View attachment 258694
Hahaha bila shaka ni hii kitu, imetusumbua sana miaka hiyo...ukiiona tu ni mbio
GARI LA WANYONYA DAMU
Kijijini kwetu ilikuwa balaa. Siku mmoja padri alisimamisha land rover katika msitu kuwapa lifti kinamama walikuwa na mizigo ya mapeasi walikimbia vibaya sana chini ya gema la barabara kwa woga, sijui kipi kilisalimika kati ya viungo vyao na mapeasi. Mzungu alisikitika sana. Binafsi niliamini huo uvumi enzi hizo lakini walipomtuhumu baba yangu kuwa ananyonya damu kwa kuwa tu ameweka rangi nyekundu kwenye sakafu nikaachana na huo upuuzi japo nilikuwa shule ya msingi. Eti Mumiani...
Enzi hizo niko Mabawa Primary Schook Tanga ilikuwa ni shida kwa kweli
Hahaha dah kitambo sana .... Ila mi hilo gari sijawahi kuliona kusema kweli , alafu nilikuwa napenda sana lukopa bajia za mwalimu wa somo la historia
nakumbuka enzi hizo simu ndo za mkononi ndo zinaingia ...kujaza vocha ni kwa dola tu..unajaza dola..!!simu nyenyewe Siemens dole gumba..
Yaani weewee tunaenda mashine za misufin pale ukikuta Land rover ya Kalalambe yule nusu nusu umwage unga duuuu
Hivi ni kweli yule Mzee Kalalambe alikua ananyonya damu?! Umenikumbusha mbali sana mkuu enzi hizo nasoma Bungo Primary school.