Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,787
30,083
GAUDENSIA KABAKA MWENYEKITI WA UWT?

Mwenyekiti wa UWT Gaudensia Kabaka ndiye aliyehusika kuwafukuza Waislam 11 Chuo Kikuu cha Dodoma na kusimamisha ujenzi wa msikiti hapo chuoni ambao ujenzi wake ulishaidhinishwa.

Leo yupo katika sherehe za kumuenzi Bi. Titi Mohamed.

Huyu ndiye kiongozi aliyewafukuza wajukuu wa Bi. Titi hapo chuoni na kuzuia ujenzi wa msikiti.

Kwa yale aliyopigania Bi. Titi Mohamed na wanawake wote katika TANU ya enzi zile huu ni msiba mkubwa.

Huyu Mama hastahili kuongoza wala kunasibishwa na umoja huu ulioasisiwa na mama zetu akina Bi. Titi, Bi. Hawa bint Maftah, Bi. Zarula bint Abdulrahman kwa kuwataja wachache.

Angalieni picha hiyo ya kwanza hapo chini pcha iliyopigwa na Mohamed Shebe ya mkutano wa TANU 1955 wakati wazee wetu wanautafuta uhuru wa Tanganyika.

Angalia huo umma Viwanja Vya Mnazi Mmoja na tazama hiyo sehemu nyeusi.

Hayo ni mabaibui ya bibi. mama, na shangazi zetu wamekuja kuujaza uwanja na kumtia nguvu Mwalimu Nyerere.

Mama zetu wameitika mwito wa "kuno kuno."

Hapo ndipo walipokuwa wakiimba nyimbo za lelemama kuhamasisha umma,
''Muheshimiwa nakupenda sana wallahi sina mwinginewe Insha Allah Mungu yupo Tanganyika tutajitawala.''

Tujitawale halafu iwe nini?
Gaudensia Kabaka anyanyase Waislam, Gaudensia avunje misikiti yetu?

Gaudensia Kabaka awafukuze chuoni wajukuu wa hawa wanawake unaowaona hapo chini kwenye picha?

Picha ya pili hao wote mbele hapo wanaongoza maandamano ya akina mama mimi mama zangu.

Hao ndiyo msingi wa UWT.

Yupo Bi. Mwamvua bint Mrisho (Mama Daisy), Bi. Titi Mohamed na Bi. Zainab Tewa.

Screenshot_20211023-213438_Facebook.jpg
 
Hili andiko limejaa chuki, unafiki na uchonganishi.

Huyu Ndugu muda wote yeye ni kuwazia dini yake tu.

Tumshukuru sana Mungu kumleta Mwalimu Nchi hii ingeangukia kwenye mikono la hii familia hakika ingekuwa ni majuto.
May Day,
Hivi unajua Nyerere kaja Dar es Salaam hana ndugu wala jamaa?

Unawajua waliompokea?

Unadhani endapo wazee wetu wamgekuwa wabaguzi wa dini au kabila Nyerere angefika hapo alipofika?

Wewe unaridhishwa na hii hali ya leo katika mgawanyo wa fursa 20:80?
 
UDOM ni taasisi isiyo na dini mkuu.
Hata wakristo hawaruhusiwi kujenga makanisa yao ndani ya eneo ya chuo.

Ni sehemu ya kupata elimu ya juu,si mahala pa kujenga madrasa Wala vyuo vya Biblia.

Kuna halls ambazo kwa utaratibu mzuri hutumika kuabudia.

Ndio ashapewa uongozi hivyo,,
Udini unakusumbua mzee.
Waislam mnateseka sana,acheni kulialia.
 
Kujenga na huku tunaboma haviwezi kutufikisha popote kama taifa.

Huu ungeweza kuwa na maans lakini sababu unachochea kuchukiana sababu ya mtendaji kuwa imani nyingine unaishia kuchochea Udini na kuharibu utaifa

Nadhani ifike mahala kiongozi anapokosea au kufanya maamuzi usiyoyapenda, yasiyokufurahisha, yasiyokua ya mrengo wako au tunapokosea au tunapofanya mabaya basi tutuhumiane kwa matendo yetu na sio kwa imani zetu
 
UDOM ni tasisi isiyo na dini mkuu.
Hata wakristo hawaruhusiwi kujenga makanisa yao ndani ya eneo ya chuo.

Ni sehemu ya kupata elimu ya juu,si mahala pa kujenga madrasa Wala vyuo vya Biblia.

Kuna halls ambazo kwa utaratibu mzuri hutumika kuabudia.

Ndio ashapewa uongozi hivyo,,
Udini unakusumbua mzee.
Waislam mnateseka sana,acheni kulialia.

✍✍✍✍✍✍👌
 
May Day,
Hivi unajua Nyerere kaja Dar es Salaam hana ndugu wala jamaa?

Unawajua waliompokea?

Unadhani endapo wazee wetu wamgekuwa wabaguzi wa dini au kabila Nyerere angefika hapo alipofika?

Wewe unaridhishwa na hii hali ya leo katika mgawanyo wa fursa 20:80?
Huwa unatengeneza picha mbaya sana ya Nyerere kama mtu aliyesaidiwa sana na waislamu alipokuja Dar es Salaam. Kumbuka kuwa Nyerere alikuja Dar es Salaama siyo kama ombaomba, bali alikuja akiwa na digrii ya M.A kama mwalimu wa St Francis College.

Kabla ya hapo alikuwa ameshafundisha St Mary's College huko Tabora (kwetu mimi na wewe); miaka hiyo ualimu ulikuwa ni kazi yenye hadhi sana. Asingejihusisha na siasa, Nyerere alikuwa ni mtu wa kuishi maisha mazuri tu wakati huo.

Mara zote unasema iwapo "wazee wetu" wa Dar es Salaama wasingemsaidia Nyerere lakini ulishasema wewe ni mtu wa Tabora, kwa hiyo uhusiano wako na watu wa dar es salaama ni dini zenu tu, na hapo ndipo tatizo lako lilipo.
 
Mzee Mohamed Said vipi leo uandishi wako umeelemewa na hasira, tumezowea kusoma simulizi zako za historia unazoziandika kwa utulivu mkubwa pasi kuonesha hasira hata siye ambao hatukuwapo kipindi hicho kina Bibi Titi tulipata darsa zuri la historia na kuliunganisha na zama zetu hizi za UDOM.
 
Fuma...
Mjadala huu unahitaji ujuzi.
Umeghadhibika unanitukana.
Kumradhi Mohamed Said, ni kweli nimeghadhibika sana na maelezo yako ya uzandiki na uchochezi kuhusu Bibi Titi, Gaudencia Kabaka na Suala la Msikiti pale UDOM!

Tunamwomba sana Mwenyezi Mungu kwamba kizazi chenye mawazo hasi na primitive kama wewe kiishe haraka katika Nchi yetu ili Taifa hili lije kupumua!

Wewe Mohamed Said ni mtu mdini , mwenye maarifa madogo sana na mwenye chuki iliyopitiliza dhidi ya Hayati Julius Kambarage Nyerere na harakati zake za kudai Uhuru wa Tanganyika.

Siku zote unataka wajinga wenzio wamwone Julius Nyerere kama mtu mshamba ambaye alifika Dar es Salaam hajui chochote na isingekuwa hao Wazee wako wa Kiislamu wa Dar es Salaam kumpokea asingekuwa chochote!

Unachosahau au ambacho hujui na hutaki kujifunza ni kwamba hata kabla ya kuja Dar es Salaam, Julius Kambarage Nyerere alikuwa ni kijana wa Chifu Burito wa Wazanaki kule Butiama na katika makuzi yake ya utoto alianza kupata hisia za uongozi kutoka kwa baba yake Chifu Burito na jinsi utawala wa kikoloni ulivyokuwa uki- operate!

Nadhani muda huo Wazee wako hao ambao mimi binafsi nawapenda na kuwaheshimu kwa mawazo yao na hawakuwa wadini na wajinga kama wewe hawakuwa na mikakati imara ya kudai Uhuru mpaka akina Dossa Azizi walipokutana na kijana mahiri na Mwalimu wa Sekondari ya St. Francis kama sikosei (Pugu Sekondari leo) Julius Kambarage Nyerere na wao kumtambulisha kwa Wazee wao.

Tambua kuwa muda huo Julius Nyerere alishatoka Makerere University Uganda, ameshasoma Tabora School ( Ambako pia nilisoma mimi Fumadilu Kalimanzila) na kuacha rekodi mbalimbali kama kijana shupavu na mwenye maono ya mbali kuhusu utawala wa kikoloni .

Wewe Said Mohamed hujui chochote zaidi ya kuokoteza "vistory" vya kwenye kahawa hapo Kariakoo na "tu- picha" twa zamani kutoka kwa familia za hao Wazee wa Kiislamu wa zamani hapo Mzizima na kuenezea UDINI WAKO!!!
 
Umeandika utumbo mtupu..
emoji706.png
hatushadadii udini ccm haina hayo makitu kaanayo huko huko kwenu.

#MaendeleoHayanaChama

UDOM ni taasisi isiyo na dini mkuu.
Hata wakristo hawaruhusiwi kujenga makanisa yao ndani ya eneo ya chuo.

Ni sehemu ya kupata elimu ya juu,si mahala pa kujenga madrasa Wala vyuo vya Biblia.

Kuna halls ambazo kwa utaratibu mzuri hutumika kuabudia.

Ndio ashapewa uongozi hivyo,,
Udini unakusumbua mzee.
Waislam mnateseka sana,acheni kulialia.
Saint,
Suala hili si la kujadiliwa na lugha za kejeli za "lialia."

Serikali inajua tatizo hili na iko kimya.

Kwa sababu maalum.

Soma historia ya uhuru wa Tanganyika kuna mengi utajifunza.

Ndipo unaweza ukawa na maarifa ya kukusaidia kujadili.
 
Mzee Mohamed Said vipi leo uandishi wako umeelemewa na hasira, tumezowea kusoma simulizi zako za historia unazoziandika kwa utulivu mkubwa pasi kuonesha hasira hata siye ambao hatukuwapo kipindi hicho kina Bibi Titi tulipata darsa zuri la historia na kuliunganisha na zama zetu hizi za UDOM.
Bagamoyo,
Anaeudhiwa asiudhike huyo ni sawasawa na punda.
 
Kumradhi Mohamed Said, ni kweli nimeghadhibika sana na maelezo yako ya uzandiki na uchochezi kuhusu Bibi Titi, Gaudencia Kabaka na Suala la Msikiti pale UDOM...
Fuma...
Mimi nisiyejua chochote nazungumza na mjuzi lakini huyu mjuzi anashindwa kutambua ukweli kuwa yapo malalamiko ya kweli.

Fanya utafiti kidogo kisha In Shaa Allah rejea tufanye mjadala:

PUBLICATIONS/RESEARCH PAPERS/ARTICLES

The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.

The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi, 2006

Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi.

Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York.

Uamuzi wa Busara, Abantu Publications 2008, Dar es Salaam.

Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No. 1, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam.

Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No.2, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam

Dar es Salaam na Wazalendo Wake Mashujaa Katika Kupigani Uhuru wa Tanganyika Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaaam

Watu Mashuhuri Katika Kuulingania Uislam Tanzania, Sheikh Ilunga, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam

Dola, Kanisa na Tatizo la Udini Tanzania, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam

The School Trip to Zanzibar, Africa Proper Education Network 2020, Dar es Salaam

Rajabu Ibrahim Kirama, Jemadari wa Vita Kuwa Jemadari wa Uislam, Readit, 2020, Dar es Salaam

In Praise of Ancestors (1987) Africa Events (London).

Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London).

Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)

The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).

Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam).

The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).

Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).

Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).

Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11th April 2004).

Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006).

Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, Nairobi.

Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa (AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg.

Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi.

Awards: Several Awards

Visiting Scholar: (2011)

University of Iowa, Iowa City, USA

Northwestern University, Chicago, Illinois, USA

Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.

OTHER COUNTRIES VISITED

Zambia, Ethiopia, Great Britain, Swaziland, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia, Sudan, Egypt, Saudi Arabia, United Arab Emirates, Oman, Yemen, Uganda, Switzerland, Iran, France, Netherlands, Turkey and Abu Dhabi.
 
Una udini balaa na unachofanya ni kujificha nyuma bibi Tit, nikukumbushe tu bibi Tit hakuwa anapigania udini Bali uhuru
Hawezi akaliona hilo..tayari kawa brainwashed..ni mwambie tu Tanzania kamwe haiwezi yumbishwa ni hoja mfu kama hizi.

#MaendeleoHayanaChama
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom