Freeman Mbowe, tueleze CHADEMA mlipompeleka Ben Saanane

Freeman Mbowe, tueleze CHADEMA mlipompeleka Ben Saanane

Hii Issue ya Ben Kupotea ni serious sidhani kama kweli amejificha kutafuta Publicity,Ben ni msoni na maarufu tu hana sababu ya kufanya hivyo,SASA NDIO NIMEAMINI BEN YUPO PEKE YAKE NA CHATU.
 
Chadema hv ndo wanatafutaga wahalifu au ni polisi je akipotea ndugu yangu niripoti polisi au chadema…
 
SATURDAY, MARCH 14, 2015
Viongozi wa Chadema kizimbani
 0      
       
Diwani wa Kata ya Ubungo, Boniface Jacob (mbele) na mlinzi wa chama hicho, Berson Mramba wakitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana. Picha na Anthony Siame
By Tausi Ally, Mwananchi
Dar es Salaam. Viongozi watatu wa Chadema, akiwamo diwani wa Ubungo, wamefikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu wakikabiliwa na mashtaka mawili ya kuteka na kujeruhi.
Diwani huyo, Boniface Jacob (32), mkuu wa walinzi wa Chadema, Hemed Sabula (48) na ofisa utawala wa chama hicho, Benson Mramba (30) walipandishwa kizimbani jana wakituhumiwa kumteka aliyekuwa mlinzi wa katibu mkuu wa chama hicho, Khalid Kagenzi.
Akiwasomea mashtaka hayo, Wakili wa Serikali Janeth Kitali alidai kuwa Machi 7, 2015 walimjeruhi na kumteka nyara Kagenzi kwa nia ya kuzuia uhuru wake.
Kitali alidai kuwa washtakiwa hao walifanya makosa hayo kinyume na kifungu cha 225 na 249 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Akisoma hati hiyo ya mashtaka Kitali alidai kuwa Machi 7,2015 washtakiwa hao kwa pamoja wakiwa katika ofisi za makao makuu ya Chadema ziliyopo Mtaa wa Ufipa, Kinondoni walimjeruhi Kangezi katika maeneo mbalimbali ya mwili wake.
Kitali alidai kuwa siku hiyo ya tukio washtakiwa hao kwa pamoja, wakiwa katika ofisi hizo za Chadema, walimteka Kagenzi na kumpeleka Hoteli ya River View iliyopo Sinza.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa wote walikana na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Wakili wa washtakiwa hao, Peter Kibatala akishirikiana na wakili John Mallya waliiomba mahakama kuwapa dhamana wateja wao kwa kuzingatia kifungu cha 148 cha Sheria ya Makosa ya Jinai Sura ya 20 iliyofanyiwa marekebisho 2002.
Hakimu Mkazi, Waliarwande Lema alimtaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili na kila mmoja asaini hati ya dhamana ya maneno ya Sh10 milioni na kwamba wadhamini hao wasiwe walimu.
Wadhamini wa washtakiwa hao waliwasilisha nyaraka zao, lakini Kitali aliomba kupewa nafasi kuzihakiki, lakini hazikukidhi masharti na hivyo washtakiwa kutakiwa kupelekwa mahabusi.
Hakimu Lema aliiahirisha kesi hadi Machi 26,2015 kwa ajili ya kutaja kuangalia upelelezi utakuwa umekamilika ama la.
Chanzo cha washtakiwa hao watatu kufikishwa mahakamani ni tuhuma zilizotolewa kuwa Kagenzi alihojiwa na maofisa wa Chadema waliomtuhumu kumwekea sumu Dk Slaa.
Tuhuma hizo zilitolewa hadharani na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Mabere Marando, ambaye alisema Kagenzi alikuwa akishirikiana na maofisa wa usalama wa taifa kutekeleza tukio hilo.
Kagenzi alichukuliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano na baada ya siku kadhaa, aliachiwa huru na kuzungumza na vyombo vya habari yale yaliyomtokea na jinsi alivyoteswa.
Wakati Kagenzi akieleza hayo, washatakiwa hao watatu walikamatwa na polisi kwa mahojiano hadi walipofikishwa mahakamani.
 
Nimefuatilia kwa makini tamko la CHADEMA lililotolewa na Mh. Tundu Lissu kuhusu kupotea kwa Ben Saanane, Katibu Myeka wa Mwenyekiti wa Taifa CHADEMA na pia Mkuu wa sera na utafiti katika Chama hicho.

Kusema kweli sijaridhika kabisa na tamko la Tundu Lissu na inatia uchungu kuona watu wazima wanafanya maigizo na maisha ya mtu. Ben ni mtanzania mwenzetu bila kujali itikadi ya vyama. Haingii akilini kuwa ujumbe wa SMS aliyoonesha Lissu ndiyo chanzo cha Ben kupotea. Huu ni ujinga unaoweza kuelezwa wajinga tu watu wenye akili hawawezi kukubaliana ujinga huu.

Niliwaambia humu JamiiForums kuwa Mbowe, Mushi, wanajua Ben alipo. Lakini cha hiyo post iliondolewa haraka humu JamiiRorums. Kuna Dada anayedaiwa kuwa karibu Ben Saanane anayejulikana kwenye mitandao kwa jina la Hilda Newton CHADEMA aliwahi kupost kwenye page yake ya fb alopoulizwa kuwa Ben yuko Africa Kusini alipotumwa kikazi.

Kinachonishangaza zaidi katika sakata Ili Ben Saanane ni ukimya wa muajiri wake hata baada ya taarifa hiyo kusambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kimataifa. Haiwezekani Katibu Myeka wa Mwenyekiti apotee kwa siku zaidi ya 20 mwajiri usishtuke. Leo mnataka kupaka matope serikali kwa kwa issue ya kijinga kama hii.

Kama SMS za vitisho tumezipata nyingi, mimi mwenyewe nimetishwa Sana mpaka vikao vizito vimekaliwa na viongozi wa chama chenu kunijadili. Mwanasiasa yeyote kutishwa ni issue ya kawaida. Ni kweli serikali inawajibu wa kumlinda kila Raia lakini hiyo haiondoi wajibu wa familia, mwajiri kumlinda mtu wao. Ndiyo maana Tundu Lissu amejenga uzio kwenye nyumba yake.

Kinachotia shaka zaidi ni pale Chama kinapozuia Makada na marafiki wa Ben kujadili suala hilo na kumlazimisha kada wake Malisa GJ kufuta post yake aliyoilaumu gazeti la Mwenyekiti wa CHADEMA, Tanzania Daima. Mimi naamini suala la Saanane ni la kimkakati wa kisiasa kutaka kuchafua serikali machoni pa kimataifa.

Viongozi CHADEMA Wanamfahamu alipo Ben. Mbowe Mrudishe Saanane akiwa hai.
Ni kweli ndio maana wamewaacha NYANI & TUMBILI waruke na kukanyagana baada ya kunogewa na NDOTO za SELO.
 
Hamna anayehangaika na mafisadi chadema kwa sasa.

Hasa hiki kitendo Cha Mbowe kwenda ulaya kutoa hotuba za kuichafua nchi kimewaudhi sana watanzania.


2020 chadema wajiandae kupungua bungeni.
 
Kuna mods walitakiwa wapelekwe selo badala ya max. Mimi nauliza endapo ben atajitokeza atakuwa na kosa kisheria? Halafu huyu anaunganisha kwenye post inayozungumzia mbowe anajua alipo ben!
 
Acha upuuzi........HILI SUALA LA BEN cdm HAMWEZI LIEPUKA KABSA...na ndio maana hata hamlichukulii kwa uzito unaostahili....Tulitegeea mpaka sasa M/KITI na hata KATIBU wametoa hata tamko kuonyeshwa kuguswa na hili JAMBO lakini kimya...ila kilichobaki nikuinyooshea SERIKALI MKONO..........mmemtumia kijana wa watu kutukana VIONGOZI huku mkiwa na lengo lenu kichwani mwisho wa siku hionekani ni SERIKALI ndio imehusika na kupotea kwake,,,,,
UMEMALIZA!
BRING BACK OUR BEN ALIVE!!
 
Yaani hadi leo hajaongelea wala kuonyesha kuhuzunika juu ya kupotea kwa msaidizi wake muhimu Ben Saanane.Hii ni zaidi ya ukauzu au ile inaitwa "uso wa mbuzi".Jitambue bhana chairman!
 
Yaani hadi leo hajaongelea wala kuonyesha kuhuzunika juu ya kupotea kwa msaidizi wake muhimu Ben Saanane.Hii ni zaidi ya ukauzu au ile inaitwa "uso wa mbuzi".Jitambue bhana chairman!
We mbona huwajali wazazi wako. Kwani hatujui!!🙁😀🙁
 
Malisa alipote humu jamii forums kwa muda ambao unaendana na muda aliopotea Malisa.Afuatiliwe huo muda alikuwa wapi.

Pili Mbowe aeleze vizuri ilikuwaje wakamtoa BEN saanane toka kuwa mwajiriwa Mkurugenzi wa Utafiti na SERA wa CHADEMA na kumfanya house boy (PERSONAL ASSISTANT) wa MBOWE ambaye si mwajiriwa wa CHADEMA? Kuna nini alikosea je ilikuwa ni kumwadhibu? Na je adhabu yake iliishia hapo?

Huyo SHAO naye wa kufuatiliwa ni kama mtu fulani hivi

soma hii habari


Wakuu Habari zenu,

Kwa vile Ben Saanane ameonesha kuwa ni mtu anayeamini katika Ukweli na uwazi kiasi cha kupambana na kumshambulia Rais Magufuli mfululizo kwenye page yake Facebook.Jamii forums na Makala za Raia Mwema,sasa hebu ajitokeze aeleze fedha hizi alizolipwa na ubalozi wa Sahara Magharibi ni zaidi ya Milioni 12 ni za nini?

Vilevile kabla ya mfalme wa Morroco kuingia zilipatikana taarifa za ubalozi wa Sahara kwa kushirikiana na balozi fulani hapa nchini ziliwalipa watu fedha ili kuhakikisha Ziara ile inachafuliwa.

Ikumbukwe baada ya hapo kuna kundi lililojiita la TASSC lilifanya mkutano na waandishi wa habari Landmark hotel.Fedha walitoa wapi?Taarifa za uhakika Ben Saanane aliongea na baadhi ya wahariri na yeye haijulikani alikuwa na maslahi gani na katika habari hiyo .

Jeshi la polisi lilimkamata na kumhoji Kijana Noel Shao ambae kwa uchunguzi wa kina hapo kabla alionekana kuwa na ushirikiano na mawasiliano ya karibu na Ben Saanane na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani.


Vilevile tutapata taarifa nzuri juu ya mmiliki wa Akaunti namba 01J1093293000.

Kama tumefikia hatua kwamba sasa watu ambao serikali iliwasomesha kwa fedha nyingi wanaamua kutumika vibaya na wasiolitakia taifa letu mema basi Tanzania haitakaa iendelee.

Kwa anachofanya kijana huyu msomi hakina tofauti na kile alichosema Evarist Chahali kuwa ni ugaidi na anatekeleza makosa makubwa ya kiuadui ya kuhujumu nchi.

Hata Marekani au uingereza hawawezi kuvumilia mambo kama haya ndiyo maana leo akina Assange na snowden wapo uhamishoni

Ndani ya mgogoro wa CUF unaoendelea kuna kiongozi Abdul Kambaya aliwahi kumshutumu kijana huyu na kutoa angalizo kwenye vyombo vya habari kuwa huyu na jussa wachunguzwe kwa karibu.Lile halikuwa jambo dogo.

Na hata kazi anayoendelea kufanya ya kumshambulia Rais Magufuli mfululizo isipodhibitiwa basi yeye na kundi lake watalifanya taiafa lionekane la ajabu kabisa.Na hata CHADEMA kitakuwa kinaongozwa na watu wasiolitakia Taifa hili mema kwani kadiri siku zinavyosonga mbele ndivyo yeye na kundi lake wanazidi kujiimarisha kwenye mitandao na wanazidi kuwa wengi huku wakifanya harakati nyingine haramu tena kwa kushirikiana na taasisi za nje.

SOURCE:Tetesi: - Ben Saanane kuna biashara gani unafanya na ubalozi wa Sahara Magharibi na Kundi la TASSC?
Polisi imeshindwa kazi?Haya mambo mbona yako mitandaoni na hatusikii polisi wakisema kitu!
Kitu kimoja nina uhakika nacho,usiombe kufanya makosa ukiwa upinzani,dola itafanya juu chini kuhakikisha inakuweka wazi na kukuchukulia hatua za kinidhamu!
Nguvu ndogo inayotumika na polisi kwny upotevu wa binadamu kuliko faru inanifanya niwe na fikra pana sana!
 
Mbona kila kukicha habari zake zinazidi kufifia, Je, ndo mmeshakata tamaa na kumtafuta au vipi? Hivi mtu muhimu chadema anaweza kupotea tu na mkakaa kimya mpaka leo hii? Kweli hii laana Mbowe, lisu &Co. haitawaacha wazima!
 
Mbona za Faru John zimefifia. Hiyo laana itawaacha salama?


Hivi Mnyama Faru unaweza kumfananisha na binadamu B.Saanane tena mtu aliyekitumikia Chama chenu kwa muda mrefu? Faru tunaweza kuwazalisha wengine hata 500, huyo Saanane mtamtoa wapi mwingine?
 
Back
Top Bottom