Gari ya nyonya damu kwa waliosoma miaka ya 90

hahahahaha alikuwa mwalimu wa hesabu nini

huyo huyo huyo mdau umesoma kaloleni primary Arusha nini kuna boya alikuwa pale ule msimu wa kutufundisha tebo ni bora ujikate na wembe then umuombe unaenda nje kunawa ila akiingia hakuna kutoka mtu kama kunya kunya darasani mdau ilikuwa mabanzi, makofi, fimbo tunachezeshewa kama mahabusu vile though mpaka leo tebo inanizingua
 
Walimu wote wamepita jkt,

Mkifanya kosa wanafunzi, shule inageuka depo angalau kwa nusu saa.

Mnaruhusiwa SAA sita home mnalipoti saa kumi.
Sababu moja wapo ni kukimbilia vichakani kuogopa chinjachinja.

chinjachnja ilikuwa balaa sometimes nagoma keda shule mama anakomali hata kwa bakora..mzee naenda chimbo aka ndela.
 
huyo huyo huyo mdau umesoma kaloleni primary Arusha nini kuna boya alikuwa pale ule msimu wa kutufundisha tebo ni bora ujikate na wembe then umuombe unaenda nje kunawa ila akiingia hakuna kutoka mtu kama kunya kunya darasani mdau ilikuwa mabanzi, makofi, fimbo tunachezeshewa kama mahabusu vile though mpaka leo tebo inanizingua

hapana mkuu sijasoma hapo.siunajua walimu wengi wakali ni wahesabu...
 
Mimi niliyesoma shamba sijui gari la nyonya damu,kwanza miaka ile kwetu kuona gari labda mara moja kwa mwezi au uamke asubuhi mapema sana saa 11 ndio utakutana na gari la abiria enzi hizo Toyota lenye uwazi nyuma.

Ila nakumbuka kulikuwa kukipita gari la Jeifung (Jeifungo) Tulikuwa tu tukikimbia sana maana tulikuwa tukisikia kuwa linabeba watoto na kuwaiba.
 
Walimu wote wamepita jkt,

Mkifanya kosa wanafunzi, shule inageuka depo angalau kwa nusu saa.

Mnaruhusiwa SAA sita home mnalipoti saa kumi.
Sababu moja wapo ni kukimbilia vichakani kuogopa chinjachinja.

kipindi kile unaanza kuchezea viboko home na mshua vya kukuamsha,
ukifika shule unachezea vya namba(mstarini)
ukiingia class unakula vya speed test, kutokukusanya daftari na makosa mengineyo
ukitoka mapunziko unakutana navyo vya kuchomolea shati
ukirudi home unacheza sana njiani ukirudi home unaenda kulala then mshua anarudi anakuamsha unachezea vya kutokuoga na kwa nini hujafua soksi ilikuwa niburudani tupu..

......siku hizi nasikia watoto wakichapwa fimbo mbili wanadondoka mashetani si usgneee huu
 
nikikumbuka kipindi hicho mpaka sasa na hali fulani ya uoga huwa inaniingia,sipendi kukumbuka kipindi hicho nilipata tabu sana hasa nikikumbuka maeneo niliyo kuwa napita kila siu wakati wakutoka shule,mpaka sasa hayo maeneo huwa nikifika kuanahali yauwoga huwainaniijia..kipindii hicho tulikuwa tunaambiwa ndo mahali ikifika saa sita mchana wanyonya damu huwavizia watu na kuwa kamata
 
dah utoto ujinga kweli..lkn ukiangalia uwoga ulitusaidia mambo mengi sana
 
Hizo zilikuwa mbinu za watoro kusudi wote tukimbie shule, kwa sababu sikuwahi kuona hiyo gari lakini nimekimbia kila ikizushwa manyonya damu.
 
nakumbuka enzi hizo simu ndo za mkononi ndo zinaingia ...kujaza vocha ni kwa dola tu..unajaza dola..!!simu nyenyewe Siemens dole gumba..
 
Tuliambiwa unakamatwa unawekwa kwenye kiti sindano inakuchoma automatic damu inaisha, kumbe walikuwa wanataka wanafunzi watokapo shuleni wawahi kurudi nyumbani wazazi wawatume. Siku hizi ukiwaambia watoto hivyo wanaweza kukibia bastora yako wakawalipue.
 
Mkuu unanikumbusha mbali kipindi icho tulikua tunaambiwa ukikutana na manyonya damu yakikunyonya damu basi yanakubakishia damu ambayo itakufikisha mpaka nyumbani.. so kama yalikukadiria nusu saa kufika home ukikimbia sana ukawahi before 30minutes ukifika home inatakiwa unywe chai birika zima bila ya sukari ndo utapona.
 
alaf kwann wazaz walikuwa hawatuambii ukweli kuhusu ili?
 
Tuliambiwa unakamatwa unawekwa kwenye kiti sindano inakuchoma automatic damu inaisha, kumbe walikuwa wanataka wanafunzi watokapo shuleni wawahi kurudi nyumbani wazazi wawatume. Siku hizi ukiwaambia watoto hivyo wanaweza kukibia bastora yako wakawalipue.

alaf wazazi ndo mana ealikuwa hawatuweki wazi..nilikuwa namuliza sana mama kuhusu nyonya damu anasema ukitoka shule sa 8 wai kurudi.
 
Uwongo huo ulivuma shuleni kwetu ijumaa gari la padre linakatiza tu shuleni watu kusikia tu inanguruma mbona hamna aliyebaki darasani
 
Back
Top Bottom