Gavana Prof. Ndulu: Benki wapo sahihi

Gavana Prof. Ndulu: Benki wapo sahihi

Pale benki inapochaji bank charges yaani makato kwa muamala wowote ujue ndio mapato ya benki. Pale ipochaji interest kwenye mkopo ujue ndio mapato ya benki. Makato ya namna yoyote yale kwa ujumla yafanywayo na benki ndio 'REVENUE' yake.
Mwisho wa mwaka wa mahesabu lazima mapato yote hayo yachajiwe kodi tunaita 'income tax' ama corporate tax..
Sasa serikali kama itaamua kuchaji VAT kwenye makato yoyote ya miamala ya kibenki ama taasisi ya kifedha maana yake ni kuwa hio VAT anawekewa anayekatwa. Mwisho wa mwezi benki hupeleka VAT hio TRA kwa kufanya hesabu za ulinganisho wa output na input VAT. Kila mwisho wa mwezi lazima hesabu hizo zifanyike na TRA kupata chao. Mara nyingi unaweza kukuta TRA hawapati kitu yaani wanadaiwa baada ya kufanyika mahesabu hayo ya VAT.
Sasa, serikali inapoamua kuchaji VAT kwa kila muamala wa mteja wa benki kwa namna alivyosema CG-Commissioner General maana yake ni kuwa hio sio VAT bali ni income tax yenye rate ya 18% badala ya 30% inayotakiwa kuchajiwa kwenye corporate businesses! Kwa hio hapo anachoongelea CG sio VAT bali ni income tax.!
Kwa mujibu wa kanuni za kodi za nchi yetu income tax huchajiwa mwishoni mwa mwaka wa mahesabu na VAT huchajiwa kila mwezi. Maana yake ni kwamba serikali iseme jina la kodi hio itakayokatwa kwenye muamala wa mteja lakini wasisema VAT maana sio VAT. Ama kama wamekubaliana na benki; benki wakatwe kwenye miamala wanayoyafanya basi mwishoni mwa mwaka itabidi benki ilipe corporate tax ya 12% maana 18% iliShachukuliwa kwa kila mwezi. Of which kitu kama hiki hakipo kwenye kanuni za ki kodi!
Nilichoelewa ni kwamba. Kwanza, Serikali wanataka kugawana na benki makato wanayokatwa wateja. Tatizo kubwa ni kuwa walidhani jina VAT ndio itatimiliza malengo hayo vizuri, bila kujua namna VAT inavyotakikana kuchajiwa. Pili, naona hawajaangaliana kwa kina kuhusu namna benki inavyopata mapato yake ambayo mwisho wa siku hulipia kodi. Tatu, hakuna namna yeyote ile serikali ikataka kuchaji kodi kwenye hizi miamala za kibenki halafu wananchi wasibebeshwe mzigo. HAKUNA. Nne, Naona Serikali haijabaini kuwa VAT kwenye maisha ya wananchi wa kawaida ndio inaongeza gharama za maisha. Naweza kusema kwa 'jicho la tatu' VAT inasaidia kwa kiwango kikubwa sana kudhoofisha sarafu ya Tanzania kutokana na kutundikwa kwenye bidhaa nyingi zenye watumiaji wa kawaida!
Ndio hivyo!
 
Tra hakuna wajuvyi wa kodi, nafasi nyingi za kugaiana tu. Hata hio vat juu ya ada ni utumiaji mbovu wa vat. Sio kila mahala una toza vat.
Hii kwa uerfu ni valu added tax. Inatumika pale mlaji anapo nunua kitu. Hutumika zaidi kwenye bidhaa na sio kwenye services. Na hii ni kodi ambayo kuna wengine wapo excempted mfano diplomats . Hawa wanapo nunua kitu au service basi huomba refund...ni usumbufu sana ila tra hawajui ku plan mambo yao kwani wana ukosefu wa wataalam wa kububi hiw yo implement tax wanazo zitunga.
Na hili la bank vat haikupaswa kuwekwa kabisa , ndio kama lile la utaliii....
Gharama za kuweka fedha benki hazitakiwi ziwe juu . Ukiweka vat ni wazi banki wata ongeza juu ada zao kufidia ile iliokatwa na vat....hivyo gharama zinaenda kwa mteja.
Tukumbuke fedha zozote zinazo wekea bank tayari aidha ni income au revenue ya makampuni au mishahara ya wafanyakazi ambao wanapitishia fedha benki.
Hizi fedha sio product, hizi tayari ndani yake kuna vat ya tra , kuna stamp duty ya tra, kuna WHT ya tra pia kuna corporate tax ya tra...na kwa wafanya kazi ni net income baada ya kutoa payee. Kuzitoza kodi kwa njia yoyote ile hata kwa kuongezeka ada juu kutokana na kuanzishwa vat ya ada sio sawa kabisa kabisa..ni kodi haramu au kodi jipu
Dah! Nasoma hili andiko mara mbili mbili inauma sana Macos upo sahihi sana, kulingana na hili tumeshamuandikia barua muhasibu wetu sie kama wafanyakazi kuomba mishahara tulipwe dirishani na si benk kama awari. Tunalipaje value added tax kwenye service? Kwa maana nyingine hata hospital walitakiwa waweke hii Vat ila wameona soni tu.
 
nashangaa ina maana hakuna mawasiliano kati ya hawa watendaji kabla ya kutoa matamko??
 
Hii VAT ya kwenye Transactions JPM na watu wake amekosea sana,Asifikiri tutamsifia kwa kila kitu.Kawaida VAT hutozwa kwa "mlaji wa mwisho" na kawaida hutozwa kwenye bidhaa na si huduma...Kwa maana ya services.Hela inapoingia bank iwe ni kwa mkopo,mshahara au vyovyote,kodi za namna tofauti zinakuwa tayari zimelipwa.

Sasa unapoenda kukata VAT kwa mfanyakazi mwenye kuchukua mshahara kupita bank,wakati umeshamkata PAYE ndani ya hako hako kamshahara unategemea nini??Hawa ngoja tuwali timing....2020 ni kuwafutilia mbali.Semina umekata,kusoma hutaki...Uje.sca hatutaki sisi
 
Huyu gavana hana msaada wowote nchini..ndio maana BOT ina mauzauza kibao..atoke tu hizi nyakati zimemzidi uwezo.
Prof ameongea ukweli mchungu, madhara ya wapinzani kutoshiriki bunge la bajeti yanaonekana, huu ndio mwanzo tu makubwa yataibuka, muda ni mwalimu mzuri tusubiri muda utaongea
 
Hii VAT ya kwenye Transactions JPM na watu wake amekosea sana,Asifikiri tutamsifia kwa kila kitu.Kawaida VAT hutozwa kwa "mlaji wa mwisho" na kawaida hutozwa kwenye bidhaa na si huduma...Kwa maana ya services.Hela inapoingia bank iwe ni kwa mkopo,mshahara au vyovyote,kodi za namna tofauti zinakuwa tayari zimelipwa.

Sasa unapoenda kukata VAT kwa mfanyakazi mwenye kuchukua mshahara kupita bank,wakati umeshamkata PAYE ndani ya hako hako kamshahara unategemea nini??Hawa ngoja tuwali timing....2020 ni kuwafutilia mbali.Semina umekata,kusoma hutaki...Uje.sca hatutaki sisi
......Uje.sca hatutaki sisi nimeipenda hiyo.[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
Hiyo ni point moja kwa upinzani,tuendelee kuisoma ikigeuka juu chini hadi iwarudie ccm
 
Sasa kukata mzizi wa fitna,wabadilishe kauli, wasiite VAT waseme wameongeza gharama za huduma za kibenki tutawaelewa maana si kila siku wanaongeza bei?mbona sukari tulinunua 4000 kilo?
 
Zamani walikuwa hawatozwi na walikuwa wanatukata.. Basi wangeacha kukata.. Au wanataka walipe na zile zote za nyum?

Zamani walikuwa wanakata nini? Unaposema "wanataka walipe na zile zote za nyuma" una maana gani? Unauhakika gharama za kibenki zilikuwa zinajumuisha VAT? Kwamba mabenki haya yalikuwa yanakusanya VAT kinyume cha sheria na bila kuiwasilisha TRA? Maana VAT kwenye hizo ada zinazotozwa kwa huduma mbalimbali za kibenki imekuwa introduced sasa.
 
Haahaa kwa hii sred,ma ccm wote walio pitisha hiyo sheria wako[emoji102] [emoji102] [emoji102] [emoji15]
 
ata jambo dogo kama hili at a mtoto wa form one anayesoma bookkeeping na commerce analielewa vizuri tu.
Tukubari tu hii wizara imeshakuwa ngumu.

Kama sikosei kiongozi wetu keshaomba msaada Rwanda.
 
Tusiwe wavivu wa kupata taarifa sahihi mabenki yapo sahihi na prof yuko sahihi tatizo tuna wabunge wengi wa ccm uelewa wao wa mambo ni mdogo saaana hawasomi.Naomba watu waaome income tax practise notice number 05/2013 iliyotiwa sahihi tarehe 1/11/2013 inayozungumzia business income ndio utajua sasa wakuu wameamua kwa makusudi kupindisha sheria za nchi.

Na lazima tujue VAT as per international taxation laws mlipaji ni final consumer and not otherwise.kama tumeamua kuwa na ' VAT' ya definition ya kibongo kibongo well and good lakini is not health kwa elimu yetu watu wako vyuoni wanasoma hivi halafu in practices wanakuta vike its ridiculous and shame kwa watu walioshiriki kupitisha mambo ya hovyo kama haya

Move hii inaonesha mwelekeo mbovu wa serikal yetu! Viongozi husika yaani BOT na TRA wanavyopingania kwenye media! inamaana hawakukaa pamoja kushauriana juu ya kuongeza kodi hiyo na pili hawana mahusiano mazuri! kwa nini wasikae pamoja wakafanya muainisho mzuri ndipo waje kwenye media waondoe mkanganyiko huu? hiyo ndo picha ninayoiona mimi!
 
Unakuwaje kamishna wa TRA afu unamislead umma juu ya kodi?na wote ktk taasisi mlioshiriki kutoa huo waraka na maelezo tuwaeleweje?
I suggest watu wawajibike hapa
Tuweke siasa pembeni mda mwingine

Kwa kweli anapaswa kujiuzulu mara moja. Hii ni fedheha kubwa.
 
Move hii inaonesha mwelekeo mbovu wa serikal yetu! Viongozi husika yaani BOT na TRA wanavyopingania kwenye media! inamaana hawakukaa pamoja kushauriana juu ya kuongeza kodi hiyo na pili hawana mahusiano mazuri! kwa nini wasikae pamoja wakafanya muainisho mzuri ndipo waje kwenye media waondoe mkanganyiko huu? hiyo ndo picha ninayoiona mimi!

Utakuta ni Mkuu wa Nchi alitoa maelekezo na wataalamu wetu hapo TRA/Wizara ya Fedha wakaogopa kupingana na mkubwa. Na bahati mbaya sana serikali ikishakosea basi kwa kuwa kule bungeni hamna kitu.
 
Dah! Nasoma hili andiko mara mbili mbili inauma sana Macos upo sahihi sana, kulingana na hili tumeshamuandikia barua muhasibu wetu sie kama wafanyakazi kuomba mishahara tulipwe dirishani na si benk kama awari. Tunalipaje value added tax kwenye service? Kwa maana nyingine hata hospital walitakiwa waweke hii Vat ila wameona soni tu.
Insurance ina VAT,.. Haha tusipochunga wanakuja na huku aisee
 
Back
Top Bottom