Follow Me If You Can!

Follow Me If You Can!

Ni ujinga kuona kila kitu anachofanya mwenzio ni cha kijinga!

Pia ni ujinga kuona ujinga aliouandika mwingine sio ujinga mzuri kama wako! Ina maana we ndio mjinga zaidi.

Ni ujinga kumwonea wivu rafiki yako kwa kupata kitu kizuri, tena na wewe unataka hichohicho badala ya kutafuta kingine!

Ni ujinga kukaa unachangia ujinga JF badala ya kufanya mambo ya maana!
 
Ni ujinga kukosea kitu ukasema kwa sauti, "Mi ni mjinga kweli", wakati akikwambia mtu mwingine kwa kosa lile lile kuwa we ni mjinga unakasirika.
 
Ni ujing kuota unakojoa kweli ukalimwaga kitandan.. Ni ujinga mikojo imekubana alaf unaendelea kuibana eti kisa uvivu wa kwenda chooni..Ni ujinga mim kuendelea kuandika huu ujinga alaf nachekelea
 
Ni ujinga kujenga jumba imara lnalodumu kwa miaka mia wakat we utaish miaka 30!
 
Ujinga ni kukaa mbele kwa dereva halafu unamwambia konda shusha tena kwa sauti kubwa...anayesimamisha gari c upo nae hapo...

mkuu hii ishanitokea wala si ujinga, nilimwambia dereva ashushe akanijibu si umwambie konda. Nilimshangaa hv ni nani mwenye klachi na breki kama siyo yeye!!
 
mkuu hii ishanitokea wala si ujinga, nilimwambia dereva ashushe akanijibu si umwambie konda. Nilimshangaa hv ni nani mwenye klachi na breki kama siyo yeye!!
Hapo driver ndo mjinga.
 
Ni ujinga kufungua duka la kupiga tattoo sudani kusini.
 
ni ujinga kufikiri kila mwenye koti jeupe daktali kumbe wengine wauza bucha
 
Ni ujinga kuandika sms huku unayatamka maandish unayoandka.
 
Ni ujinga kuoga alafu ukimaliza unajifuta na kuchafua taulo.
 
Ni ujinga mtu kukupa habari za msiba unaanza kuhamaki kwa kusema “Waaoooo....”
 
Ni ujinga kumkaribisha mgeni na kumwambia;"jisikie uko nyumbani kwako",akiingia chumbani je?
 
ni ujinga kumtawala mtu kwa miaka 50 na bado unamdanganya anakubali,ni ujinga kuendelea kumwongoza mtu ambaye hata ukimtendea ndivyosivyo haulizi
 
Ni ujinga kuweka kufuli kuuubwa la shaba kwenye mlango wa mbao.
 
Ni ujinga kila mfuko laini wa plastic kuuita rambo!
 
ni ujinga kutamka masaburi wakati hujiu maana yake
 
Back
Top Bottom