Gavana Prof. Ndulu: Benki wapo sahihi

Gavana Prof. Ndulu: Benki wapo sahihi

Gazeti la Mwananchi.Wakati TRA ikiitaka BOT izichukulie hatua bank zilizotangaza kuongeza gharama za huduma za kibenk,BOT imesema mabenk yapo sawa!Prof.Ndulu anasema mabenk watakuwa mawakala wa TRA tu katika kukusanya VAT lakini si walipaji,kwa hiyo hawezi kuwachukulia hatua.Beno Ndulu ametolea mfano unapokua unauza duka unakuwa wakala tu wa TRA na sio mlipaji.....KUMEKUCHA
Siamini habari hii..
 
Chukulia mfano mdogo tu,unadhani siment isingekuwa na VAT ungenunua 17000?jibu ni hapana ingekuwa pungufu,kwa hiyo na bank charges ni hivyo hivyo
 
Hahahahaha jana nilijua tunaingizwa chaka na T. R. A

Tangu lini V. A. T akalipa mfanya biashara. V. A. T ni consumption tax.

Nchi ya miujiza hiii. Tangu lini kuwe na double standards kwamba bank ndo zilipe VAT ila biashara zingine mteja ndo alipishwe.

Yani tumefikia pabaya sana kama taasisi kubwa hivi za kuaminika zinapishana kauli hadharani.
vilaza kila eneo tutafika? wasema ndiooooo wametufikisha hapa !
 
Siamini habari hii..
yani vijana wa Lumumba ni bure bure kabisa. Hata kama. mnalipwa buku mbili zenu msijitoe akili kiasi hiki.

Chukua smartphone yako unayotumia kupost humu. Google neno V. A. T. Soma definition ya VAT ndo ujue anatakiwa alipe mlaji au biashara.

Khaaaaaa am shamed to be a Tanzanian, Kama ndo wavivu wa kufikiri hivi. Yani asubuhi akili yako inatakiwa iwe active lakini umeamua utumie akili za usiku.

No wonder Kenya hatutakaa tuwapite na wataendelea kutudharau milele kama hizi ndo akili zetu.
 
Tra hakuna wajuvyi wa kodi, nafasi nyingi za kugaiana tu. Hata hio vat juu ya ada ni utumiaji mbovu wa vat. Sio kila mahala una toza vat.
Hii kwa uerfu ni valu added tax. Inatumika pale mlaji anapo nunua kitu. Hutumika zaidi kwenye bidhaa na sio kwenye services. Na hii ni kodi ambayo kuna wengine wapo excempted mfano diplomats . Hawa wanapo nunua kitu au service basi huomba refund...ni usumbufu sana ila tra hawajui ku plan mambo yao kwani wana ukosefu wa wataalam wa kububi hiw yo implement tax wanazo zitunga.
Na hili la bank vat haikupaswa kuwekwa kabisa , ndio kama lile la utaliii....
Gharama za kuweka fedha benki hazitakiwi ziwe juu . Ukiweka vat ni wazi banki wata ongeza juu ada zao kufidia ile iliokatwa na vat....hivyo gharama zinaenda kwa mteja.
Tukumbuke fedha zozote zinazo wekea bank tayari aidha ni income au revenue ya makampuni au mishahara ya wafanyakazi ambao wanapitishia fedha benki.
Hizi fedha sio product, hizi tayari ndani yake kuna vat ya tra , kuna stamp duty ya tra, kuna WHT ya tra pia kuna corporate tax ya tra...na kwa wafanya kazi ni net income baada ya kutoa payee. Kuzitoza kodi kwa njia yoyote ile hata kwa kuongezeka ada juu kutokana na kuanzishwa vat ya ada sio sawa kabisa kabisa..ni kodi haramu au kodi jipu
 
Zamani walikuwa hawatozwi na walikuwa wanatukata.. Basi wangeacha kukata.. Au wanataka walipe na zile zote za nyum?
Huyo prof naye hajui. TRA wamesema mabenki yalikuwa yakusanya bila kulipa. Sio new makato. Mwee

Hivi hii dhana ya kwamba eti zamani mabenki yalikua yanatukata VAT halafu hayawasilishi TRA imetoka wapi? Huu ni upotoshaji wa kiwango cha juu. Wangeikusanya kwa nguvu ya sheria ipi wakati sheria ya VAT ndio imefanyiwa marekebisho mwaka huu? Analosema Profesa ni sahihi kabisa. Serikali ilikosea kuiita hii kodi VAT kama walitaka mabenki ndio yalipe. VAT siku zote ni kodi inayolipwa na mlaji/mteja...hivyo ukishasema unatoza VAT jua moja kwa moja umembebesha mzigo mwananchi wa kawaida na sio mfanyabiashara/mtoa huduma.
 
Prof. Ndulu yuko sahihi!
Bongo kazi kweli yale makato walikua wanakata wananchi mabenki yalikuwa makusanyo yao au ilikuwa faida yao?
Ndullu alirakiwa alieleze kama ni sahihi benki zilikua zinakata hela uwakala wa ukusanyaji ulikuwa unafanywa na nani
 
Tuliwaambia mapema sana....Dr Mpango anataka kutumianguvu badala ya weledi wa finance! Sasa naona wanataka kuua mabenki! Watanzania wako makini zaidi kwenye romours kuliko hata facts! Sasa tunasubiri muafaka tuone go slow ya wananchi kuweka pesa bank! Wataweka wafanyakazi tu sababu zinapita huko! Ama la subirini anguko la mabenki!
 
Gazeti la Mwananchi.Wakati TRA ikiitaka BOT izichukulie hatua bank zilizotangaza kuongeza gharama za huduma za kibenk,BOT imesema mabenk yapo sawa!Prof.Ndulu anasema mabenk watakuwa mawakala wa TRA tu katika kukusanya VAT lakini si walipaji,kwa hiyo hawezi kuwachukulia hatua.Beno Ndulu ametolea mfano unapokua unauza duka unakuwa wakala tu wa TRA na sio mlipaji.....KUMEKUCHA
Huo ndio ukweli wenyewe hakuna lingine labda mabenki yasiwe VAT registered.
 
Kwa mujibu wa act ya Vat Ndulu yuko sahihi KIDATA anatakiwa kwenda ITA kupatiwa mafunzo ya Induction course ambayo ni ya lazima kwa kila mwajiriwa mpya wa TRA. Vinginevyo atashindwa kumshauri rais pia ni vyema akawatumia wasaidizi wake kabla hajatoa tamko lolote linalohitaji uelewa wa kodi. Yeye ni CEO tuu mengine afanye rejea kabla hajaongea huo ni ushauri tùu
 
Acha waisome namba ccm mbele kwa mbele
 
Back
Top Bottom