Fursa za biashara kwa kila mkoa hapa nchini

Fursa za biashara kwa kila mkoa hapa nchini

Ni kweli ila kupenyeza dar lazima kichwa kiume, kama hauna mtaji was kutosha. Ndo maana MTU akitajirika sana mkoan hukimbilia dar kupanua zaidi biashara. Tofauti na startup kucompete na giants ni ngumu sana hasahasa kupata office space
Dar kuna fursa nyingi mnoo
 
Kama ni fani yako au unauwezo wa kuajiri wenye hizo fani kwenye mikoa yenye watu wengi;anzisha clinic za afya mfano meno,macho n.k kwa siku huwezi kukosa laki
 
Me natafuta sehemu nzuri ya kufungulia duka la vipodozi kwa mtaji wa 6mil dodoma.,ila tatzo mji cjaujua bado...
 
3.KIGOMA.
katika mkoa wa kigoma kuna fursa za kilimo biashara kwani ardhi bado iko chini kwa bei, Kigoma hulimwa mazao kama mahindi, maharage, .
hivyo biashara ya mazao hasa kupeleka nchi jirani kama Burundi kupitia mipaka ya munanila au nyamgali inafanyika sana, Lakini pia kuna biashara ya udaga yaani hii ni ile mihogo inayokaushwa ambayo huuzwa sana Burundi, Uganda na Rwanda ikitokea sana wilaya za kasulu na kibondo.
kukigoma shamba la hekali moja linauzwajena uvuvi pia ziwa tanganyika na mto malagarasi ambapo samaki wa mto malagarasi , kambale na kamongo huuzwa hadi tabora na mikoa mingine
kigoma pia kuna vitenge wax , delux, hitaget ambavyo huuzwa mikoa mingine kwa bei ya juu.
 
3.KIGOMA.
katika mkoa wa kigoma kuna fursa za kilimo biashara kwani ardhi bado iko chini kwa bei, Kigoma hulimwa mazao kama mahindi, maharage, .
hivyo biashara ya mazao hasa kupeleka nchi jirani kama Burundi kupitia mipaka ya munanila au nyamgali inafanyika sana, Lakini pia kuna biashara ya udaga yaani hii ni ile mihogo inayokaushwa ambayo huuzwa sana Burundi, Uganda na Rwanda ikitokea sana wilaya za kasulu na kibondo.
kukigoma shamba la hekali moja linauzwajna uvuvi pia ziwa tanganyika na mto malagarasi ambapo samaki wa mto malagarasi , kambale na kamongo huuzwa hadi tabora na mikoa mingine
kigoma pia kuna vitenge wax , delux, hitaget ambavyo huuzwa mikoa mingine kwa bei ya juu.
 
Yap naona vijana mmeamka sasa kutafuta fursaa na sio mnajikalia tu na kuwaweka wazaz hasar ya kuwalisha kila siku,anyway mi nko dodoma huku,fursa huku ni usafiri hasahasa Toyo,trip moja ya toyo sio chini ya 5000 sasa piga umepata trip 5 tu hapo unakuwa na 25000 per day kwa mwezi una 750,000 kwa miezi 10 una 7.5 mil hapo umekosa nnn,fursa ni mtazamo wako tu,karibuni
Dodoma upatikanaji wa matunda mtaani ni nadra sana. Au wenyeji hawatumii mi niliona ni fursa pia.
 
kama kichwa cha habari kinavyoeleza naanza kama ifuatavyo.
1.RUVUMA.
mkoani ruvuma kuna kilimo cha mazao ya biashara kama kahawa katika wilaya ya mbinga, soya na ufuta hulimwa namtumbo, kuna biashara ya mahindi kutoa songea kupeleka mikoa mingine kwani wanazalisha sana mahindi, lakini pia unaweza kupeleka bidhaa mbalimbali za madukani ukauwauzia wenye maduka,
Ruvuma pia bidhaa za mtumba kama viatu, nguo za kike, mashuka vinanunuliwa sana.
Ruvuma wana kilimo cha mpunga wa kumwagilia katika wilaya ya namtumbo hasa vijiji vya kitanda.

Kwa sasa hali ni mbaya sana hayo maeneo kwani wanategemea sana kilimo cha mahindi na ndio hayo wanayo yakutosha sana ndani hawana pakuuzia watu n hawana pesa kabisa debe moja la mahindi ni 1000
 
Hello wana JF, Hususan kwa wale mliopo mkoani Kilimanjaro, Nimefkiri na kutafakari njia rahisi ya kutukutanisha vijana na rika lingine hasa walio eneo moja kwa lengo la kuangazia fursa za kibiashara, masoko na fursa nyinginezo kama kuunda vikundi, kampuni au viwanda vidogo vidogo......

Hivyo nawakaribisha wote mliopo mkoani Kilimanjaro tushirikishane mengi hapa.........

Kwa kuanza utatueleza unapopatikana, biashara yako n fursa zilizopo pamoja na jinsi wengine wanaweza kuzifkia fursa hzo........ N. K katika kupambana na umaskini...

Karibuni wadau wote:
 
Back
Top Bottom