Gari Moshi (Train) zaanza safari jijini Dar es Salaam!

Gari Moshi (Train) zaanza safari jijini Dar es Salaam!

Status
Not open for further replies.

thatha

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2011
Posts
15,340
Reaction score
1,573
Leo tarehe 01 octoba 2012, nimefrahi sanaa kuona mabadiliko ya dhati ktk taifa letu katika sekta ya usafiri jijini Dar. Juzi tuliskia majaribio ya treni kutoka maeneo ya ubungo mpaka tktt ya jiji, jana tukaskia project kubwa ya mabasi yaendayo kasi katika jiji la Dar es salam.

Leo tumeona na tunashuhudia uzinduzi wa safari mpaya za treni ambazo zitapita kandokando ya jiji mpaka kurasini.. Mwakyembe ameonyesha njia.

Hii ni picha ya treni ikiwa na abiria leo asubuhi jijini Dsm


.
69189_10151909225210931_1608798866_n.jpg
 
Ni hatua nzuri sana,tunahitaji usimamizi imara ili zisife
 
naomba msaada nijue route ni kwenda wapi na wapi???
Hata mimi napenda kujua inaanzia wapi na kupitia maeneo gani!
Je ina kituo humo katikati, au ikitoka ndo basi hadi kurasini?

Vinginevyo hii itasaidia sana kuongeza ufanisi makazini maana watu watawahi kufika, na kurudi majumbani kwa muda!
Tuombe Mungu iwe sustainable!
 
naomba msaada nijue route ni kwenda wapi na wapi???

Yeah,,binafsi nia shaka sana na efficiency yake ktk mukhtada wa kupunguza foleni,train inapita pembeni tu ambako hakunaga msongamano lets wait and seee
 
Mabehewa yale yale ya kwenda bara?? Wameandaa miundombinu ya vituo na sehemu ya kukatia tiketi?? Madeleva wa daladala na boda boda sasa wawe waangalifu kwenye junction ya barabara na reli ili kuepuka ajali.

Big up Mwakyembe lakini uwe unakwenda Appolo for checks up
 
hiyo ndio tz tunayoitaka.
Laiti mambo yangekuwa hivi siku zote tungefika mbali.
 
Duuu! Kweli Maendeleo yanaletwa na wananchi wenye nia. Mafisadi aibu tupu na mabasi yao. Kelele za nauli sasa watakoma ubishi.
 
naomba msaada nijue route ni kwenda wapi na wapi???

Kibamba kupitia ubungo hadi katikati ya jiji na maeneo ya chanika,kisarawe,jeti rumo reli hadi katikati ya jiji/kurasini
 
Hatua nzuri sana hii. Nampongeza mwakyembe kwa kuamsha reli hizi zilizokuwa zimesahaulika.
 
Mwanzo Mzuri......tuwe makini na uendeshaji wake sasa.Tuchukue taadhari katika makutano ya barabara isije leta maafa. Tusije sikia siku imeishiwa mafuta siku za mbeleni.Otherwise Good attempt
 
Hii ni hatua ya kupongezwa!!!! Nina uhakika hii route sio ya Ubungo kwani hapa Ubungo sijaiona treni ikipita mitaa hii.

Tiba
 
mkuu hiyo ndiyo route yake kweli, umeanzisha thread nzuri usiiharibu mwenyewe kwa kuingiza masihara. kibamba kuna reli kituo wapi?..........
Kibamba kupitia ubungo hadi katikati ya jiji na maeneo ya chanika,kisarawe,jeti rumo reli hadi katikati ya jiji/kurasini.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom