*Na Kwinyara Kwintara*
Mbunge wa Ndanda ndugu Cecil David Mwambe, ameweka wazi nia yake ya kuwania uenyekiti ndani ya CHADEMA. Kwanza nampongeza na ni haki yake kikatiba ndani ya misingi ya CHADEMA.
Sitoandika mambo mengi kuhusiana na Mh. Huyu ila nataka niweke wazi mambo muhimu tu ya angalizo.
Kwa wenye kumbukumbu nzuri kabisa Cecil Mwambe ni miongoni mwa Wabunge na wanachama wa CHADEMA waliowahi kufika bei ya kununulika na CCM ikiwa chini ya serikali inayoongozwa na Magufuli.
Mwambe alikata tuhuma hizo kujisafisha lakini dhamira ya Mwambe ni kuifanyia kazi CCM. Mwambe amekubali kupokea pesa kutoka CCM ili kuendesha kampeni za kuwania uenyekiti ndani ya CHADEMA, Mwambe amekubali kufanya kazi na idara ya usalama kitengo cha siasa Ikulu kinachodhamiria kumuondoa Mbowe kwenye uenyeketi wa CHADEMA kikiamini uhai mkubwa wa CHADEMA ni mwenyekiti na katibu wa chama husika.
Vikao kadhaa vimefanyika kumuhadaa Mwambe asihamie CCM kwanza maana watamtumia akiwa ndani ya CHADEMA kuiua CHADEMA. Cecil Mwambe ni wakala wa kuvujisha siri nyingi za CHADEMA kwa serikali na CCM, amekua miongoni mwa wale wabunge waliodai kupinga kukichangia chama chao kikatiba.
Kwa ufupi Mwambe ni wakala na pando la CCM ndani ya CHADEMA,wenye masikio na wasikie, na kama mnataka uhai wa CHADEMA, CECIL DAVID MWAMBE asipewe hata nafasi ya kujaza fomu, Msajili na Serikali wanamtaka Mwambe awe Mwenyekiti wa CHADEMA na watampitisha kwa nguvu kama ilivyokua kwa Lipumba CUF ili asimamie dhamira ya CCM kuiua CHADEMA.
Cecil D. Mwambe hafai kua Mwenyekiti wa CHADEMA, anapwaya na ni pando la CCM ndani ya CHADEMA kwasasa.