Freeman Mbowe aungwe mkono uchaguzi ndani CHADEMA

Freeman Mbowe aungwe mkono uchaguzi ndani CHADEMA

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Kuna mambo yanajirudia kila wakati mpaka yanachosha. Unapokaribia uchaguzi ndani ya Chadema kuna maneno kuhusu Mbowe lazima uyasikie

– Mbowe anajilipa ruzuku yote. Kateka mali zote za chama. Mbowe anaendesha chama kama ofisi binafsi.n.k

Maneno haya yanajirudia kila msimu wa uchaguzi wa chama hicho.

Tuliyasikia wakati wa Chacha Wangwe. Wakati wa Zitto Kabwe. Sasa Kigogo wa ‘twita’ anayarudia kwa namna ileile. Kwa mwenye akili timamu hii inachosha.

Kama hizi ndiyo propaganda basi hizi ni za kipumbavu. Kichekesho zaidi ni wanaozitumia kushindwa kuelewa kuwa hazina mashiko. Uchaguzi wao ukiisha na haya maneno yanaisha.

Tuwekane sawa kwenye hili. Chama kinachopigania ukombozi au kutaka kushika dola, kikipata kiongozi imara hakimbadilishi ovyoovyo. Hii ni ‘prinsipo’. Yasser Arafat kafa akiwa kiongozi wa PLO kwa miaka mingi kule Palestina.

Dunia nzima, kiongozi wa namna hii huondolewa kwa kushindwa kustawisha chama na si vinginevyo. Huyu ndiye Mbowe.

Ukiwa na kiongozi asiye na msimamo mtaishia kuwa na vyama visivyosikika. Akili za Mbowe, msimamo wake, uchumi wake. Ndiyo yaliyopelekea akute chama kina wabunge watano na sasa wako sabini.

Unamuondoaje? Labda kama huna nia ya kushika dola. Propaganda za kula ruzuku lazima zife kibudu.

Kuna watu wakisikia shamba la Mbowe limeharibiwa na DC wanawaza matembele, nyanya chungu, sukuma wiki, kabeji na matuta ya viazi – wanalifananisha na mashamba ya bibi na babu zao huko Mpwapwa au Malinyi kama siyo Matombo.

Tunatakiwa kumshangaa Mbowe kuacha utajiri chekwa wa familia yake na kuja kuhangaika na siasa huku mitaani na kina Sugu.

Mwanzoni watu walikuwa ‘bize’ na Kigogo huko ‘twitani’. Kuna wakati akataka aniteke kiakili na mimi. Lakini kuanzia kwenye suala la ‘flash’ za ajali ya yule kigogo wa ukweli. Nikaanza kupata shaka. Ni sampuli ya watu wanaoamua kujipa nafuu ya nafsi zao kwa kuandika wanachojisikia.

Lowassa, aliitwa fisadi kila siku. Watu wakachoka kuona mtu mmoja anabebeshwa zigo lote la ufisadi. Kwanini hashtakiwi? Kwanini sasa hafungwi? Maswali yasiyo na jibu yalipelekea ageuke shujaa 2015.

Ndiyo Mbowe, shutuma anazopewa mbona Msajili wa vyama na CAG hawajawahi kusema lolote? Hata wapinzani wa Mbowe wamechoshwa nazo.

Tufanye siasa safi, zenye tija na manufaa kwa nchi. Hizi za ovyo ni upuuzi.

#Mbowe Tano Tena#
 
Hakika kaka wote wanao kesha wakipiga kelele za Mbowe ni vibaraka na maadui wa cdm huo ndiyo ukweli tusimame na mwenyekiti wetu ili chama kisonge mbele
 
Attachments

  • FB_IMG_1495969323891.jpeg
    FB_IMG_1495969323891.jpeg
    20.4 KB · Views: 73
kwani uchaguzi nafasi ya mwenyekiti lini? Utaratibu ukoje? Je wagombea wa nafasi ya mwenyekiti lini wanaanza chukua fomu? Je fomu ni bei gani? Kurejesha fomu lini? Maana hizo ndo sifa za demokrasia pia Mkuu.
Uchaguzi ni mwaka huu December.Taratibu nyingine tutazitoa baada ya vikao vya Kamati Kuu
 
Mbona hatujawahi kuwasikia mnamuuliza Lyatonga kwamba uchaguzi wanafanya lini?
kwani uchaguzi nafasi ya mwenyekiti lini? Utaratibu ukoje? Je wagombea wa nafasi ya mwenyekiti lini wanaanza chukua fomu? Je fomu ni bei gani? Kurejesha fomu lini? Maana hizo ndo sifa za demokrasia pia Mkuu.
 
Hawawezi kutupangia na hizo chokochoko zinatoka lumumba na kijitonyama
Kabisa mkuu.Ushindi wa Mbowe mwaka huu utakuwa ni mkubwa mpaka maadui zetu wataingia mvunguni
 
Haahaa hongereni, maana hata wanaccm wanadai hivohivo kwamba yeyote anayempinga magu Ni msaliti au katumwa na wapinzani.
Nakubaliana na CCM kabisa.Maswala ya Mwenyekiti wa CCM inawahusu nini upinzani? Waachiwe wanachama wa CCM waamue juu ya Mkiti wanayemtaka
 
Tetea upendavyo lakini ukweli ni kuwa muda wa Mbowe kuendelea kukaa madarakani umepita. Ni kipi ambacho Mbowe kwa sasa unaweza sema anakifanya hapo cdm ambacho kinampa uhalali wa kubaki kama mwenyekiti? Kama ni kura zinaporwa kama kawaida tena kwa sasa ni zaidi. Kama ni viongozi wamehama kibao kwenda ccm, kama ni nguvu ya umma hana uwezo wa kuitisha maana hadi tunavyoongea ana kesi ya kubambikiwa. Ukimuacha Lissu ambaye sababu yake ya kuvuliwa ubunge inafahamika ni mkakati wa rais huku akiwa matibabu, je ni kipi kilimshinda kumuhoji Nassari kutokuhudhuria bunge mpaka akafutwa ubunge?

Ni kweli ccm chini ya Magufuli anaihujumu cdm, lakini tuna uwezo wa kujua ipi ni hujuma dhidi ya cdm, na kupi ni kung'ang'ania madaraka kwa Mbowe. Sisi ni washabiki wa cdm na wanachama na tunaijali cdm kama taasisi, ila hatuna ujinga wa kung'ang'ania kiongozi ambaye tunaona kabisa uwezo wake umegota na anakirudisha chama nyuma. Historia ya Mbowe ndani ya cdm isiwe kigezo cha kuendelea kuwa mwenyekiti, na wala hujuma za rais dhidi ya cdm isiwe kichaka cha Mbowe kung'ang'ania madaraka.
 
Mbowe Tano Tena
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom