Fursa za biashara kwa kila mkoa hapa nchini

Compact

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
3,946
2,000
Wapendwa ni muda sasa nawaza wapi panafaa kwa biashara na mzunguko wake wa pesa ni mkubwa kulinganisha na mahala pengine.
Toa mji wa mamwinyi TANGA
Je, ni biashara ya aina gani?

Ukiachana na biashara za Mazao kwa kuwa kilimo hakifanywi kwa kiwango kikubwa, Dar es Salaam ni jiji linolafaa sana kwa Biashara. Bidhaa nyingi sana zinauzika kutokana na utitiri mwingi wa watu. Sema kuna ushindani wa hali ya juu.

Arusha pia ni jiji zuri sana kwa biashara. Haswa ukizingatia kuwa linatembelea sana na wageni kutoka nchi za nje.
 

Kingdavi.ii

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,181
2,000
Wapendwa ni muda sasa nawaza wapi panafaa kwa biashara na mzunguko wake wa pesa ni mkubwa kulinganisha na mahala pengine.
Toa mji wa mamwinyi TANGA
Inategemea ni biashara gani unataka kufanya lakini mahali popote ambapo kuna watu lazima kuna fursa ya biashara kutokana na uhitaji wetu sisi wanadamu
 

Kingdavi.ii

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,181
2,000
Mahitaji yanatofsutiana kutokana na mazingira, uchumu na mfumo wa , maisha: mfano unaweza kusafirisha mazao kama viazi mviringo, nyanya kutoka Southern highland kama IRINGA, MBY au NJMB kwenda DAR nakuchukua mzigo kama bales za nguo viatu na vifaa vya ujenzi au vya pikipiki kwenda maneo ulipotoka BUT huu ni mfano halisi mmoja , muhimu ni kufanya survey au feasibility study ya biashara unayoitaka kutokana na mahitaji ya eneo. Ahsante
 

Aventus

JF-Expert Member
Mar 8, 2013
1,706
2,000
Naipendelea simiyu zamani(bariadi)ni mji unaoanza kuwa.naona watu wengi wanafanya biashara hasa za nguo,mazao na mengineyo.ila biashara za pale ni za msimu.

Kwa kua ni mji unaokua na kuona wajenzi wengi wanapenda tofali za kuchoma nikajaribu kwa mtaji mdogo tu
Tofali bichi sh.7@1
Kuni sh 50000 mapori mengi
Usafiri 20000 wa tela la ngombe. kuleta maji 10000.
Eneo nilipewa bure bada ya biashara niliwapa 20000 ya shukrani tu.
Wa kuchoma na kupanga niliwapa lak 1.
Nilichoma tofali 10000.
Mahesabu ni
7×10000+50000+20000+20000+100000+10000=370000
Mtaji ni 370000 fanya kuna tofal zitaharibika so weka 30000.pesa yote ya mtaji ni lak 4 mpaka tofali kuiva teyar kwa kuuzwa.

TWENDE KWENYE BIASHARA SASA

minimum tofali moja 120tsh
120×10000=1200000tsh

Kama bei ya kawaida 150 tsh
150×10000=1500000tsh

Ukitoa mtaji jibu utakua nalo umebaki na faida ya sh. Ngap

MUHIMU
hii biashara ni ya wakati wote ila bei zinapanda tokana na msimu.msimu wa mvua ndo tofali haikamatiki.msimu wa kiangazi bei inakua chini mana wapiga tofali ni wengi sana.

CHANGAMOTO
biashara hii siyo ya hapo kwa papo wakati mwingine inachukua mda mpaka kuja kuuza so kama huna shughuli ingine utataabika mzee.

Kama biashara yako itakua ni ya huakika na kuaminika utakula tenda nyingi mkuu na hizo ndo zinalipa hakuna mfano.sababu ukiweka mtaji mkubwa na faida inakua kubwa mfano ukiweka tofali laki moja faida utaipenda zaidi.
Pia kuna wale wanunuzi watofal chache chache hawanunui tanuru nzima waepuke wanavuruga malengo

Note:hii biashara nilifanya 2014 sijui kwa sasa bei zikoje
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom