Gavana Prof. Ndulu: Benki wapo sahihi

Gavana Prof. Ndulu: Benki wapo sahihi

Huyo prof naye hajui. TRA wamesema mabenki yalikuwa yakusanya bila kulipa. Sio new makato. Mwee
mkuu naona wewe ndo hujui, kipindi ambacho walikuwa hwalipi nao hawakumtoza mteja wao, walipoanza kulipa nao wameanza kutoza mteja! tatizo lipo wapi? kama wangelipishwa toka zamani nao wangelitoza toka zamani hizo.
 
Huyu gavana hana msaada wowote nchini..ndio maana BOT ina mauzauza kibao..atoke tu hizi nyakati zimemzidi uwezo.
We huelewi haya mambo, ni vyema ukijinyamazia ukasoma koment za watu tu! Hivi watu mkiona bank mnafikiri kule ndo hela zimerundikwa tu bira hesabu. Mi nafanya kazi bank hali ya uchumi siyo nzuri, kuendesha bank si kitu rahisi. serikal kusema bank hazilipi si kweli! mitandao ya kijamii skuzote kulikuwa na kiasi cha makato kinachokwenda serikalin! Leo nyie mnamdharau Gavana! Nduru ni gavana moja mzuri sana asiyekubari kuyumbishwa! kwa serikal hii tukiwa na viongoz watakao kubari kuongozwa kwa remot uchumi wa nchi utaanguka kabisa!
 
Kwa mawazo haya basi safari ni ndefu.

Utasemaje mabenki yalikuwa hayalipi kodi wakati wanalipa corporate tax kwenye faida wanazopata? Na moja ya mapato yao ni bank charges?

Pia, kama unaongelea VAT, hiyo VAT ilikua exempted in previous Acts, hivyo hawakupaswa kuzilipa.

Kuna watu wanajua kodi ni kodi. Hawajui tofauti ya corporate tax wala VAT. Si ajabu haya ndo mawazo ya wakubwa. Ujinga mtupu.
Ukisikiliza mfano aliouto kamishna wa TRA ni kama vile kulikuwepo na kodi ambayo haikuwa inalipwa. Katoa mfano kwamba kama tozo lilikuwa 1000, na bank walikuwa wanachukua lote sasa itabidi tozo hilo hilo litozwe kodi ya 18% ambayo na kama sh 153 na sh 847 ndio ibaki bank. Ikiangalia vizuri huo mfano wake ni kwamba ile sh1000 iliyotozwa na bank tayari ina VAT ambayo ilikuwa hailipwi jambo ambalo sio kweli kwani kulikuwa na exemption kabla sheria kubadilishwa hivi karibuni. Kwenye hiyo 1000 TRA wanatakiwa wachukue 180 na sio 153. Na mteja ambaye hii kodi ya VAT ndiye hasa inamhusu atalipa 1180 badala ya 1000 ya awali ambayo ilikuwa imesamehewa VAT. Huo ndio ukweli nyingine ni porojo tu. VAT ni kodi ya mlaji wala sio ya mfanyabiashara.
 
Gavana yupo sahihi wengine wote wanamumunya maneno. Kwa mfano umekwenda kununua bidhaa let's say ya 1,000,000tshs bila VAT utalipa hiyo amount hapo juu na ukiuziwa na VAT bei itaongezeka na kuwa 1,180,000. Sasa mnataka kuniambia mwenye duka atakubali kukulipia wewe mteja 180,000 au wewe mteja ndiye utakayelipa hiyo 180,000.?
Vivyo hivyo kwa mabenki hawatakubali kumlipia mteja VAT ya let's say transaction ya ku-withdraw laki moja walikua wanakukata bank fee ya 2,000 bila VAT then sasa hivi na VAT bank fee itakua 2,360. Tatizo lipo hapo kwenye VAT. Mwenye benki na Mteja wa benki anaona anaonewa na muuza duka na mteja anayenunua vitu dukani pia anaona anaonewa kwa sababu wote hatujazoea.
Kama nilivosema mwanzoni gavana aweza kuwa sahihi ameongea bila kumung'unya maneno hao wengine wote wanatugeukia mwisho wa siku mtakujajua
 
Nimefuatilia kwa makini michango ya mabingwa humu na nimejiridhisha pasi na shaka kwamba KOSA NAMBA MOJA lililofanywa na Serikali na Bunge ni jina la kodi yenyewe yaani VAT. Hii inaonesha jinsi mihimili hii hususan ule wa Bunge ulivyokosa japo weledi wa kurekebisha kosa la kijinga kama hili.

This is a proof beyond reasonable doubt kwamba Bunge letu haliko makini na mambo hufanywa kwa mtindo wa bora liende as long as limeletwa na Serikali hakuna wa kuhoji kwa umakini au kukosoa bila woga. Hii sio kuisaidia Serikali au nchi bali ni hujuma ya wazi.
Upo sawa mkuu, hapo kwenye jina lenyewe ndo wamechemka kabisa..
 
Huyo prof naye hajui. TRA wamesema mabenki yalikuwa yakusanya bila kulipa. Sio new makato. Mwee
Mabenk wanalipia kodi kila muamala tangu zaman na malipo hayo hufanyika kwa kila mwezi kile wanachoingiza kama faida huwa kinakipiwa serikali ilikurupuka ukikata na kwenye muamala means benk zitalipa kodi Mara mbili
 
.... Na mteja ambaye hii kodi ya VAT ndiye hasa inamhusu atalipa 1180 badala ya 1000 ya awali ambayo ilikuwa imesamehewa VAT. Huo ndio ukweli nyingine ni porojo tu. VAT ni kodi ya mlaji wala sio ya mfanyabiashara.
Hii iko vizuri; tunakula kwa kodi.
 
God bless you my learned brother. Laiti kama watawala wetu wangesoma na kuelewa madini uliyoweka hapa. Tusingefika hapa leo. Salute!
 
kitendo cha ile kodi kuiita VAT,Basi mzigo unaenda moja kwa moja kwa mlaji.Labda ibadilishwe jina na isiwe VAT.Profesa yuko sahihi.TATIZO HII NCHI KWA SASA MAAMUZI YA TULIOWAPA DHAMANA YANATOLEWA KWA HOFU YA KUTUMBULIWA.
mkuu pamoja na na kuwa mimi si mwana uchumi, bado naona kodi hii ikimrudia mtumiaji wa mwisho bila kujali itapewa jina gani. itahamishwa kwenda kwa wateja kupitia kupanda kwa gharama za uendeshaji na gharama za huduma zitapanda.
 
Uzuri namba tunaisoma wote bila kujali chama gani!!
 
mkuu pamoja na na kuwa mimi si mwana uchumi, bado naona kodi hii ikimrudia mtumiaji wa mwisho bila kujali itapewa jina gani. itahamishwa kwenda kwa wateja kupitia kupanda kwa gharama za uendeshaji na gharama za huduma zitapanda.
Wanachofanya wanasiasa ni kutuchezea akili,wataalamu (wana uchumi) kukubali kuweka proffession zao kando na kutumika kisiasa....Drama za Sukari ni udhibitisho tosha....
 
Mkuu mbona unasahau kuwa na hizi Benki zina gharama za uendeshaji? Mbona unasahau kuwa hizi Benki pia zinalipa 30% corporate tax? This is strictly business hivyo kuna haja ya pande zote kukaa chini na kutafuta suluhu.
 
Unakuwaje kamishna wa TRA afu unamislead umma juu ya kodi?na wote ktk taasisi mlioshiriki kutoa huo waraka na maelezo tuwaeleweje?
I suggest watu wawajibike hapa
Tuweke siasa pembeni mda mwingine
 
Back
Top Bottom