Fursa za biashara kwa kila mkoa hapa nchini

kama kichwa cha habari kinavyoeleza naanza kama ifuatavyo.
1.RUVUMA.
mkoani ruvuma kuna kilimo cha mazao ya biashara kama kahawa katika wilaya ya mbinga, soya na ufuta hulimwa namtumbo, kuna biashara ya mahindi kutoa songea kupeleka mikoa mingine kwani wanazalisha sana mahindi, lakini pia unaweza kupeleka bidhaa mbalimbali za madukani ukauwauzia wenye maduka,
Ruvuma pia bidhaa za mtumba kama viatu, nguo za kike, mashuka vinanunuliwa sana.
Ruvuma wana kilimo cha mpunga wa kumwagilia katika wilaya ya namtumbo hasa vijiji vya kitanda.
Korosho tunduru, alizeti, tangawizi madaba, dagaa nyasa
 
2.KATAVI.
mkoa huu almaarufu mpanda una fursa pia za kilimo cha mpunga, hasa maeneo jirani na kakese lakini pia kule maji moto , lakini pia unaweza kwenda kununua mpunga ukaweka stock ukauza bei ikipanda au unaweza kukoboa mchele na kuusafirisha hadi maeneo mengine ya nchi.
lakini katavi pia kuna shughuli za uchimbaji wa madini hasa dhahabu na wachimbaji wametawanyika maeneo mbali mbali kulingana na migodi midogo midogo ilipo.
kuna shughuli pia za utalii kwani kuna mbuga ya katavi katika mkoa huu kwa hiyo fura kwenye utalii unaweza kunufaika nazo.
 
wenyeji wa mikoa husika mtaongezea fursa zilizopo kwenu kwa sababu sitotaja zote nikamaliza.
 
3.KIGOMA.
katika mkoa wa kigoma kuna fursa za kilimo biashara kwani ardhi bado iko chini kwa bei, Kigoma hulimwa mazao kama mahindi, maharage, .
hivyo biashara ya mazao hasa kupeleka nchi jirani kama Burundi kupitia mipaka ya munanila au nyamgali inafanyika sana, Lakini pia kuna biashara ya udaga yaani hii ni ile mihogo inayokaushwa ambayo huuzwa sana Burundi, Uganda na Rwanda ikitokea sana wilaya za kasulu na kibondo.
kuna uvuvi pia ziwa tanganyika na mto malagarasi ambapo samaki wa mto malagarasi , kambale na kamongo huuzwa hadi tabora na mikoa mingine
kigoma pia kuna vitenge wax , delux, hitaget ambavyo huuzwa mikoa mingine kwa bei ya juu.
 
4.MBEYA&SONGWE
mkoa huu ni mkubwa na fursa zake ni nyingi kulingana na kupakana na nchi kama zambia na malawi mazao ya chakula na biashara hupatikana kwa wingi
mpunga na mchele ndio uko huko
viazi mviringo au viazi ulaya hutoka mikoa hiyo na kuuzwa mikoa mingine huko ndio kinatoka kiazi cha chips iliyoshiba.
lakini pia kuna hiriki ambayo hulimwa kule ileje.
kuna biashara ya kahawa pia hasa songwe.
biashara ya mtumba nguo na viatu pale sido.
Mbeya kuna vyuo pia hivyo stationaries ni fursa pia.
mbeya kuna fursa nyingi mno wenyeji wa mikoa hiyo wataongezea.
 
KAGERA/BUKOBA.
mkoa tajwa hapo juu una fursa nyingi pia za kibiashara ikiwamo bidhaa za vifaa vya ujenzi kama cement na mabati kwani hakuna viwanda vya vifaa hivo kwa hiyo fursa hiyo kwa kagera ipo nje karibu wilaya zote kuanzia muleba, karagwe, Bukoba mjini na vijijini nackadhalika.
lakini pia kuna shughuli za uvuvi kwani kuna ziwa victoria sasa hapa wilaya ya muleba ndio yenye visiwa vingi vya uvuvi hapa kunabiashara ya dagaa wakavu na wakukaangwa ambao husafirishwa nje na ndani ya nchi na kuna soko la uhakika maeneo mengi,
lakini pia kuna kuweza kusafirisha samaki wabichi kutoka Kagera kwenda kuwauza mikoa mingine au hata viwandani ,
kuna kilimo cha kahawa na maharage hasa karagwe ambapo maharage hupelekwa mikoa mingine
lakini kuna kilimo cha mpunga pale kibaoni ambacho hilipa sana.
kuna ndizi na senene ambazo huuzwa pia mikoa mingine.
 
6.KILIMANJARO/ARUSHA.
mikoa hii kama mnavyofahamu biashara ilizaliwa huku kila fursa nitayoitaja hapa ilishachangamkiwa.
uchimbaji wa madini ,lakini pia kuna utalii katika mikoa tajwa.
fursa nyingine ni mtumba ukifanikiwa kufikisha mtumba wa nguo na viatu mikoa hii utapiga pesa mno.
kwani wenyeji wa mikoa hii hupendelea mavazi ya mtumba.
usisahau makoti hasa yale ya ngozi au leather za kiume na kike mikoa hii hawapendi vitu feki hivyo ukipeleka vitu og utafanya biashara.
kuna kilimo cha vitunguu pia kilimanjaro.
kuna viwanda huku unaweza kwenda kuchukua pia viatu pale karanga ukauza sehemu nyingine.
kuna viwandakama A to Z unaweza kuorder bidhaa mbali mbali ukapeleka maeneo mengine.
mikoa hii imepakana na kenya hivyo unaweza kuangaliabidhaa zilizo Arusha na Kilimanjaro ukazipeleka Kenya kama anavyofanya monoban huuza sana unga wa mahindi pale kenya.
fursa ni nyingi huku hizo ni baadhi tu wenyeji wataongezea
 
KAGERA/BUKOBA.
mkoa tajwa hapo juu una fursa nyingi pia za kibiashara ikiwamo bidhaa za vifaa vya ujenzi kama cement na mabati kwani hakuna viwanda vya vifaa hivo kwa hiyo fursa hiyo kwa kagera ipo nje karibu wilaya zote kuanzia muleba, karagwe, Bukoba mjini na vijijini nackadhalika.
lakini pia kuna shughuli za uvuvi kwani kuna ziwa victoria sasa hapa wilaya ya muleba ndio yenye visiwa vingi vya uvuvi hapa kunabiashara ya dagaa wakavu na wakukaangwa ambao husafirishwa nje na ndani ya nchi na kuna soko la uhakika maeneo mengi,
lakini pia kuna kuweza kusafirisha samaki wabichi kutoka Kagera kwenda kuwauza mikoa mingine au hata viwandani ,
kuna kilimo cha kahawa na maharage hasa karagwe ambapo maharage hupelekwa mikoa mingine
lakini kuna kilimo cha mpunga pale kibaoni ambacho hilipa sana.
kuna ndizi na senene ambazo huuzwa pia mikoa mingine.
Mkuu ni mwezi gani ambao maharage yanapatikana kwa wingi? Na no maeneo gani yanapatikana kwa wingi huko karagwe?
 
Nimetembelea Lushoto hivi majuzi ila sikuwa na muda wa kutosha kuzuru vema ila nimevutiwa sana na ule mji. Nataman sana kuishi pale coz hali ya hewa ni nzuri mno. Napenda kujua kuna issue gani za msingi ninazoweza kufanya pale za kuniingizia hela kama biashara, kilimo, ufugaji, huduma au lolote tu ilhali nisikae bure. Please mwenye info za Lushoto!!!
 
WEWE NI MKAZI WA WAPI NA WASHUGHULIKA NA NINI?

TUANZIE HAPO KWANZA.
 
Ukifungua biashara inabidi iwe tofauti hapO utapata wateja,ila ikiwa ya kawaida ambayo hata mwenyeji anaweza fungua esabu imekula kwako labda uwe msambaa au mpare.watu gani hadi kwenye biashara wanazungumza kikabila tuu,ptuuuuu
 
acha wivu wenyewe tunapendana sana
 
Back
Top Bottom