anaweza kumudu kuliongoza taifa hili kama walivyoonyesha kwa kumpigia kura nyingi kuliko mgombea yeyote wa upinzani katika nafasi ya urais (mwaka 2010)," alisema Heche.

Heche alisema ingawa ndani ya Chadema kuna viongozi wengi wenye uwezo wa kuliongoza taifa, nyota ya Dk Slaa bado inang'ara.

Msimamo wa Heche uliungwa mkono na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ambaye alisema ni sahihi Dk Slaa kugombea urais mwaka 2015.

Lema alisema katika historia ya chaguzi za vyama vingi nchini, hakuna mgombea wa upinzani aliyewahi kupata kura nyingi kama Dk Slaa mwaka 2010 akadai kwamba ndiyo maana hivi sasa CCM kinafanya kila njama kumdhoofisha.

Lema alisema hatua ya kumtangaza Dk Slaa kuwa mgombea wa urais mwaka 2015, itaondoa harakati za chinichini zilizokuwa zikifanywa na watu ndani na nje ya Chadema kuwagombanisha viongozi wakuu wa chama hicho, hasa Mbowe na Dk Slaa.

Wanaopinga

Wakati Mtei akieleza kuwa Mbowe amepata Baraka za chama,
Profesa Baregu alisema kutangazwa kwa jina la Dk Slaa kuwania urais ni maoni binafsi ya mwenyekiti huyo.

"Hayo ni maoni yake, lakini vikao vya chama ndivyo vyenye uamuzi wa mwisho kuteua jina la mgombea urais na havijakaa," alisema Profesa Baregu.

Alipoulizwa maoni yake kuhusu sababu za Mbowe kumtangaza mgombea urais sasa kabla ya wakati, Profesa Baregu alisema: "Mbowe atakuwa amefanya hivyo kwa sababu watu wengi walikuwa wanadhani kwamba yeye pia anawania nafasi hiyo ya urais."

"Hivyo ili kuweka mambo sawa ameamua kutangaza mapema kuwa hatawania urais na kwamba Dk Slaa ndiye anayefaa kuwania nafasi hiyo," alisema.

Profesa Baregu alisema haoni tatizo kwa wanachama wa Chadema kutangaza nia mapema kwa sababu hiyo ni haki yao kwa mujibu wa katiba... "Hata kama watu wengi watatangaza nia ya kuwania urais, siyo jambo baya katika ujenzi wa demokrasia, lakini uamuzi wa mwisho ni wa vikao vya chama."

Kauli ya Profesa Baregu kuhusu vikao iliungwa mkono na Dk Mkumbo ambaye alisema kwamba anachojua vikao vya chama ndivyo vyenye uamuzi wa mwisho kuhusu uteuzi wa wagombea wa ngazi ya urais.

Dk Mkumbo alionyesha shaka kama kweli Mbowe alimtaja Dk Slaa kuwa ndiye atakayewania nafasi hiyo akisisitiza: "Ninachofahamu ni kwamba yeye ametangaza kuwa hatagombea nafasi hiyo."

kwenye red ni maeneo ambayo mwandishi aliyazingatia katika uandishi wake hususan maoni ya mtei na baregu
 
Mimi nimeomba clip kwani kutokana na hizi siasa chafu zinazochezwa hapa nchini imefika mahali vyombo vingi vya habari vimekuwa bias ktk kuripoti habari; mfano kuna hawaamini kama Tanzania Daima linaweza kuandika habari inayoikosoa CDM, gazeti la uhuru haliwezi kwenda kinyume na CCM na wengine wanasema gazeti la mwananchi linaegemea kwa zitto kabwe n.k.
Kwa mtazamo huu nimekuwa makini sana ktk kuamini habari za kisiasa bila kufuatilia vizuri.
 
....ashakum si matusi, huyo mzee tayari hayupo sawa kichwani, haiwezekani eti mtei hajui kuwa chama hakijateua bado mgombea urais, huyu sasa apumzike maana bila shaka sasa uzee umeshamuingia kwenye ubongo....


bora wewe umefumbua macho umeona hilo,,LA...akisema ye ndo basi...alimjia juu zitto lakini kwa dr.slaa na mbowe hakuna shaka.
 
Mbowe alisema Dr Slaa atapewa fursa ya kugombea lakini yeye binafsi hatagombea. Mazingira ya kauli ya Mbowe ni baada ya magazeti na vyombo vingi vya habari kusema Mbowe na Dr slaa wapambana kwa ajili ya nafasi ya urais. Kuweka sawa kasema yeye hapana ila Dr Slaa atapewa nafasi tena kutokana maoni ya wananchi walio wengi.

Sasa hao wanaotaka kuchanganya habari lengo lao nini.
 
pro-chadema jf naombeni majibu, kwa nini chadema kinaitwa chama cha demokrasia wakati hakuna demokrasia.

nawewe pro ccm utujibu,kwanini chama chenu kiitwe chama cha mapinduzi?
Mapinduzi ya kuifanya nchi hii kutoka ya kijamaa kwenda kwenye nchi ya kifisadi??
 
@Mohmedi Mtoi, Unajipendekeza kwa viongozi wa Chadema mpaka unatia aibu.

Wasome wakaskazini wenye chama kina Mtei, Molemo, kauli zao.

Wewe Ritz ndiye unatia aibu unajipendekeza Lumumba mpaka unatia kinyaa.
 
Last edited by a moderator:
TANZANIA DAIMA DEC 31,2012 (
ila aliweka bayana kuwa mgombea wao wa mwaka 2010, Dk. Willibrod Slaa, bado anatosha kugombea wadhifa huo kutokana na kazi nzuri aliyoifanya ya kuwapatia wabunge wengi.
Msimamo huo wa Mbowe, jana ulitawala katika mijadala ya wananchi kwenye mazungumzo ya kawaida na mitandao ya kijamii, huku wengi wakimuunga mkono na kudai si king'ang'anizi wa madaraka.)

[TD="bgcolor: #ffffff"][/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"][/TD]

Mtoi aliuita mtego kwa vile Mwannachi iliripoti. Sasa kwa vile na Tanzania daima wamekariri, atakuja aseme; Kwa vile chama kimeamua basi ndio ivo ivo! Kuweni huru guys kutoa maon yenu hata kama yanapingana na chama. Hiyo ndiyo itakayosaidia kujenga taasisi yenye nguvu inayoweza kisimama peke yake badala ya kutegemea majina.
 
Gazeti la mwananch sikuhizi wanaandika habari ya kuisifia CHADEMA kesho yake wana ikandia, hiyo wanaifanya makusudi ili kuwagawa wananch, hako kamtindo nimejaribu kukafuatilia nimebaini hilo na nimejilisha kabisaa.

Mwananchi limekaa kimtego mtego na kwanguvu za Allah hawato weza mwisho wake watakua kama gazeti la uhuru na mzalendo habari leo jambo sijui nini vile nk, magazeti yamebaki mawili tu,TANZANIA DAIMA NA MWANA HABARI hayo mengine ni yaudaku kama ya shigongo wa ccm
 
Back
Top Bottom