Gari Moshi (Train) zaanza safari jijini Dar es Salaam!

Status
Not open for further replies.
..Mkuu nina wasiwasi kama kweli foleni itapungua kama tunavyofikiria. Baadhi ya watanzania tuna kasumba ya kuona ufahari kuzunguka mjini wakiwa na magari yao. Kwa hiyo mswahili kuacha gari yake nyumbani akapande treni mh!!... Huenda ikatumika tu kwetu sisi tusiokuwa na magari.
Kwanza packing za mjini zitapand kwahiyo ukienda na gari lako andaa pesa ya packing mimi napendekeza iwe sh 20,000 per 30min
 
Hili linahitaji pongezi za hali ya juu... Hopefully Mwakyembe kajipanga vema na huu ni mwanzo tu wa hio huduma ya treni kushamiri nchini, hasa jiji la Dar lenye msongamano wa transportation.

Ila itakuwa vema kama kwenye vituo vya hizo treni kukajengwa parking lot kubwa kwa maana kuwa si lazima niende na gari mpaka mjini, ila gari litanisogeza mpaka kwenye kituo cha karibu cha treni.
 
Afadhali umenisaidia hiyo picha ipo Michuzi na imepigwa jana wakati wakitest route hiyo.

Leo Ubungo maziwa asubuhi nimeona wanaendelea na kuweka vizuri mataruma ya reli,huyu jamaa sijui ana maana gani kuleta uzi wa uongo hapa JF.Treni bado haijaanza kufanya kazi.
 
Nadhani hapa hapa Bongo? Hilo parking lot haiwezi kuwa kihenge cha wezi waking'amua hilo? Labda kwa malengo ya ku park mda mfupi. Na eneo la stesheni muhimu. Ila tu mie bado sijajua hilo treni linapita wapi kuenda wapi na route yake ni ipi hasa.
 
Sina uhakika kama treni zimeanza kazi leo siwezi kubisha ila hiyo picha sio ya leo ni uongo ni ya ijumaa wakati treni ya Tazara ilipofanya majaribio
 
Nilisikia Ubungo Maziwa na kuelekea tabata kisha stesheni. Sijui nauli ikoje, sijui vituo vikoje, sijui muda wa treni ukoje,sijui lolote mpaka nikaonane na TRL wanipe habari labda.

Basi tutoke tunakotoka kwa Bajaj maana itakuwa ngumu sana kutumia treni kama unakaa mbali na kituo, ilihali una usafiri wa gari.
 
Hata mimi napenda kujua inaanzia wapi na kupitia maeneo gani!
Je ina kituo humo katikati, au ikitoka ndo basi hadi kurasini?

Vinginevyo hii itasaidia sana kuongeza ufanisi makazini maana watu watawahi kufika, na kurudi majumbani kwa muda!
Tuombe Mungu iwe sustainable!


Mwakyembe onyesha njia.
 

Attachments

  • Treni.png
    Treni.png
    101 KB · Views: 99
Tukiacha siasa tukawa watekelezaji, hii nchi tutaibadili chini ya miaka mitano ikawa one of the best economies in Africa.

This will remain a pipe dream as long as DHAIFU is still in control!!
 
Angalau wamejaribu! Hongera Mh Dr Mwakyembe pamoja na team yako. Watanzania wamechoshwa na porojo wanataka kuona results.
 
Do we know the price per trip? Is it possible to buy a day or a week travel card ?Msaada tutani tafadhali
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom