Gari ya nyonya damu kwa waliosoma miaka ya 90

Gari ya nyonya damu kwa waliosoma miaka ya 90

Fukara

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2013
Posts
1,624
Reaction score
931
Wasalaam wanaJF

Jana nilikuwa nikiangalia kovu nilipoumia kwa kuanguka nilipokuwa shule ya msingi, baada ya wenzangu kusema gari ya nyonya damu inakuja watoto wengi tukakimbia ,mimi na baadhi ya watoto tukaanguka wengi tukaumia.

Wenzangu wa miaka hiyo mnakumbuka hii kasumba?Ila mpaka tunamaliza darasa la saba hatuja wahi kuona gari hiyo ya nyonya damu...wewe unakumbuka nini miaka hiyo ya old is gold?

Wenzangu mnaikumbuka hii?
 
Kipindi hicho nilikuwa mdogo hivi kijijini huko,

kwa kuwa sijawahi kuliona basi nikisikia gari ya nyonya damu najenga picha ya zile gari za ambulance hasa na ile alama + nyekundu,
Basi ilikuwa ni tabu tupu hasa nikitumwa mafuta ya taa na kibiriti dukani na bibi yangu jioni jioni hivi.
 
Umenikumbusha mbali aise utotoni tushatoka nduki sana tukiona combination alafu dereva mzungu, mpaka mmoja wetu alingoka meno kwa sababu ya kukimbia
 
Kipindi hicho nilikuwa mdogo hivi kijijini huko,

kwa kuwa sijawahi kuliona basi nikisikia gari ya nyonya damu najenga picha ya zile gari za ambulance hasa na ile alama + nyekundu,
Basi ilikuwa ni tabu tupu hasa nikitumwa mafuta ya taa na kibiriti dukani na bibi yangu jioni jioni hivi.

dah back in a days...
 
kitu cha combi nyekundu wanakuja ukikimbia wanakumulika na kioo chao unapata kizunguzungu unadondoka duh...kweli kipindi kile uongo ulikuwa unapangiliwa

mm nilikuwa najua gari ya ambulance ndo nyonya damu.
 
Na wachuna ngozi.

Jamani!!!!

Eti wanaenda kutengenezea dawa!!!
 
mm nilikuwa najua gari ya ambulance ndo nyonya damu.

umo umo story zenyewe zilikuwa zinabadilika siku bada ya siku kama zilivyo za dengue na panya road....ila siku hizi shule za msingi hata raha hakuna.. nakumbuka miaka hiyo alitoroka ng`ombe kichaa vingunguti basi ile tunaenda class kwa mstari tukitokea mstarini duh ilikuwa bonge ya patashika......

tulikuwa na ticha mkuu nyoko kweli na yeye akakimbia mziki wa huyo ng`ombe basi tulifurahi saana yaaani ni zaidi ya miaka kama 19 ila kila tunapokutana na wadau story ya kwanza ni ya ng`ombe....eti siku hizi mwalimu ana m-hug mwanafunzi khaaa
 
hii kitu ilikua ni uzushi tu pamoja nilikua nakimbia nikisikia ila cjawai liona hilo gari....
 
umo umo story zenyewe zilikuwa zinabadilika siku bada ya siku kama zilivyo za dengue na panya road....ila siku hizi shule za msingi hata raha hakuna.. nakumbuka miaka hiyo alitoroka ng`ombe kichaa vingunguti basi ile tunaenda class kwa mstari tukitokea mstarini duh ilikuwa bonge ya patashika......

tulikuwa na ticha mkuu nyoko kweli na yeye akakimbia mziki wa huyo ng`ombe basi tulifurahi saana yaaani ni zaidi ya miaka kama 19 ila kila tunapokutana na wadau story ya kwanza ni ya ng`ombe....eti siku hizi mwalimu ana m-hug mwanafunzi khaaa

BRN imeharibu utamu kabisa zamani ilikuwa balaa mwalimu akifa tunashukuru
 
Wakati tuko form one umeme ukikatika usiku mnaamshwa na kuambia mchukue ndoo mkalete umeme
 
acha acha acha kabisa kuna ticha mpaka leo tunasalimiana ila sitaki mazoea nae mixer najishtukia nahisi sijachomekea shati acha kabisa

hahahahaha alikuwa mwalimu wa hesabu nini
 
umo umo story zenyewe zilikuwa zinabadilika siku bada ya siku kama zilivyo za dengue na panya road....ila siku hizi shule za msingi hata raha hakuna.. nakumbuka miaka hiyo alitoroka ng`ombe kichaa vingunguti basi ile tunaenda class kwa mstari tukitokea mstarini duh ilikuwa bonge ya patashika...... tulikuwa na ticha mkuu nyoko kweli na yeye akakimbia mziki wa huyo ng`ombe basi tulifurahi saana yaaani ni zaidi ya miaka kama 19 ila kila tunapokutana na wadau story ya kwanza ni ya ng`ombe....eti siku hizi mwalimu ana m-hug mwanafunzi khaaa
Walimu wote wamepita jkt,

Mkifanya kosa wanafunzi, shule inageuka depo angalau kwa nusu saa.

Mnaruhusiwa SAA sita home mnalipoti saa kumi.
Sababu moja wapo ni kukimbilia vichakani kuogopa chinjachinja.
 
Mkuu, siku moja tulienda training ya zima moto pale makao makuu mjini Dar-es salaam, katika mambo mengi waliyotufundisha ni pamoja na utaratibu wao wa kufanya kazi kwamba iwapo kuna tukio la dharura gari lao likiwa mbioni kwenda kwenye tukio ikitokea ukazubaa njiani wanaruhusiwa kukugonga na hakuna kesi,wewe unahesabika kama sehemu ya wahanga wa tukio husika.

Kutokana na mafunzo hayo ndo nikaelewa dhana nzima ya lugha ya magari ya nyonya damu. wazazi walikuwa wanajaribu kuwajengea watoto woga kwa magari hayo ili kuwaepusha kugongwa na kupoteza maisha.
 
Back
Top Bottom