Naomba kutofautiana, box to box midfield, ni kiungo anayeweza kudefend na kuongoza mashambulizi. Kwa maana kuna aina mbili za viungo, mkabaji (no.6) na mshambuliaji (no.8).
Katika hao wapo wanaofanya moja tu ya hayo, either kukaba tu au kushambulia tu, Makelele alikua mkabaji tu, wakati kiungo kama Zizou alikua mshambuliaji tu,
Sasa box to box midfield anakua na uwezo wa kufanya yote haya, anaprotect beki zake na team ikianza kushambulia, unamkuta kwenye box (18) ya wapinzani anashambulia. Kiungo wa namna hii ni kina Yaya Toure, Pirlo, Ramires, Shweinsteiger, hata Lampard kwa msimu ulioisha alikua anacheza sana kwenye hii role, Gerrard, Xavi, Alonso, Khedira, Vidal n.k
Makelele hakuwahi kuwa box to box midfield, in fact ilikua nadra sana hata kumuona akivuka mstari wa katikati kwenda kwenye half ya upinzani, yeye alikua na kazi moja tu, kukaba. Mikel hata yeye hawezi kwa sababu mzito sana. Ndio maana wachezaji kama hawa ni nadra sana kuwaona wanafunga magoli