SoC02 Fursa iliyobadilisha maisha yangu

Stories of Change - 2022 Competition

Skull App

Member
Jul 7, 2018
47
56
FURSA ILIYOBADILISHA MAISHA YANGU

UTANGULIZI
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, najua mtakua mmeitikia “Kazi iendeleee”. Twende kwenye fursa sasa.

Hii ni fursa amabayo inayoweza kumsaidia kijana au mtu yoyote kutoka kwenye wimbi kubwa la umasikini kuelekea kwenye safari ya mafanikio na kutimiza ndoto zake, Je unajua ni fursa gani?

Endelea kuwa nami kwenye hili andiko langu pendwa litakalokwenda kubadilisha maisha yako endapo utafanya maamuzi sahihi ya uwekezaji.

MCHONGO WENYEWE HUU HAPA (FURSA YENYEWE HII HAPA CHINI)
Fursa yenyewe ni uzalishaji na ushonaji wa chupi za kike na za kiume kwa kutumia mashine za kawaida za kushonea nguo (in a small scale), Ndiyo namaanisha ni uzalishaji wa nguo za ndani za kiume (boksa) na za kike (chupi). Ukiweza kujitanua unaweza fanya uzalishaji wa hata wa sidiria.

Hahahaha! Najua unashangaa sana, hata mimi nilijishangaa sana pale nilipoota eti niko mnadani nauza chupi,nilicheka sana,dah! Eti mimi Skull App mwenye shahada yangu kutoka chuo kikuu maarufu kinachotambulika na serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenye android apps zangu google playstore niuze chupi? Hahahaha! Nilicheka sana.

Huwezi amini mpaka sasa hii ndiyo fursa ninayoitegemea sasa ukiachana na hizo fursa nyingine

KIJANA KAMATA FURSA (KAMATA FURSA MTU WANGU)
Nashauri, Kijana kamata hii fursa ya uzalishaji na uuzaji nguo za ndani za kike (chupi) na za kiume (boksa), Kwani hii fursa unaweza kuifanya ukiwa na mtaji mdogo sana ambao kwa kijana au mtu yeyote anaweza kupata mtaji huo kwa urahisi zaidi.

UZALISHAJI WA NGUO ZA NDANI (CHUPI NA BOKSA)

MAHITAJI

- Mashine ya kushonea chupi (Cherehani)

- Vitambaa vya kushonea na chupi.

- Chupi zilizo shonwa tayari kwa ajili ya kuchukua na kulinganisha vipimo vya chupi utakazo kwenda kuzalisha.

- Tape ya kupimia vipimo vya chupi kipindi cha uzalishaji

- Urembo unao wekwa kwenye chupi.

- Vifaa vingine vidogo vidogo mfano Pini au ring kwa ajili ya kubania vitambaa, uzi tofauti tofauti wa rangi tofauti tofauti, Nakadharika.

UJUZI
Hutakiwi uwe na ujumbe mkubwa wa ushonaji katika uzalishaji wa nguo za ndani (chupi na boksa) ila unatakiwa ujue jinsi ya kudhibiti mashine ya kushonea, pia uwe na uwezo wa kupima vipimo utavyo kwenda kutumia kwenye uzalishaji wa nguo za ndani (chupi na boksa).

UPATIKANAJI WA VITAMBAA NA UREMBO
Vitambaa vya uzalishaji nguo za ndani (chupi na boksa) unaweza kuagiza mwenyewe kutoka China au kwa hawa jamaa wanaojiita RABA ONE wako zao hukoo mtoni Kijichi.

MTAJI
Makadilio ya mtaji wa kuanzisha uzalishaji wa ushonaji wa chupi za ndani za kike na za kiume ni kama inavyo onekana kwenye mchanganuo ufuatao

1. Bei ya machine ya kushonea chupi yaani cherehani – Makadilio ya tsh 450,000 au unaweza kununua pia min sewage machine ya tsh 150,000 ya kuanzia inayouzwa na hawa jamaa wanaojiita RABA ONE wanopatikana huko mtoni kijichi Dar es salaam (au unaweza kuazima mashine ya kushonea nguo (cherehani) ili kupunguza gharama.

2. Vitambaa vya kushonea nguo za ndani – Makadilio ni 5000 @ meter

3. Roler ya urembo wa kuzungushia chupi – Makadilio ni 5000 @ roler

4. Tape ya kupimia vipimo vya chupi kipindi cha uzalishaji – Makadilio tsh 6000

MASOKO
Kuhusu masoko wewe utajua mwenyewe, Haha haha! Mimi niko zangu Maswa-Simiyu na wasukuma wana nunua kweli kweli, wanajua bidhaa zinatoka China, kumbe najifungia zangu chumbani na kimashine changu cha mchongo nafanya mambo huku nikijilipua na kinywaji chetu pendwa baridii cha kanda ya ziwa.

MUHIMU: Na amini, masoko ya uuzaji chupi yapo ya kutosha kwani kuna huitaji mkubwa sana wa uvaaji wa chupi nchini Tanzania, kwa makadilio rahisi kwa kila watu 10, watu 9 wanavaa au wanatumia chupi, hivyo tunaweza kusema soko la chupi linapatikana katika mikoa yote ndani ya Tanzania.

CHANGAMOTO
1. Ubinafsi kupelekea uzalishaji kuwa mdogo
Eh! bana mimi ni mbinafsi haswa, sasa kwanini niwashtue watu juu ya fursa inayonipa pesa za kutosha wakati nataka nipige pesa kimya kimya bila watu kujua, Kuna watu wata iuliza kwanini nimetoa siri hii huku jamii forums, haha haha! Si nimeona kuna Tsh 5,000,000/=, najua kabisa kwa wazo hili halisia azikwepekwi kuja kwangu, nimeshapigia hesabu kuongeza mtaji ili niiweze pia kuajiri vijana wenzangu na kulipa kodi kwani kwa sasa sijafanikiwa kuajili kijana yeyote pia siajfanikiwa kuanza kulipa kodi na kurathmisha biashara hii kutokana na kuwepo kwa mtaji mdogo usiotosheleza.

ANGALIZO: Mtaji mdogo hupelekea mtu kuwa na hali ya ubinafsi.

2. Ushindani kutoka China na viwanda vikubwa duniani
Ushindani wa uzalishaji wa nguo za ndani kutoka China na viwanda vikubwa kutoka sehemu mbalimbali unaathiri uzalishaji wa ndani wa nguo za ndani, kiukweli uzalishaji unaotoka China na sehemu zengine za dunia bidhaa zake zinazalishwa kwa ubora zaidi kuliko huu uzalisha tunaofanya kwa kutumia mashine ndogo yaani cherehani ila wenzetu wanatumia mashine zinazohusisha tekinolojia kubwa hivyo kupelekea uzalisha wao kuwa mkubwa zaidi na ni bora zaidi.

3. Mtaji kuwa mdogo
Mtaji kuwa mdogo (mtaji usiotosheleza mahitaji ya uzalishaji nguo za ndani) ni changamoto kubwa sana, hii hupelekea uzalishaji mdogo usiokidhi mahitaji ya wanunuaji wa nguo za ndani, endapo mtaji ukiwa mkubwa pia uzalishaji utakuwa mkubwa kwa kuongeza idadi ya vitendea kazi vitakavyotumika katika uzalishaji wa nguo za ndani.

HITIMISHO
Kijana kamat fursa mtu wangu, nasisitiza tena kijana kamata fursa mtu wangu husije sema sijakwambia, Hii ni fursa ambayo inaweza kukupeleka au kukuanzishia safari moja nzuri ya mafanikio, kwani inaonyesha kwa asilimia kubwa Tanzania na pia duniani kwa ujumla uvaaji wa nguo za ndani unafanyika na umefanikiwa kwa asilimia kubwa, hivyo kupelekea kuwa na soko la uhakika kupitia uzalishaji wa nguo za ndani yaani chupi kwa wasichana na boksa kwa wavulana.

MUHIMU: Nawakumbusha msisahau kunipigia kura ndugu zangu ila niweze kushinda na kuboresha huu uwekezaji wangu uwe kwa kiwango kikubwa.

Ni mimi mdau wenu

Skull APP

Maswa - Simiyu
 
Back
Top Bottom