Gari ya nyonya damu kwa waliosoma miaka ya 90

Gari ya nyonya damu kwa waliosoma miaka ya 90

kitu cha combi nyekundu wanakuja ukikimbia wanakumulika na kioo chao unapata kizunguzungu unadondoka duh...kweli kipindi kile uongo ulikuwa unapangiliwa

nakumbuka hii kitu. nakumbuka kuna siku walitaka kuja shuleni kwetu sasa wale wa kubwa wa shule walibeba majembe,kwanja ili wawapige hao nyonya damu.tulikimbia sana
 
Dah. Kumbe nastahili kuitwa Babu... Miaka ya tisini tayari nipo kwenye ajira!!!
 
Fukara

Dah, mkuu umenikumbusha pia, tulikuwa tunakimbia hovyo aisee.
Walikuwa wanasema wanyonya damu wanakioo chao kikikumulika tu wanakuvuta.
 
Last edited by a moderator:
Mim wa mjini mambo hayo wala sikuyasikia kabisa ndiyo kwanza nayaskia hapa!
 
Dah, mkuu umenikumbusha pia, tulikuwa tunakimbia hovyo aisee.
Walikuwa wanasema wanyonya damu wanakioo chao kikikumulika tu wanakuvuta.

tulio umiaga kwa kuwa kimbia hawa watu inabidi tudai fidia asee..
 
Walikuwepo kabisa hawa watu tena wakikuta uko peke yako wana kudaka wakikutoa damu ukifa wanakupiga chata na kuna kua hamna case.
Damu inapelekwa mahospitalini huko.

Wanapinga ila hawajafuatilia kwa undani walikuwa na vibali hata ukifa hamna kesi!! siyo lazma waamini ila ukweli ndiyo huo!
 
Fukara

Nilikuwa nipo Darasa la Pili Pale Shule ya msingi Sinza Miogoni.
 
Last edited by a moderator:
Mh! kunavingi vyakukumbuka utoto haswa shuleni unaweza taman kurudi nyuma
 
Nakumbuka enzi hizo bado niko kijijini mwaka 1991 tuko kichakani tunachanja kuni na wenzangu ikatokea helicopter ikatupita kwa juu ikiwa karibu sana tulikimbia vibaya mno maana ndio mara ya kwanza helicopter kuiona au kupita kijijini kwetu.

Basi yule rubani kutuona tunatoka mbia akaamua kutuelekezea kwetu kwa kugeuka maana alituona washamba tulikuwa tunajigonga kwenye mawe kama vile the gods must be crazy. Nina kovu kwenye paja hadi leo sitasahau kipindi kile maana kama tulikuwa kama jambazi anikimbia helicopter ya polisi
.
umenichekesha sana mkuuivi zamani sijui palikua na nn
 
si mchezo nilikuwa nakumbuka uji wa mchele, pia nilikuwa nabeba kidumu cha maji kwa ajili ya kumwagilia Maua

hahaha mbolea na kuni vilihusika sana hapo...mlikuwa mnatumia vicheti au
 
Fukara

ha ha haaa, tulikuwa tunatishana kuhusu gari la nyonya damu na wanafunzi wa Tambaza
 
Last edited by a moderator:
Hii inshu ya damu kweli ilikuwepo mana hospital zilikuwa na uhaba wa damu kutokana na mwamko mdogo wa watu kuchangia damu miaka iyo ..serikali iliweka baadhi ya watu kusolve hilo tatizo ambapo hata itokee mtu kanyonywa damu kesi inakuwa haina nguvu but kwa sasa mambo ya kunyonyana damu hayapo mana magonjwa ya zinaa mengi kama ukimwi ndo usiseme hali ni tete kila mtu mgonjwa ckuhzi

Hii issue ilikuwa kubwa na ilikuwa inasemekana kuwa kulikuwa na majeruhi wengi (Wanajeshi) wetu waliokuwa wakipigana vita Mozambique na baadae vita ya Uganda na walikuwa na uhitaji mkubwa wa damu,

Mumiani ilikuwa ni balaa, shule nzima ilikuwa inatawanyika, na ilikuwa inasemekana wakikunyonya wanakupiga muhuri kwenye kwapa na polisi wakiokota maiti cha kwanza ni kufungua kwapa na wakikuta muhuri tu hakuna kesi hapo
 
Nakumbuka enzi zile panic ya nyonya damu shule ni taharuki.
 
Dah...tulikuwa tunaingiwa na hofu sana tukiona gari la wagonjwa tulikuwa tunawaita muumiani au nyonya damu,asante mkuu kwa kunirudisha nyuma na kukumbuka zile nyakati zetu....
 
Daaah, kitambo sana, umenikumbusha Darajani primary school baadae ikajulikana kama Gilman Rutihinda.!

Kumbukumbu nzuri sana hizi.
 
Back
Top Bottom