Freeman Mbowe aungwe mkono uchaguzi ndani CHADEMA

Freeman Mbowe aungwe mkono uchaguzi ndani CHADEMA

Atawale Chadema milele si ndio chama chake, wengine wahamiaji tu. Safi sana labda kama wamezaliwa uchagani.
 
Habari.

Kwa masikitiko makubwa nimepewa taarifa kutoka ndani ya Chadema kwamba ,baada ya msajili wa vyama vya siasa kuiandikia Chadema ijieleze kwa nini hawafanyi uchaguzi wa mwenyekiti wa chama kinyume na katiba ya chama ,sasa Mbowe ameanza kuhaha!!

Kinyume kabisa na katiba ya chama na ni uvunjwaji mkubwa wa katiba ya chama kinachojiita cha kidemocrasia nchini ,sasa Freeman Mbowe amesambaza vijana mitandaoni wanaoendesha kampeni ya ## mbowe 5 tena#, Lengo kubwa la kampeni hii ni kumfanya Mbowe aonekane anakubalika sana ndani ya chama na awe mwenyekiti wa milele !!

Ukweli ni kwamba Mbowe tangu alipokiuza chama kwa Lowasa hakubaliki tena ndani ya chadema kwa sasa ndiyo maana kuna kundi la wabunge wamekataa kuchangia chama kila mwezi.
Vijana mliosambazwa mitandaoni mkae mjiulize je Mbowe ndiyo ana akili pekee ya kuiongoza chadema hamna mwingine? Na kama jibu ni ndiyo basi ili kukamilisha huo udikteta ondoeni neno democrasia kwenye chama chenu.
View attachment 1225084
Kwani we kinakuuma nini we si gamba,chadema waachie wenyewe pambana na hali zenu za kumuongezea mwenyekiti wenu muda wa kutawala milele.
 
Kwani we kinakuuma nini we si gamba,chadema waachie wenyewe pambana na hali zenu za kumuongezea mwenyekiti wenu muda wa kutawala milele.
Kinachoumiza ni katiba ya chadema kuvunjwa na DJ
 
CCM yangu viko wapi vyuo vya kuwajenga vijana?
Naikumbuka TANU yangu hodari ya vijana wenye kujenga hoja na wazalendo kweli.
Leo hii tumesukuma matumbo mbele zaidi, hakuna uzalendo hata kumwaga damu za watu ni jambo la kawaida
 
Siku ukifanya hivyo na baada ya hapo,Mungu akafanya yake unayempenda akaondoka kabla hata hiyo mitano haijaisha!!
Usiyempenda akaja utafanyaje?
Nae Mungu akambariki akaishi miaka makumi,utayavumilia hayo maumivu kwa miaka hiyo dahali? Na kibaya zaidi hujui maumivu yako yatakoma lini!
Historia iko wazi,huko nyuma taifa LA Israel lilikua likitawaliwa na mwenyezi Mungu kupitia makuhani na wapakwa mafuta wake,watu walichoka kutawaliwa kwa mtindo huu nao wakamuomba Mungu awaache wajitawale wenyewe kupitia wafalme,nae akaruhusu jambo hilo.
Sasa kama watu walichoka kutawaliwa na Muumba wao itakuwaje binaadamu mwenzao?
Binaadamu ameumbwa na hulka ya kutaka mabadiriko na kuchoka mambo Yale Yale.
Ndio maana hata upendo kwa wanandoa hupungua kadiri wanavyo ishi pamoja,upendo wa mwanzo hauwezi kuwa sawa na wa baada ya miaka mitano.
Kuwa makini.
 
umechokozwa boss... usirushe ngumi...[emoji1787][emoji1787]
Kuna mambo yanakera sana Bongo

Hoja ya kuwaangalia wenzetu wamefanya na sisi tufanye kama wao ni hoja dhaifu sana kwa msomi kuisema kama kigezo cha rais kuongezewa muda

Vile vile hoja ya kusema yeye kafanya mambo makubwa kwa muda mchache hakuna wengine walio wenza huo pia ni upungufu wa kufikir

Ila twende mbele turud nyuma kuna mambo bongo yanaumiza sana tena yanakera
 
Kuna mambo yanakera sana Bongo

Hoja ya kuwaangalia wenzetu wamefanya na sisi tufanye kama wao ni hoja dhaifu sana kwa msomi kuisema kama kigezo cha rais kuongezewa muda

Vile vile hoja ya kusema yeye kafanya mambo makubwa kwa muda mchache hakuna wengine walio wenza huo pia ni upungufu wa kufikir

Ila twende mbele turud nyuma kuna mambo bongo yanaumiza sana tena yanakera

Nipo na ww lakn ningependa uendelee zaidi kupambanua mawazo yako kiundani zaid ili ueleweke mbadala wa hayo mawazo uliyoyaona kwa mtoa mada. Nyambua nyambua kidogo mkuu
 
Kupata kiongozi mzuri ni sawa na kupata mke mwema, unabadili badili videmuuuuu, siku ukipata mkali wao unao jumla, unatulia. Kama huyu tuliyempata ni mkali wao, basi aongoze jumla.
 
Kama mwenyekiti anavyojitangaza kwamba hajawahi tokea Rais kama yeye tangu kuumbwa kwa Tz na haitatokea!!!!
 
Kiujumla chadema inahitaji marekebisho makubwa sana ya ndani.kuendelea na watu walewale itawapa shida huko mbeleni...

Huwezi kupambana na changamoto mpya na ukadhani utazikwamua kwa kutumia mbinu zile zile za zamani!!! Wanachadema inabidi walitambue hilo ama sivyo chama kitadumaa zaidi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom