Gari ya nyonya damu kwa waliosoma miaka ya 90

Gari ya nyonya damu kwa waliosoma miaka ya 90

Kijiji nilichokulia,wanafunzi tukiwa bado tuna wenge LA nyonya damu,chinja chinja,chuna ngozi,ikaibuka story nyingine kabsaa ambayo mpaka Leo nikikumbuka huwa sins uhakika kama ni kweli au LA,na kama ni uongo mtunzi alijipanga.

Kwanza nakumbuka zikaanza tetesi kuwa kwenye mpaka unaotenganisha kijiji chenye shule tunayosoma na kijiji tunachoishi kuna nyoka mkubwa sana mweusi anaishi kwenye mbuyu mkubwa uliopo eneo hilo.yeye anasuhiri tu upite peke yako anakimbia na ncha ndogo ya mkia mwili wote anausimamisha kivizia kichwa huku anakukimbiza.tukachoka.

Sasa dogo mmoja akaja kutupa mkasa kuwa akiwa anatoka kusaga kijiji cha shule na baiskeli anarudi home,Hamadi!!!!machine inachomoza vichakani sababu baiskeli ulikuwa moto akafanikiwa kulipita,likaanza kumfuata nyuma speed.dogo kasimamia ukucha baiskeli wapi dude linamkaribia tu.akaona isiwe tabu.

Anasema kulikuwa na dimbwi kubwa LA maji barabarani akatupa baiskeli akachumpa ndani ya maji na kuzamia humo,kakaa sekunde kazaa mpaka pumzi zikaisha akaona aibuke kucheki msala.akakuta jembe limemsamehe limeondoka. Akaokota baiskeli yake huku unga wote umelowa.na kurudi home huku anatetemeka.du yaani kuanzia hapo tukawa tunasubiriana wote ndio tunarudi na magongo in case jamaa akitokea.

Nakumbuka mengi mazuri ya wakati ule.
 
kipindi kile unaanza kuchezea viboko home na mshua vya kukuamsha,
ukifika shule unachezea vya namba(mstarini)
ukiingia class unakula vya speed test, kutokukusanya daftari na makosa mengineyo
ukitoka mapunziko unakutana navyo vya kuchomolea shati
ukirudi home unacheza sana njiani ukirudi home unaenda kulala then mshua anarudi anakuamsha unachezea vya kutokuoga na kwa nini hujafua soksi ilikuwa niburudani tupu..

......siku hizi nasikia watoto wakichapwa fimbo mbili wanadondoka mashetani si usgneee huu

dah mkuu umenikumbusha mbali kuna mwalimu wetu alikkuwa anaitwa abduh uyo nishamuombea sana afe alikuwa nuksi.
 
Hizo zilikuwa mbinu za watoro kusudi wote tukimbie shule, kwa sababu sikuwahi kuona hiyo gari lakini nimekimbia kila ikizushwa manyonya damu.

sisi watoro walikuwa wanaitwa CHIMBO AU NDELA
 
watoto wa digitali ngoja tujifunze historia tu apa
 
miaka ya 80 ilikuwepo pia?

Kuna baadhi ya njia za vumbi tulikuwa hatupiti ie msitu wa CCP moshi hasa baada ya saa 12,na mto kama karanga ukienda kucheza,kulikuwepo na chunusi mnyonya damu baadhi ya maeneo ya mto
 
Nakumbuka enzi hizo bado niko kijijini mwaka 1991 tuko kichakani tunachanja kuni na wenzangu ikatokea helicopter ikatupita kwa juu ikiwa karibu sana tulikimbia vibaya mno maana ndio mara ya kwanza helicopter kuiona au kupita kijijini kwetu.

Basi yule rubani kutuona tunatoka mbia akaamua kutuelekezea kwetu kwa kugeuka maana alituona washamba tulikuwa tunajigonga kwenye mawe kama vile the gods must be crazy. Nina kovu kwenye paja hadi leo sitasahau kipindi kile maana kama tulikuwa kama jambazi anikimbia helicopter ya polisi
 
Great memories.
Long time kitambo.
Ukisikia hayo mambo unakimbia kwa speed ya kisigino kugusa chogo
 
Kule Rukwa sina hakika ni wilaya gani kuna Padre alikuwa anakwenda kuongoza ibada kijiji kimoja, kwa bahati mbaya gari lake likapata hitilafu njiani, akapata lift ya gari la red cross wakampeleka mpaka alikotakiwa kuongoza ibada, waumini walikuwa wakimsubiri kanisani na mara wakaona gari la red cross linaingia,

ndipo wote walipotimua mbiyo kujinusuru wakijua nyonya damu wameingia kwa mbinu mpya, hata walipobembelezwa kuwa padre alipewa lifti hawakukubali wakaishia ....sina kumbukumbu hatima yake ilikuwaje mliopata kusikia huu mkasa miaka hiyo mwaweza kuihariri hii post
 
Nakumbuka enzi za wachuna ngozi

Kuna mkanda(VHS) walirekod waliokamatwa na ngozi

Wote walikuwa wamevaa shati zinachata ya Nike na Fila

Toka siku hiyo tulikuwa tukiona MTU kavaa shat ya nike au fila tunatoka baruti tukijua ni mchuna ngozi..

Duuu..maisha ya zaman ni noumaaaa
 
kitu cha combi nyekundu wanakuja ukikimbia wanakumulika na kioo chao unapata kizunguzungu unadondoka duh...kweli kipindi kile uongo ulikuwa unapangiliwa

sanaa
aiseeee mi nishaambiwaga na kaka zangu eti wamekimbizwa na nyonya damu
 
Mkuu unanikumbusha mbali kipindi icho tulikua tunaambiwa ukikutana na manyonya damu yakikunyonya damu basi yanakubakishia damu ambayo itakufikisha mpaka nyumbani.. so kama yalikukadiria nusu saa kufika home ukikimbia sana ukawahi before 30minutes ukifika home inatakiwa unywe chai birika zima bila ya sukari ndo utapona.

hahahahahahaha aiseee.....
 
Nakumbuka enzi hizo bado niko kijijini mwaka 1991 tuko kichakani tunachanja kuni na wenzangu ikatokea helicopter ikatupita kwa juu ikiwa karibu sana tulikimbia vibaya mno maana ndio mara ya kwanza helicopter kuiona au kupita kijijini kwetu.

Basi yule rubani kutuona tunatoka mbia akaamua kutuelekezea kwetu kwa kugeuka maana alituona washamba tulikuwa tunajigonga kwenye mawe kama vile the gods must be crazy. Nina kovu kwenye paja hadi leo sitasahau kipindi kile maana kama tulikuwa kama jambazi anikimbia helicopter ya polisi
hahahahah this is not fair
i have to screenshot this

hahahahahahahahaha aiseeeee mkuu nimecheka hadi mkojo
 
Huu ujinga wa wanyonya damu almanusura uvunje miguu ya watu...
 
Back
Top Bottom