Freeman Mbowe: TRA walinidai Kodi Bilioni 2, Wakafunga akaunti zangu zote za biashara mpaka binafsi, Wakachukua hela

Jiwe ana madhambi sana.Sijui kama'',atakuwepo mbinguni',pamoja na maombi mazito aliyopigiwa kipindi cha maziko!
 
Ujasiri wa kuyakalia kimya madhira yote Mbowe aliupata wapi wakati yeye ni mwanasiasa na mfanyibiashara mkubwa na ana fursa ya kupata attention ya vyombo vya habari vya dunia? Kwa ujasiri wa ukimya wa kuvumilia hayo yote, Mbowe atakuwa alikuwa na vimeo vingi, mbona Lisu hakuchoka kuupigia kelele ukandamizaji aliokuwa anafanyiwa?

Vv
 
Mbowe amekosa Utu, hivi inawezekanaje leo hii anamkashifu na kumshambulia mtu aliye kufa?!!! ili iweje sasa?

watanzania walio wengi waneumia sana kwa kuondokewa na Huyo unaye mkashifu leo hii.
huu sio uungwana
Watu walipanga waongee haya baada ya kumaliza uongozi wake, lakini hajawahi maliza unategemea watu waongee lini? Maana kipindi mwenyewe yupo hai ilikuwa anakushughulikia fasta tu.
 
Mbowe ni muongo.

Mbowe anasema alifungiwa akaunti zote lakini akaamua kwenda kufanya Biashara Dubai, hizo hela za kwenda kuanzisha biashara Dubai zilikua akaunti gani kama akaunti zake zote TRA walifungia?
MwanaCCM akili zao ni kuwahurumia tu. Kwa hiyo wewe unafikiri watu wote wanaofanya biashara huweka fedha zote sehemu moja? Hata wewe usiweke fedha zote sehemu moja. utakuja kulia kilio cha kichanga siku moja. Fedha za Mbowe za biashara ndani ya Tanzania zilikombwa na Jiwe akabakiwa na kiasi alichoweka sehemu nyingine ambayo Jiwe na wewe huwezi kuifikia. asingepata hiyo akili leo mbowe angeishije?
 
Magufuli alikuwa mtu mbaya sana.
Lile kaburi lake linapaswa kupigwa pingu, kutandikwa viboko au kuwa sehemu ya watu kujisaidia haja ndogo.
Hafai kabisa kukumbukwa kwa mema yoyote.
Nasikia kuna JWTZ wanalilinda usiku na mchana. sijui wanaogopa nini kitatokea. Naishi jirani na Chato. Kuna msululu wa JWTZ wanapokezana kila siku usiku na mchana kulilinda Kaburi la Jiwe. Nafikiri wanahisi kuna kitu kinaweza kufanyika. Jinsi watu walivyo na hasira naye wanaweza kubomoa na kuchukua mwili wake kwenda kuwapa nyangumi pale ziwani
 
Mo siku akifunguka jinsi alivyolazimishwa kuhamisha hela siku alipotekwa ndipo mtajua kuwa hamjui. Nina ushahidi wa wazi wazi jinsi Jiwe alivyopora uwekezaji wa watu kwa kuwatisha. Yani ulikuwa unawekwa kwenye chumba usiku wa manane kazi ilikuwa moja kusaini nyaraka ama ukutane na chuma.

Kuna mmoja alisainishwa nyaraka usiku wa manane ili makampuni yake yataifishwe na hakuwa na jinsi maana TAKUKURU walikuwa wanamtisha kuwa akikaidi hatorudi tena kwao.

Yani kikosi kazi cha Jiwe kilikuwa kinaandaa nyaraka then unachukuliwa unapelekwa juu ghorofani na unakaa nao wewe peke yako! Hata mwanasheria wako haruhusiwi kuwepo.


Ebwanaeee Nenda zako mzee!
Weeee
 
Back
Top Bottom