Mungu awajalie watz wapate macho ya rohoni kwamba ccm ni genge la wauza madawa ya kulevya na majangili ya mali za umma, popote watz tuamke kuizika ccm rasmi ndio kilicho baki, CHADEMA MUNGU AWALINDE DAIMA NA AWAPE KIBALI MACHONI PA WENYE AKILI ILI MLETE UKOMBOZI WA KWELI KWA TZ
Leo Jumamosi, kuanzia majira ya saa 8, Mkiti wa CHADEMA, Freemam Mbowe, akiambatana na Naibu Katibu Mkuu Bara Zitto Kabwe atautikisa mkoa wa Tabora kwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya Chipukizi.
Viongozi wengine watakaokuwepo ambao tayari wamewasili mjini hapa ni Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni, Benson Kigaila, Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri, John Mrema na wabunge wa Kanda ya Magharibi (Kigoma, Katavi na Tabora) .
Lengo kubwa la mkutano huo ni kukamilisha uzinduzi wa Kanda ya Magharibi.
Tayari manispaa ya Tabora na vitongoji vyake kuna shamrashamra za aina yake na mkutano huo unatarajiwa kuzidi kusimika Chadema katika mkoa huu wenye historia kubwa ya mageuzi.
Itakumbukwa sera ya kugawa chama kikanda tayari imeleta mafanikio makubwa tukichukulia chaguzi ndogo za Madiwani zilizofanyika hivi karibuni ambapo Chadema imeshinda kata za kutosha na kura karibu asilimia 50% ya kura zote zilizopigwa zikijumlishwa pamoja.
Mkuu wa Habari Chadema
Tumaini Makene akishirikiana na
Molemo anatarajiwa kutuletea Live Coverage kutoka eneo la tukio.
-----------------------------------------------
Updates kutoka mkutanoni...
-------------------------------------------------
Sasa amepanda Mbunge Sabrina Sungura. Anasema wananchi wa Kigoma walishaikataa CCM siku nyingi. Anawataka wana Tabora nao kufanya hvyo, wananchi wanaitikia mwisho uchaguzi uliopita. Amewataka watimize ahadi hiyo. CCM chama kinachomaliza rasilimali, tembo wanateketezwa na CCM, watoto wetu na wajukuu watarithi nini! Kigoma ilikuwa waifute CCM wakachakachua majimbo 3.
Sasa anafuatia Mkurugenzi wa Bunge na H/shauri John Mrema. Sasa anaelezea kadhia ya kodi ya simcard, kodi kwenye M-pesa, tigo pesa, airtel money, na zote, kila sh. 100 kwenye matumizi ya simu imewekwa kodi sh. 36.5 hiyo ni mbali na simcard tax. Anasema CCM wana beep, wakiruhusiwa watakuja na kodi zote za manyanyaso! Watanzania wasikae kimya!
----------------------------------
[/QUOTE]