-Mbowe ni Mfanyabiashara anayelipa kodi kwa Mujibu wa Sheria
-Kuna kasumba mbaya imeibuka inayojenga Taswira hasi kwa kila mfanyabiashara.Hatuwezi kujenga Taifa kubwa kwa mentality hizi
Sera ya CHADEMA kulingana na Mrengo wetu kiitikadi ni kuwa Mazingira mazuri ya Biashara na mfumo wa soko uendeshe uchumi ambapo individual efforts zinakua rewarded.
Umaskini si jambo la kujivunia.CHADEMA kimeweka msimamo wake very Clear.Kuweka mazingira mazuri ya kibiashara na kukuza uchumi kupitia uboreshaji wa maisha ya mtu mmoja mmoja.Tungefuata sera sahihi za kiuchumi na kibiashara basi nchi hii ingekua na mabilionea wengi zaidi na turnover ya wafanyabiashara tunaowaona leo hii ingekua tofauti na turnover zao kwa sasa.
Leo hii kutokana na kuwa na sera ya 'Kuchanganyikiwa" ya kiuchumi na kijamii hatuwezi hata kuweka estimation ya kuwa tutakua na Mamilionea au mabilionea wangapi in 5-15 years baadae.Tunapiga ramli kama waganga wa Kienyeji badala ya scientific forecasting
Hizi mentality za Kimaskini tunazoona zimejengwa kwa muda mrefu na kupaliliwa na mfumo na zinajenga chuki kwa kila mfanyabiashara lakini cha ajabu wanasiasa wezi wezi na waroho wa mali za Umma wanakua celebrated na kushangiliwa kuwa fulani ni Noma.Tunajenga taifa dogo la ovyo lenye uwezo wa kupiga reverse kimaendeleo tu na sio zaidi ya hapo.
Kuhusu Malicious intent kwa kuandika story zenye malengo mabaya kisiasa ni.jambo la hatari sana
Raia Mwema nimekua nikiliheshimu na hadi sasa nawapa benefit of doubt ili niwe rational.
Ukweli wa jambo lolote ni suala la Muda.Sidhani sasa kama Raia Mwema wamebadili dimension ya Legacy yao waliojenga kwa muda Mrefu kwa kuamua kwenda Gutter na irresponsible Journalism.
Jenerali Ulimwengu ana heshima kubwa nchini kitaaluma na katika weledi.Sidhani kama anaweza kuruhusu mambo haya
Wakati huo huo hatuwezi kupuuza kila lisemwalo maana kuna mambo mengi.Uchaguzi ndani ya CHADEMA unakaribia,Hoja ya Kuficha Mabilioni nje inaweza kuwa diluted kwa mbinu mbalimbali na pia kwa kuwa kuna wanasiasa wanahusika na hoja hii wanaweza kuitumia kisiasa kujinufaisha na kuwalenga maadui zao kwa sababu wanazozijua ambazo no doubt ni za Kisiasa
Najua wanapita wahariri hapa,Sasa sote tujiulize ;
Je,Tunapokubali kutumia vyombo vyetu kwa maslahi ya kisiasa ya watu wachache tunaitendea haki jamii?Je,misingi ya Demokrasia na mhimili wa media tunautendea haki?Tunakuza au tunafifisha tasnia ya Habari?