Wanyambo wana msemo wao usemao "mchawi mpe mwanao amlee"... Tumeona mwenyekiti wa taifa CHADEMA ndugu Freeman Mbowe, akiwa na mafanikio makubwa kama mwenyekiti wa chama cha upinzani nchini. Chini ya utawala wake ameongeza wabunge wengi, madiwani wengi na wenyeviti wa mitaa wa kutosha. Kwa mafanikio hayo CHADEMA wameona 'potential' yake na kuamua awaongoze kwa miaka kumi na tano, na bado wanataka kumpa mitano mingine.
Vivyo hivyo kwa CCM kwanini wasibadili katiba yao ngazi ya chama, pia ngazi ya nchi kwakua wapo wengi bungeni na ndio wanaongoza serikali. Kufanya marekebisho ya kuondoa ukomo wa mtu kugombea na kutawala hasa akiwa ni mtu mchapakazi, muadilifu, na mleta maendeleo.
Nchini China, xhi ji ping ameongezewa kutawala nchi hiyo mpaka pale atapochoka, yaani kifupi anatawala maisha yake yote. Mnataka tumzungumzie bwana Ping kuhusu maendeleo ya China? Tutakesha..! Nchini Korea kaskazini, urusi, Germany chini ya counsellor angel markel, UK chini ya Queen Elizabeth, mfalme wa Spain, Rwanda, Uganda nk. Kama nchi hizo wameweza Tanzania tutakwama wapi?
Demokrasia sio lazima kila mtu atawale, ni suala la kukubaliana Fulani atutawale kwa kupindi Fulani. Kama CHADEMA tulivyokubaliana.
Ndani ya miaka isiyozidi minne ya huyu jamaa JPM, tumeshuhudia uthubutu wa hali ya juu ambao tukiweka pembeni unafiki, na ubinafsi tutakubaliana the guy anahitaji muda zaidi kutuvusha tulipo.
Miradi mikubwa ya ujenzi kama vile SGR, stigliers gorge, madaraja, barabara, zahanati, elimu bure, nk. Ndani ya miaka minne tu, ifike mahali tuwe na shukrani japokua kodi ni zetu, maana tunajua wengine ni nini walifanyia hizo kodi.
Mie binafsi nna ugonjwa wa kupenda vitu vizuri, kwahyo kwenye siasa mtu anayepiga kazi ndo nampenda, suala la chama kwangu ni option mamba 5, nne za kwanza ni uthubutu, uchapaji kazi, kujituma, na elimu ya mtu. Ndio maana naunga mkono mbowe kuongoza CHADEMA hata miaka 50, pia Magufuli kuongoza hata miaka 30.
The irreplaceable