Freeman Mbowe aungwe mkono uchaguzi ndani CHADEMA

Freeman Mbowe aungwe mkono uchaguzi ndani CHADEMA

AMEANDIKA BABA ASKOFU BAGONZA (PHD)

Maana yangu hii:

- Wanaosema Mbowe kawa MwenyeKiti wa maisha, wanageuka na kuunga mkono kuondoa ukomo wa vipindi vya urais katika katiba?!
wamemtuma mtu alijifanya mkulima kutest zari, katesti, tusishangae majibu ya mahakama na msajili akayafanyia kazi.
kauli za juzi kwamba akiondoka atamwachia nani stigla, barabara, bomberdier na sgr imekupa jibu, usisubiri malaika.
WAtu hao hao, wanaomba Mungu wengine allah, kila uchao Mbowe asigombee uenyekiti, wanataka mtu wao, huku ni ikiwa haijulikani.

-Wanaounga mkono Mbowe apate mpinzani ndani ya chama chake katika uchaguzi, wanageuka na kupinga uwepo wa mgombea mwingine ndani ya chama chao hapo mwakani!?

Wanaopinga mgombea pekee kwenye chama cha jirani, hao hao wanapiga kura kwa mgombea pekee katika chama chao, tena wengine kwa kuwaachia wengine wawaandikie kwenye kura ili waaminike kuwa hawakuasi msimamo.

-Wanaotabiri na kutamani kuwa upinzani ufe, hao hao wanasisitiza kiongozi wa chama hicho anayeonekana mbaya, aondolewe. Si angebaki ili akiue vizuri!?

-Wanaoshabikia kuwa upinzani umeisha, wanageuka na kushangilia msajiri anapoandika barua ya kutishia kufuta usajiri wa vyama vya upinzani!? Afute nini ikiwa upinzani haupo?

Nilimaanisha contradictions hizi masikioni zikizoeleka zinaondoa radha ya maisha. Kwa shule zilifuta Debate Clubs?
 
Kiwango cha ujinga wako na chuki kwa CHADEMA kitafakari urudishe heshima yako.
Kwa ccm katiba hairuhusu kwa CHADEMA katiba inaruhusu.

Hata CHADEMA awali Katiba ilikuwa hairuhusu, ila 2006 yakafanyika mabadiliko kijanja yaliyomuweka Mbowe mpaka leo madarakani.

Hivyo amini hata CCM wanaweza kufanya hivyovyo kuanzia kwenye katiba ya Chama hadi bungeni kwenye katiba ya jamhuri ambako bunge ni lao kwa asilimia 90.

Hivyo kama hupendi Magufuli kutawala milele anza kwanza kupinga ujinga unaoendelea ndani ya CHADEMA..
 
Baba Askofu, labda utuambie hiyo injili imetoka kitabu kipi ili sisi waumini wako tuelewe, maana naona siasa imechukua nafasi kubwa kwenye maisha yako kuliko neno LA Mungu!
Au au uliingia taranta isiyo yako?
 
Ni ajabu kila anayempinga Mbowe ni mwanaCCM
Hongereni wanacdm kwa kumuamini mbowe mpeni tano tena akamilishe ishirini madarakani, ila tunawapa tahadhari sisi wanaccm hatuna time na mambo yenu wala hatuwapangii, ila na sisi jiwe tunamwamini ikifika 2025 nasi tutaimba nyimbo zenu za tano tena kwa jiwe na ole wenu mpige kelele ya ccm hayawahusu.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiko kwenye mchakato Wa Uchaguzi wa ngazi ya Taifa. Kuna kila dalili kuwa Mwenyekiti Wa chama hicho Taifa anayemaliza muda wake, Freeman Mbowe atajitosa tena kuwania nafasi hiyo kwa kipindi kingine (sijui ni cha miaka mingapi).

Kinachoshangaza ni sababu zinazotolewa na Watiifu wa Mbowe kwanini wanaona anafaa kuendelea kuongoza chama hicho kwa kipindi kingine, eti wengine watakuwa mapandikizi ya CCM.

Ni kweli kwamba yeyote atakayejitokeza kupambana na Mbowe atakuwa ni pandikizi la CCM? au hii ndiyo namna ya kuwazuia wengine kuchukua fomu wakiogopa kuitwa jina baya la pandikizi la CCM? CHADEMA kuna Mbowe tu? Tukubaliane na kuamini hivyo?

Binafsi naona kama kauli hii inakidhalilisha Chama na Wanachama kwa ujumla.
Screenshot_20191007-084025.png
 
Mtu mwenye uwezo mzuri wa kufikiri hawezi kuiunga mkono chadema
Ccm inapendwa na wazee na wasio na elimu(akili)Hakuna mtu wa ccm ambayr utesema ni intelligent za maana.Nianze kwa kuwataja.....1.magufuli2.kabudi3.Bana.4Tulia.5Nimrod mkono 6.Tibaijuka7.Kigwangwala8.bashiru.9.Membe.10.katibu wizara ya maji naniliuuu yule11.Lipumba

Ukija upinzani 1.Lissu,2Kambole 3.Kibatala.4.Zitto.5Maalim seif 6.Karume F.7.......Just to mention few of them lakin nikwambie hao wachache tukiweka mdahalo pale Nkurumah hall tukaweka mada Lakima ccm wakimbie.Maana wengi wao PhD zao na Degree ni za kubebwa hasa yule namba 1.
 
kwanza unashtuka unaona neno Askofu..
Ukianza kusoma unaona mafumbo, vijembe na siasa..

Thanks God sio Askofu wa RC
AMEANDIKA BABA ASKOFU BAGONZA (PHD)

Maana yangu hii:

- Wanaosema Mbowe kawa MwenyeKiti wa maisha, wanageuka na kuunga mkono kuondoa ukomo wa vipindi vya urais katika katiba?!
wamemtuma mtu alijifanya mkulima kutest zari, katesti, tusishangae majibu ya mahakama na msajili akayafanyia kazi.
kauli za juzi kwamba akiondoka atamwachia nani stigla, barabara, bomberdier na sgr imekupa jibu, usisubiri malaika.
WAtu hao hao, wanaomba Mungu wengine allah, kila uchao Mbowe asigombee uenyekiti, wanataka mtu wao, huku ni ikiwa haijulikani.

-Wanaounga mkono Mbowe apate mpinzani ndani ya chama chake katika uchaguzi, wanageuka na kupinga uwepo wa mgombea mwingine ndani ya chama chao hapo mwakani!?

Wanaopinga mgombea pekee kwenye chama cha jirani, hao hao wanapiga kura kwa mgombea pekee katika chama chao, tena wengine kwa kuwaachia wengine wawaandikie kwenye kura ili waaminike kuwa hawakuasi msimamo.

-Wanaotabiri na kutamani kuwa upinzani ufe, hao hao wanasisitiza kiongozi wa chama hicho anayeonekana mbaya, aondolewe. Si angebaki ili akiue vizuri!?

-Wanaoshabikia kuwa upinzani umeisha, wanageuka na kushangilia msajiri anapoandika barua ya kutishia kufuta usajiri wa vyama vya upinzani!? Afute nini ikiwa upinzani haupo?

Nilimaanisha contradictions hizi masikioni zikizoeleka zinaondoa radha ya maisha. Kwa shule zilifuta Debate Clubs?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom