Kamati ya Kudumu ya Bunge ya PIC yahimiza taasisi za Serikali zinazodaiwa na SUMA JKT kulipa ili kutodhoofisha jitihada za uwekezaji

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa mitaji ya umma (PIC), imepingeza jitihada mbalimbali sinazofanywa na SUMAJKT ambazo zimmedaiwa kuwa zimekuwa chachu ya kukuza uchumi wa Taifa na mtu mmoja mmoja.

Akizungumza kwa niaba ya Kamati ya PIC, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deus Clement Sangu (Mb), baada ya ziara ya ukaguzi wa kiwanda cha nguo pamoja na kiwanda cha maji ambavyo vipo chini ya SUMAJKT eneo la Mgulani Jijini Dar es salaam, amesema kuwa katika kiwanda cha nguo kimeongeza udhalishaji mara baada ya kutumia zaidi ya milioni 390 kwa ajili ya maboresho.

"Leo tumekuja kutembelea baadhi ya miradi inayoendeshwa na kampuni ya SUMAJKT ya uzalishaji mali, kipekee tumepata fursa ya kutembelea sehemu mbili, kwanza tumekuja kutembelea kwenye kampuni tanzu ya uzalishaji nguo na kampuni tanzu ya uzalishaji maji"

Ameeleza kuwa "Tumeona hapa tulipo tumekagua kiwanda cha nguo ambapo zimewekezwa fedha takribani milioni 391, na kwakweli kazi kweli kazi tuliyoiona hapa ni kubwa, mwanzo walikuwa na uwezo wa kuzalisha nguo 350 sasa wazalisha pisi 700 na bado wanahitaji kupewa nguvu zaidi ili hata waweze kudharisha pisi 1000 kwa siku."

Pia ameongeza kuwa "Tunaona namna walivyojipanga wamefikia hadi wateja wa nje ya Nchi, tunaambiwa hapa kwamba wana wateja hadi kwenye visiwa vya Comoro, kwahiyo uwekezaji huu kama Kamati ya Kudumu ya Bunge tunasema tunaosimamia mitaji ya umma tunasema ni uwekezaji ambao kwanza unatia hamasa na kuleta tija."

Aidha amesema kuwa uwekezaji kwenye viwanda hivyo umekuwa ukileta tija mbalimbali ikiwemo kuchangia katika sekta ya ajira, ambapo amesema kuwa katika kiwanda hicho cha nguo vijana zaidi ya 350 wameajiliwa kwenye ikiwa wengine wanaotokea ndani ya jeshi la kujenga Taifa huku akidai kuwa wengine uraiani ambao ni karibia asimia 70.

Amesema kuwa kutokana na ushirikiano ambao umekuwpo baina ya Kamati hiyo na SUMAJKT, amedai kuwa wataendelwza ushirikiano huo kwa kushauriana na kupaza sauti zao ili kuhakikisha uwekezaji unaendelea kukua na unaleta tija zaidi kwa umma.

"Sisi kama Kamati ya Kudumu ya Bunge ambao tunaangalia uwekezaji wa mitaji ya umma tunataendele kutoa ushirikiano mkubwa kwa SUMAJKT ili uwekezaji zaidi uweze kuwekwa kwa sababu tunaona shughuli zinazofanyika hapa zina tija kubwa kwa Nchi lakini pia kwa mtu mmoja mmoja unapotoa ajira kwa vijana." Amesema Mwenyekiti wa Kamati hiyo

Hata hivyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo amesema kuwa wanzao taarifa kuwa baadhi ya taasisi za Serikali ambazo zinadaiwa na SUMAJKT hivyo wametoa rai kwao kwa kuwaimiza kulipa gharama hizo ili kutochelewesha uwendelaji wa miradi ambayo hipo chini ya SUMAJKT

"Kama kamati ya Bunge tunaendelea kuhimiza taasisi zile zote za Serikali wanaodaiwa na kampuni ya uzalishaji mali ya SUMAJKT waweze kurejesha hizo fedha ili taasisi yetu iweze kusonga mbele."

Lakini pia amesema kuwa ni jambo linaloleta matumaini kwa SUMAJKT kuanza kutanua soko kufikia mataifa ya nje, jambo ambalo amesema kuwa wataendelea kuliimiza zaidi, ambapo amesema kuwa hata Rais Samia amekuwa akiimiza suala hilo la kukuza diplomasia ya uchumi.

Pia Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT, Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele, amesema kuwa kiwango cha uzalishaji kimeongezeka lakini bado lengo lao ni kuongeza uzalishaji zaidi.

"Tumetumia zaidi ya milioni 390 kuhakikisha kiwanda hiki tunakiboresha kwa kuongeza Mashine na 'line' nyingine, tulikuwa na 'line' za udhalilishaji lakini sasa tuna sita kwahiyo tumetoka kwenye uzalishaji wa nguo 300 au 400 kwa sasa tunauwezo kuzalisha nguo 700 kwa siku lakini tuna malengo ya kuzalisha nguo 1000 kwa siku"amesema Meja Jenerali Rajabu

Hata hivyo amesema kuwa matunda ya diplomasia ya kiuchumi kiuchumi yameanza kuwawezesha kutanua soko kuuza bidhaa wanazozalisha nje ya Tanzania, ambapo amesema kuwa licha ya kupata tenda Comoro lakini walipata tenda ya kuuza viatu kwenye Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

"Tunamshukuru Mh.Rais ambaye ni amri Jeshi Mkuu kwa kukuza diplomasia ya uchumi, mahusiano na Nchi nyingi ni mazuri sana, viongozi wa majeshi hasa wapotembelea Tanzania wanapotembelea Jeshi letu la Ulinzi wa Wananchi wamekuwa wakija kutembelea kiwanda hiki na viwanda vingine vya SUMAJKT "amesema Meja Jenerali Rajabu

Kuhusu suala la madeni kwenye baadhi ya taasisi za Serikali Meja Jenerali Rajabu amekili kuwa lipo.

Aidha Mbunge Nkasi Kaskazini, Aida Joseph Kenani ambaye ni mjumbe wa Kamati ya PIC ameshauri SUMAJKT kupitia kiwanda hicho cha kuzalisha nguo kufikiri namna wanaweza kutumia mitambo zaidi ili kuongeza uzalishaji, akitolea maelezo suala hilo Meja Jenerali Rajab amesema kuwa watalifanyia tathimini suala hilo.
View attachment 2815247View attachment 2815248View attachment 2815249
IMG_20231115_103440_655.jpg
 
Hiyo Suma JKT inafanyiwa auditing na CAG??
Wao Suma wanalipwa kiasi gani Kwa mlinzi mmoja na wao wanalipa kiasi gani?
 
Back
Top Bottom